secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,984
- 51,055
Huyo wa kuingilia penzi letu ni yupi?Baelezee papi 👌🏽
Na atakuja kuliharibu kwa gia ipi?
Yeah, Nikiwa nawe basi am so hapi.
Huyo wa kuingilia penzi letu ni yupi?Baelezee papi 👌🏽
Hayupo nakwambiaa!!🤣Huyo wa kuingilia penzi letu ni yupi?
Na atakuja kuliharibu kwa gia ipi?
Yeah, Nikiwa nawe basi am so hapi.
😁😁😁, meno yangu yote 32 inje inje yaani!Hayupo nakwambiaa!!🤣
Vogue, 😂😂😂Na jumapili tupo nao Supadome masaki
Kwani Bahati alivyo imba dunia haina huruma
Mbn sikuona sehemu akiomba wachungaji ama waamini wenzie msaada zaidi ya kuwalaumu mawifi na mashemeji mwishoni kaangukia kwa Dokita wa gari linalokula mafuta
cc Seran secretarybird BICHWA KOMWE
😂😂😂ingawa Joel anaimba vizuri pia macho makubwa sana.
Hujamuelewa...Mipaka ya kidini ipo tukiongea sisi , utasikia ubaguzi ..Anayo haki ya kusema hivyo , hata sisi si ruhusu kusherehekea chrismass kwa kula chakula au kushirikia sherehe, kushirikiana katika mambo ya ibada za kidini haitakiwi ila mambo mengine ya kijamii fresh .
Kuna muda , sio mnapiga kelele kila kitu kina mipaka yake .Akiongea shekhe hapo , utasikia ni ubaguzi wa kidini au chuki za kidini ,..Ukweli ni huko , utaamua mwenyewe umeze au uteme.
Mimi binafsi , nikiitwa katika sherehe ya kdini ya kikristo kama sikukuu siendi kwa sababu nawaheshimu imani yao , na mimi siwezi kumkaribisha kwenye sikuu ya dini yenu naona kama namvunjia heshima ; hatokuwa comfortable .
Tuchunge mipaka ya kidini ni heshima sio ubaguzi .!
Wewe hujaelewa , hiyo ni mipaka ya kidini , nyimbo za dini na kidunia haziendani ..Choyo kipi , wali wa siku moja ukane dini yako ya miaka yote , mipaka ya kidini ni muhimu sio chuki ila ni kuheshimu imani ya mtu.Hujamuelewa...
Hajasema hivyo kwasababu Mond ni muislamu...
Angesema hivyo hata kama Lwanga angeshirikiana na Nandy...
Halafu...
Wewe kunikaribisha Idd el fitri unavunja sheria gani ya dini ndugu?
Punguza choyo.
Ebu tuachane na mambo ya kuelewa tujikite kwenye msosi wa sikukuu...Wewe hujaelewa , hiyo ni mipaka ya kidini , nyimbo za dini na kidunia haziendani ..Choyo kipi , wali wa siku moja ukane dini yako ya miaka yote , mipaka ya kidini ni muhimu sio chuki ila ni kuheshimu imani ya mtu.
Apambane na Hali yakeMuimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili nchini, Bahati Bukuku, amekosoa vikali ushirikiano wa kimuziki kati ya waimbaji wa Injili na wasanii wa muziki wa dunia (secular music), kauli inayojiri mara baada ya mwimbaji mwenzake wa nyimbo za dini, Joel Lwaga, kuachia wimbo wa pamoja na msanii nyota wa Bongo Flava, Diamond Platnumz.
Bukuku ameweka wazi msimamo wake nchini Tanzania kuwa kwa mujibu wa imani yake na misingi ya Maandiko Matakatifu ya Biblia, si sahihi kwa mwimbaji wa Injili kufanya kazi na wasanii wa muziki wa dunia.
Elezo lake linasisitiza kuwa mwimbaji wa Injili tayari ni mhubiri wa neno la Mungu, hivyo kulingana na maandiko, hatakiwi kuchangamana na mambo yaliyo nje ya misingi ya kiroho.
Akifafanua zaidi jinsi anavyouchukulia ushirikiano huo, Bukuku alibainisha kuwa ingawa Diamond Platnumz si mtu mbaya wala adui, njia anazopita kulingana na Biblia si za kiroho.
Aliongeza kuwa mwimbaji wa kweli wa dini anapaswa kutanguliza kumtumikia Mungu na kuwajali wanaowahudumia badala ya kuangalia maslahi binafsi, msimamo ambao umeendelea kuzua debate kubwa miongoni mwa wadau wa muziki wa Injili na burudani nchini.
"Ukishakuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili tayari wewe ni mhubiri wa Injili, pia hutakiwi kuchangamana na giza... Unapokuwa mwimbaji wa kiroho inatakiwa usijiangalie wewe, mwangalie MUNGU unayemtumikia na unaowatumikia pia," alisema Bahati Bukuku.
View attachment 3677375
View attachment 3677373