Bajeti 2021/22: Kodi ya uzalendo ni kaa la moto. Kila laini ya simu itakatwa Sh. 100 kila siku

Sometime natetea nchi yangu ila inafika mahala nasema dah...hiv kwel kama nchi tunashindwa kujikwamua ila kwa kukamua wnaanch had damu...hiv hao officials wa serikal na wengneo wanaolipana 11m++++...wao mbona wanachkua hela nying sana jaman..kwa kaz gani...dah.anyway...yaan mnakata watu kwenye line za simu

Au hii imekaa kimkakat kupunguza watu kumilik line/account nying za simu kupunguza risk za kiusalama..nahis labda lengo ndo hili
 
hiv hao officials wa serikal na wengneo wanaolipana 11m++++...wao mbona wanachkua hela nying sana jaman..kwa kaz gani...dah.anyway...yaan mnakata watu kwenye line za simu
Hawa wakubwa, kama wananchi tusipoamka kutoka kwenye usingizi huu wa pono watatutafuna mpk tufe.

Tufike mahala tuandamane tupinge na na tushushe mishahara yao toka 11m hadi laki 5 kwa mwezi. Halafu tuone kama kutakuwa na hizo nyinmbo zao za uzalendo.
 
Na ukiitaka vita itokee bungen mule..ongelea maslah yao kupunguzwa hata kidogo...Daktal specialist analipwa hata mil3 haifik...anapiga kaz usiku na mchana siku 7 za week 24hr.....wao wanakenua tu mule wanavuta minimum 11m...hii ni zaid ya unyonyaj.
 
Unakuta mbunge anajisifia kusema watu wangu. Huku hao watu wakiteseka, fukara. Shule majengo shida, huduma za afya tabu. Mtu mmoja analipwa mamilioni.
Hakuna haki. Wabunge wenyewe majimboni hawaonekani. Wakienda Bungeni maswali ni yale yale toka nazaliwa hakuna linalo badilika. Utasikia korosho, Pamba, ufugaji, madini, elimu. Hivi haya yote hayajapata ufumbuzi toka wakati wa Nyerere hadi Leo! Miaka 60 tunaongelea jambo lile lile!
Ulaya ya miaka ya hamsini na tisini ilikuwa masikini si kama ya Leo. China, Malyasia, India, Korea na nyinginezo walikuwa masikini.
Je sisi watanzania tumelaniwa nini? Nyerere alitupatia viwanda leo vyote hakuna.
Shida ni nini? Nilibahatika kufanya kazi serikalini, nilipo ingia nilishangaa mengi. Hapo nikajua Tanzania kwendelea ni kazi. Tutapiga mark time.
Tunahitaji kubadili mfumo wa kiutumishi. Tunahitaji kubadili matumizi ya fedha na mshahara. Tunahitaji kubadili mfumo wa utekelezaji wa miradi.
Pia kubadili mfumo wa Bunge. Na kuwa na wabunge wachache. Kufuta viti maalum. Na wabunge wawajibishwe mara wanapokuwa si wawajibikaji.
Hivyo tunahitaji muundo mpya wa serikali. Hata baraza la mawaziri hatuhitaji utitiri wa mawaziri.

Kuna mtaalamu wa ujenzi ni Afisa mkubwa walijenga barabara isiyo na kiwango ktk kumhoji akanambia akijenga ya kiwango yeye na familia yake watakula nini?
Anajua hyo isiyo na kiwango baada ya muda itahitaji matengenezo hivyo atapata fedha. Nilichoka!

Afisa mmoja mkubwa anateuliwa na Rais akanambia usipo kula fedha ya serikali wengine wanakula. Usiangalie kuendeleza nchi. Jiendeleze mwenyewe.
Baada ya muda niliona niache kazi ya serikali na kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa.

Tuombeni na kudai Katiba mpya. La sivyo hata vyama shindani vikiingia bado ni yale yale.
 
Mkuu tuanze na mabango kusimama barabarani aiseee...
 
Haya yote maza anayajua vizuri sn
 
Acheni kulalamika ovyo tutafute pesa tulipe kodi nchi ipate maendeleo wenzetu wana kodi mpaka 45% lakini wanalipa sisi Tsh 100 tena inaweza iwe Tsh20 watu mnashinda mnaliaaaaaa bas tumieni tu barua.
Watu kama nyie ndio mlisababisha uhuru kwa mwafrika ukachelewa sababu ya kutokuelewa unatakiwa kusimama na nani na kumpinga.

Swala hapa sio kiasi kidogo cha pesa kutozwa kama kodi, bali swala ni matumizi mabaya ya nafasi ya uongozi kujinufaisha kimfumo.

Hali ya wananchi kiuchumi ni mbaya sana kwasasa, na hawa wanaojiita viongozi na watendaji wamebakia kubuni vyanzo vya mapato ambavyo Kimsingi ukitazama katika mzani wa haki ni vyanzo haramu kutumika na serikali.

Sasa umeona wapi unatia utitiri wa tozo katika mambo muhimu kwa wananchi kama mawasiliano ya simu na mtandao, nishati kama gesi , mafuta ya taa, na mafuta ya petrol na diesel. Vitu ambavyo raia wanavihitaji kuendesha maisha na kuishi kwa furaha.

Shida ni moja, haujui kuwa hawa jamaa wanahitaji hizo pesa ili kuendelea kuishi kifahari na kutapanya. Unaweza nionyesha mbunge au waziri mwenye maisha ya kawaida?!

Ndio maana kwenye hili hutoona hata wabunge wa upinzani kupinga sababu hizi tozo ni mapato yao kuendelea kuishi kifalme na familia zao.

Sasa unless na wewe una benefits zako serikalini ila kama ni umeongea tu basi nakushauri ujifunze vizuri ukweli wa mambo usikalie kusikiliza wanachoongea hawa wajaalaana wanaojiita viongozi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Bado ile 100 kwenye mafuta na ile buku moja ya jengo inayotozwa kwenye luku, sasa unajiuliza tangu lini zile nyumba duni za vijijini zikalipiwa kodi, maana nyingi zitakuwa zimeshaunganishwa na umeme wa REA kwa hiyo nazo zina LUKU.
 
Kuwa na utu ni kazi sana, maana inakuhitaji ujikane nafsi yako kwanza ndipo uweze kuelewa hali ya mwingine. Huyu anaonekana ndio wenzake na akina Sabaya na makonda.

Kujikuta wana uzalendo na taifa ambalo hawajui hata kinachoendelea huko kwa mabwanyenye.....

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
wao wanakenua tu mule wanavuta minimum 11m...hii ni zaid ya unyonyaj.
Wengine wanasinzia tu mle. Wengine wanasaini na kuondoka. Nobody cares ili mradi posho inaingia.

Tukipunguza posho za wabunge kwa 25% hakutakuwa na haha ya tozo kwenye laini za simu.
 
Mkuu tuanze na mabango kusimama barabarani aiseee...
Acha tu mkuu tuendelee kulala usingizi wa pono. Wenzetu Kenya waliwahi kwenda kuzingira jengo la bunge wakati wabunge wao walipotaka kujiongezea posho zao. Sisi tumelala tu mpk wanaleta Kodi ya umiliki wa lqini ya simu.
 
Acheni kulalamika ovyo tutafute pesa tulipe kodi nchi ipate maendeleo wenzetu wana kodi mpaka 45% lakini wanalipa sisi Tsh 100 tena inaweza iwe Tsh20 watu mnashinda mnaliaaaaaa bas tumieni tu barua.

Kateni hela za wabunge, au uzalendo ni kwetu tu?
 
Mbona imeandikwa vizuri kuwa utakatwa kutokana na unavyoweka vocha

Mtoa mada acha upotoshaji
Usitetee ujinga ndugu. Raia kama wewe ndio mnawapa kichwa hawa wanaojiita viongozi kujizungusha pale bungeni na kushindwa kuja na akili za kisasa kubuni mbinu mpya za mapato yasiyomuelemea mwananchi wa kawaida.

Nyie ndio mnawafanya wakae miaka nenda rudi wakitegemea vyanzo vile vile vya mapato na wasijue tunaelekea wapi.

Anyway, watu wanaongezeka kwa kasi ila bado mipango tuliyo nayo ndio hii ya kipuuzi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Nilichosema ni kuwa aache upotoshaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…