KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
- Thread starter
- #41
Hapo pa kupiga amri ndipo panapofanyiwa kazi mkuu na tafiti mbalimbali zinazoendelea, mojawapo ikiwa uthibitisho wa kimaabara kuwa coronavirus anaathiriwa na joto, mionzi na unyevunyevu, kwa pamoja. Hii sio ramli tena, bali ni jambo lililothibitishwa kwa utafiti.Ipe muda muda tu, itathibitisha uhalisia wake, hamna anayeijua mpaka sasa zaidi ya kupiga ramli.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa basi, hii haina maana kwamba mazingira hayo ndio yatakuwa tegemeo la moja kwa moja kuiondoa coronavirus; hapana. Hakuna utafiti uliofikia hitimisho hilo, ila itaeleweka sasa kwamba, hali ya joto/unevunyevu/mwanga ni sehemu mhimu katika kupunguza nguvu ya coronavirus kusambaa na kufanya maambukizi.
Maana ya hili ni kwamba ni lazima njia nyingine za kinga zitumike sambamba ili kuongeza kinga zaidi, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kutumia barakoa na hata kupata chanjo yenyewe.