Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Bajeti iko poa sana. Vitu vingi vimeshuka kodi au kusamehewa kabisa. Ilikuwa ngumu na gharama kubwa kukusanya kodi za majengo (TRA WANAJUA HILO) Mtu atoke sinza aende KINONDONI KULIPA ELFU KUMI AU 50000 KWA MWAKA? bora waingize huko ambapo hakutakuwa na ukwepaji wa hiyo KODI.
TUWE WAZALENDO, SISI KILA KITU TUNALALAMIKA KAMA WAPUMBAVU HIVI.
Bali wanaopaswa kulipa ni wenye nyumba si wapangaji , tafuteni namna ya kuwaengua wapangaji
 
Yaani naona kabisa bajeti alizo kuja nazo ni mzigo kwa wanachi kuanzia Hili LA kodi ya jengo ukija LA. Laini za simu unaona kabisa huyu ni mzigo kwa watanzania ambao ni walala hoi.

Jiulize mtu amesaidiwa umeme wa LEA na wajukuu huko kijijini Leo unampa mzigo wa kulipi nyumba ambayo hata hadhi ya kuwekewa umeme ilikuwa haina.

Mungu atupe uvumilivu na hili maana naona mpango alifanya vitu ambayo vilikuwa haviendani na watanzania ila huyu kafanya ambavyo havipo kabisa Tanzania.
Serikali imeludisha kodi ya kichwa,
 
Una nyumba!?? Tuanzie hapo kwanza!!
nina nyumba 5 , 2 Kyela , 3 Dsm , kati ya hizo 1 ya Kyela na 1 ya Tandika naishi mwenyewe , sasa hizi 3 kwanini wapangaji wangu wakatwe kodi ya jengo ?
 
Kitendo cha Waziri wa Fedha kupendekeza kodi ya majengo ikatwe kwenye manunuzi ya umeme kinapaswa kufafanuliwa vizuri ili wananchi waelewe vizuri.

Hii ni kwa sababu nyumba nyingi zina wapangaji na ambao ndio walipaji wa bili ya umeme kwa vile wao ndio wanaoutumia, ziko nyumba ambazo wenye nyumba hawamo kabisa, wanaokaa humo ni wapangaji tu, wanawezaje kulipishwa kodi ya jengo kupitia ununuzi wa umeme huku wakiwa si wenye nyumba?

Hata kama hela hiyo itakatwa kidogo kwa mtindo wa kudunduliza, lakini haipaswi kulipwa na wapangaji .

Hili lifafanuliwe au lifutwe tuweke utaratibu mwingine utakaowalipisha kodi ya majengo wahusika tu.
Inapaswa kulipwa na nani?We si ndo unakaa kwenye nyumba?
 
Vipi kuhusu wale wanaoishi nyumba za serikali kama polisi, wanajeshi, Marc, Ras, mawaziri na makatibu wakuu wa wizara watakuwa wanalipia Kodi ya nyumba za serikali kupitia luku? Au Sheria hiyo imewabaguaje? Je, mashule, hospitali na ofisi za umma zinazonunua umeme wa luku nao watachangia Kodi za majengo ya umma wanunuapo luku?
Aliyelielewa hili anifafanulie tafadhali kwani sijabahatika kuisikia hotuba!
 
Back
Top Bottom