Bajeti 2021/22: Kodi ya uzalendo ni kaa la moto. Kila laini ya simu itakatwa Sh. 100 kila siku

Mnapata shida sana si nendeni nchi jirani tu mchukue laini za simu kama mimi sasa hivi natumia sim kadi kutoka nchi mbili tofauti na zote zinafanya kazi vizuri tu.
 
Bro unaelewa kweli.....

""Yoote haya yameshindwa kuwa vyanzo bora vya kodi hadi wanakuja kuchukua Kodi ya laini? Tena sh 100/= kwa siku??!!!"""

Hiki ndio CHANZO KIPYA BROO.

#YNWA
 
Yaah..Kwa hilo nitaunga mkono... mbunge atakayeona mshahara ni mdogo aachie wengine, wako wengi tena wenye uwezo na wengine wasomi mtaani ambao wako tayari kutumikia wananchi, kwa mshahara unaofanana na nchi yetu maskini, na sio haya maposho na mishahara kufuru' wanayolipwa kwa sasa hawa wabunge wasio na tija...
Subirini mi niingie ikulu!!nitashusha mishahara ya wabunge!kufikia robo ya wanaochukua sasa!!Hapo nita expose uzalendo wao!!!
 
Zungu amependekeza iyo Kodi,anajua ye Hana muda mrefu huenda sir God akamuitaji, kwaiyo Hana Cha kupoteza
 
Wala kodi wanalipa hiyo percentage lakini sii u aona walivyo fanya nchini mwao...hela inatumika ipasavyo. Elimu bure mpaka chuo kikuu. Health care ya ukweli, barabara za ukweli.

Tatizo sio kulipa kodi tatizo hiyo hela inatumikaje
Kweli kabisa, tatizo linakuja kwa serikali kujenga ' confidence' Kwa walipa kodi kuwa na moyo wa kulipa zaidi, watakavyo ona matumizi mazuri/ faida zinazopatikana kutokana na kodi yao. Sio kuona matumizi mabovu na mengine yasio ya lazima kwa pesa zao... mfano wa kama hilo jengo la BOT lilifunguliwa lilijumuisha mpaka na 'Ghym ya mazoezi' sijui kwa wafanyakazi, ambao kiuhalisia kulingana na mishahara yao mizuri, bado walikuwa na uwezo wa kutumia Ghym nyingine tu za kawaida na pia kuongeza mapato sekta binafsi.... nafikiri project zetu kwa nchi maskini' zijikite zaidi kuhakikisha' Value for money' and not for ' prestige'....
 
Wala kodi wanalipa hiyo percentage lakini sii u aona walivyo fanya nchini mwao...hela inatumika ipasavyo. Elimu bure mpaka chuo kikuu. Health care ya ukweli, barabara za ukweli.

Tatizo sio kulipa kodi tatizo hiyo hela inatumikaje
Ikikusanywa tu pale wizara ya fedha wanaigawana chini ya kiongozi wao Mwigulu, na hakuna cha kuwafanya
 
Tatizo wenye mamlaka hawajali watu wa hali ya chini, ndio maana sehemu zao za kazi wanaweka na viburudisho vyao kana kwamba ni jengo la starehe
 
Mbona imeandikwa vizuri kuwa utakatwa kutokana na unavyoweka vocha

Mtoa mada acha upotoshaji
Kuwa ukiweka vocha ndo wanapora hiyo 100?... Au hujaweka vocha wiki wanakata hiyo 700 baada ya kuweka ka buku?
 
Nisipo weka vocha kwa kwa miezi miwili inamaana nikija kuweka baada ya hiyo 2 months watakata tsh 100 *60 days?
 
Huu ni ukosefu wa ubunifu wa hali ya juu.

Hivi mtu inabidi akatwe kodi ngapi kwenye mambo ya simu? , mbona kuna kodi nyingi sana mtu tayari anakatwa pindi akitumia simu yake kwa ajili ya data au mawasiliano ya kawaida?

Huu ni uporaji na siyo kodi hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…