KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Namba zetu za maambukizi na vifo hadi sasa vinaelekea kuwa tofauti na zile za wenzetu walioko kwenye nchi za baridi.
Ushahidi unaanza kupatikana sasa kueleza tofauti hizi kati ya nchi zetu na za hawa wengine.
Ingawa pamekuwepo na dhana ya kuhusisha joto, unyevunyevu na mwanga katika kupungua kwa kasi ya maenezi ya coronavirus, dhana hii bado ilikuwa haijapata ushahidi wa kimaabara kuhusisha hali hizo na kupunguza kasi ya kuenea kwa coronavirus.
Sasa uchunguzi huo umefanyika na inabainishwa wazi kwamba corona anadhurika haraka anapokutana na mazingira hayo ya joto, mwanga na unyevunyevu.
Huu utakuwa ni ushahidi wa kujitosheleza kuhusu bahati yetu ya kutokuwa na kasi ya maambukizi kama ile tuliyoiona Italy, Uingereza, USA na kwingineko.
Corona anadhurika haraka, kwa hiyo maambukizi yanapungua. Hii haina maana kwamba maambukizi hayatakuwepo kabisa. Maambukizi yatakuwepo kama haya tuliyokwishayashuhudia, lakini kasi yake haitafikia ile inayoonekana kwenye nchi za baridi.
Maana ya utafiti huo ni kwamba, sisi tukiongeza juhudi ya kuongeza kuzuia maambukizi, kama kunawa mikono, barakoa na kutokaribiana zaidi, nafasi yetu ya kuzuia maambukizi na vifo inaweza kuwa kubwa zaidi.
Hii ina maana, Mungu, alishasikiliza sala zetu kuhusu ugonjwa huu, ndiyo maana katuweka hapa tulipo.
Tuzidi kusali/kuswali.
Najua utataka nikupe source ya utafiti huo. Vuta subira. Kwa sasa nikupe tu kwamba tafiti za aina hii zinaendelea India, USA na kwingineko.
Hata sisi hapa tungeweza kufanya; aaah, acha tupige siasa kwanza. Kwa sababu siasa inalipa!