Napoleone
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 10,087
- 16,036
Sometime natetea nchi yangu ila inafika mahala nasema dah...hiv kwel kama nchi tunashindwa kujikwamua ila kwa kukamua wnaanch had damu...hiv hao officials wa serikal na wengneo wanaolipana 11m++++...wao mbona wanachkua hela nying sana jaman..kwa kaz gani...dah.anyway...yaan mnakata watu kwenye line za simuMapendekezo ya bajeti ya 2021/2022 ni kwamba moja ya vyanzo vya fedha iwe ni kodi ya laini za simu.
Kila laini ya simu kwa mujibu wa mapendekezo yaliyosomwa na waziri wa fedha itakatwa kati ya Tshs 10/= mpk Tshs 100/= kwa kila siku. Bila kusahau VAT na makato mengine yaliyokuwepo yataendelea.
Yaani wabunge ndiyo wataamuua iwe kiasi gani. Wakiamua tukatwe Tshs 10/= sawa wakiamua Tshs 80/= sawa ama wakiamua Tshs 100/= sawa. Kwa kifupi ni kwamba wabunge watapendekeza kiwango cha kutoza kisichopungua Tshs 10/= lkn pia hakitazidi Tshs 100/=.
Kwa kia siku, haijalishi mtumiaji anaumwa, yuko mahabusu, yuko labour, anauguza ama hatumii hiyo laini atakatwa hicho kiasi.
Ukiweka buku, kabla hujapiga ama hujanunua kifurushi wanakata Tshs 100 yao bila kusahau VAT. Kama hujakatwa kwa muda wa wiki 2 kwasabb hujatumia laini kwa wiki hizo 2 na laini ilikuwa haina kifurush chochote Wala mobile money, basi ukiweka buku yote wanachukuwa na bado unakuwa na deni la Tshs 400/= pamoja na VAT.
Maana yake kwa kutotumia laini wiki 2 (siku 14) unakuwa na deni la Tshs 100/= × 14 = 1,400/=.
Usipoitumia laini kwa wiki 3 ni bora ukasajiri nyingine tu.
Hiyo ndiyo Kodi ya uzalendo aliyoipigia kelele mbunge Zungu na kukubaliwa na waziri Mwigulu.
Tuna mali chungu nzima:
- Madini ya kila aina,
- Gesi za kila aina, mpk Helium, .
- Wanyama pori,
- Mbuga za wanyama,
- Misitu,
- Bahari
- Bandari,
- Mafuta,
- Makaa ya mawe,
- Mlima mrefu kuliko yote Afrika
Yoote haya yameshindwa kuwa vyanzo bora vya kodi hadi wanakuja kuchukua Kodi ya laini? Tena sh 100/= kwa siku?
Au hii imekaa kimkakat kupunguza watu kumilik line/account nying za simu kupunguza risk za kiusalama..nahis labda lengo ndo hili