Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Muimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili nchini, Bahati Bukuku, amekosoa vikali ushirikiano wa kimuziki kati ya waimbaji wa Injili na wasanii wa muziki wa dunia (secular music), kauli inayojiri mara baada ya mwimbaji mwenzake wa nyimbo za dini, Joel Lwaga, kuachia wimbo wa pamoja na msanii nyota wa Bongo Flava, Diamond Platnumz.
Bukuku ameweka wazi msimamo wake nchini Tanzania kuwa kwa mujibu wa imani yake na misingi ya Maandiko Matakatifu ya Biblia, si sahihi kwa mwimbaji wa Injili kufanya kazi na wasanii wa muziki wa dunia.
Elezo lake linasisitiza kuwa mwimbaji wa Injili tayari ni mhubiri wa neno la Mungu, hivyo kulingana na maandiko, hatakiwi kuchangamana na mambo yaliyo nje ya misingi ya kiroho.
Akifafanua zaidi jinsi anavyouchukulia ushirikiano huo, Bukuku alibainisha kuwa ingawa Diamond Platnumz si mtu mbaya wala adui, njia anazopita kulingana na Biblia si za kiroho.
Aliongeza kuwa mwimbaji wa kweli wa dini anapaswa kutanguliza kumtumikia Mungu na kuwajali wanaowahudumia badala ya kuangalia maslahi binafsi, msimamo ambao umeendelea kuzua debate kubwa miongoni mwa wadau wa muziki wa Injili na burudani nchini.
"Ukishakuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili tayari wewe ni mhubiri wa Injili, pia hutakiwi kuchangamana na giza... Unapokuwa mwimbaji wa kiroho inatakiwa usijiangalie wewe, mwangalie MUNGU unayemtumikia na unaowatumikia pia," alisema Bahati Bukuku.