Mimi sio extremist ila naongelea mipaka na kuheshimu imani ya watu wengine , kwa mfano : wewe dini sio yako ukaribishwe ili iweje na ile sherehe ni ya kidini ?
Unajua , mimi sio mnafiki kwamba nikuite kwenye jambo ambalo halikuhusu ...Tutaendelea kushirikiana ila sio kwenye mambo ya imani kwani tuko tofauti tayari ..Mbona wewe haukaribishwi kwenye ngoma na mila za makabila mengine , sijakuona mhaya anamualika mchaga kwenye ngoma zake au shughuli za tamaduni yake .
Naongea ukweli si unafiki , nikikukaribisha labda kuna kipi kipya ? kama wali tunakula kila siku hata wewe unakula , siku hiyo waacheni wahusika ...Mfano mwingine; wewe haufungi eti nikuite ule futari wakati futari ni maalumu kwa waliofunga . Mna tabia hiyo ya kujifanya wema ila tunawajuab, hapa Tanga kuna kanisa wanasema kabisa watu wasile kwa waislamu , mtalishwa majini hasa katika maulidi , siwezi kupingana nao kwa vile ni kinyume cha imani yao ..Uislamu ni uwazi, unachanwa makav laiv sio nyie waoga kwa kujifanya wema .
Ukijua mipaka yako utaishi na watu vizuri . kwa hiyo , kama sikukuu yako umepika ngurwe mimi nije kule kwa kusherehekea na wewe kisa ni sikukuu yako. Ukija kama mgeni kwangu utakula ila sikukuu ya kidini hapana siwezi kuingilia imani yako , nina ndugu wakristo wanakula kwangu kipindi wakija likizo ila kwenye sikukuu siwezi kuingilia imani yao , eti niwaite waje kusherehea kivipi yaani ?