Bahati yetu ni Jua, Unyevunyevu (humidity) na Joto - Corona hatambi

Ipe muda muda tu, itathibitisha uhalisia wake, hamna anayeijua mpaka sasa zaidi ya kupiga ramli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo pa kupiga amri ndipo panapofanyiwa kazi mkuu na tafiti mbalimbali zinazoendelea, mojawapo ikiwa uthibitisho wa kimaabara kuwa coronavirus anaathiriwa na joto, mionzi na unyevunyevu, kwa pamoja. Hii sio ramli tena, bali ni jambo lililothibitishwa kwa utafiti.

Sasa basi, hii haina maana kwamba mazingira hayo ndio yatakuwa tegemeo la moja kwa moja kuiondoa coronavirus; hapana. Hakuna utafiti uliofikia hitimisho hilo, ila itaeleweka sasa kwamba, hali ya joto/unevunyevu/mwanga ni sehemu mhimu katika kupunguza nguvu ya coronavirus kusambaa na kufanya maambukizi.
Maana ya hili ni kwamba ni lazima njia nyingine za kinga zitumike sambamba ili kuongeza kinga zaidi, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kutumia barakoa na hata kupata chanjo yenyewe.
 
Ninakubaliana nawe juu ya hili. Baadhi ya nchi ni swala la kutokuwa na uwezo wa kupima na kutoa takwimu kamilifu. Hawa wangekuwa na uwezo takwimu zao kidogo zingeonyesha uhalisia wa hali iliyopo kwenye nchi hizo.

Baadhi yetu, kama Tanzania, sisi tunasukumwa na kutaka tuonekane hatuathiriki. Namba zetu tunataka zionekane nzuri tu hata kama tunajua kwamba hali sivyo hivyo. Hili ni tatizo.

Lakini pamoja na kutokuwa na uwezo wa kupata takwimu sahihi, kinachozungumziwa kwenye mada hii ni utafiti unaoonyesha pasipo shaka kwamba hali ya joto/unyevunyevu/mwanga, mazingira haya yanapunguza wingi wa coronavirus, kwa hiyo kutoa mwanya zaidi wa kupunguza kasi ya maambukizi. Hali hiyo haizuii moja kwa moja coronavirus kuendelea kuwepo na kusambaa, lakini kasi yake inapunguzwa.
Kwa hiyo, njia za ziada, kama kunawa mikono,kuvaa barakoa na njia zingine mhimu zikitumika sambamba na mazingira hayo, hali ya maambukizi katika nchi hizi kidogo inakuwa si sawa na hali za milipuko iliyokwishaonekana sehemu mbalimbali duniani..

Kwa hiyo juhudi inabidi ziongezwe katika njia za kukinga ili maambukizi yaendelee kupungua zaidi.

Na hapo hapo, kumbuka kwamba watu wengi wamekwishaambukizwa tayari, hata wengine wasioonyesha dalili za ugonjwa kabisa.

Kwa hiyo ugonjwa utaendelea kuwepo, ila tunaweza kuuhimiri zaidi kwa kuongeza umakini katika njia za kinga, huku mazingira yetu ya joto/unyevunyevu/mwanga navyo vikisaidia.
 
Mpuuzi wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uongo Philippine ni kiangaza kwa sasa man's take ni kipindi cha baridi
 
South Africa IPO kwenye tropic ya cancer kama Tanzania but eneo lake limeathiriwa na makutano ya bahari na kutengeneza baridi Kali pale port Elizabeth ,unajifanya mjanja kumbe hujui chochote
 
South Africa IPO kwenye tropic ya cancer kama Tanzania but eneo lake limeathiriwa na makutano ya bahari na kutengeneza baridi Kali pale port Elizabeth ,unajifanya mjanja kumbe hujui chochote
kwa Hiyo korona inapiga Port Elizabeth huko kwingine mambo shwari?
 
Weka source basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna suala la watu weupe kuathiriwa pakubwa na magonjwa ya mafua, tangu enzi za ukoloni na utumwa watu weuoe walidondoshwa kwa wingi sana na mafua aina ya Influenza, wacha watafiti watupe majibu.
 

Mimi naona lockdown ni bora kwa kupunguza maambukizi lakini wengine walioiona lockdowns wameanza kukasirika na kuvunja utaratibu
Njaa kitu kingine Mkuu
USA na kila kitu wameanza kutoka kwa maelfu nje tena wamebeba na bunduki kabisa kujihami na jeshi


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

Kwahiyo hapa walengwa ni waKristo [kusali] na waIslam [kuwali] . Je sisi tunaoabudu miti na mawe makubwa makubwa hata yale Mheshimiwa fulani aliandika yeye ndio Rais mbona tumetengwa ?.Bora niurejee uraia wangu wa zamani kama huku kwenu mnadharau dini zetu za mabab tangu enzi na enzi.
 
South Africa IPO kwenye tropic ya cancer kama Tanzania but eneo lake limeathiriwa na makutano ya bahari na kutengeneza baridi Kali pale port Elizabeth ,unajifanya mjanja kumbe hujui chochote

Rudia ‘geography’ yako vizuri.South Africa ipo kwenye Tropic ya Capricorn na siyo cancer
 
South Africa wanazika??.wamezika wangapi out of 2000 ambao wako positive?
 
Naamini tz wagonjwa wa Corona Ni wengi Sana hata 500 wanafika.

Sema hatupimi na tunazidi kuambukizana. Na lockdown imechelewa tumeshaambukizana vya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…