Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Kwa kuwa kwa sasa wazee na wastaafu wana exemption ya kodi ya majengo , Je itakuwaje watakapokuwa wananunua luku?
 
Unalikataa peke yake,usitusemee na sisi, kwani Kuna sheria inaingilia makubaliano ya mwenye nyumba na mpangaj kuhusu Kodi ya pango?!
Mbona vitu vidogo sana, Kama Kodi ya chumba kwa mwezi efu hamsini, kwa miezi sita 300,000/= basi atatoa iyo 6000/= na alipe tsh. 294000/=
Mbona simple,
 
Braza we ni kichwa
 
Tunamsubiri msemaji wa serikali afafanue hapa
 
Ivi nyie watu mnatakaje kwani???
Mnalalama madawa hospital hamna, mara maiti zetu zinalipishwa hela kibao, serikali inafanya ubunifu katika ukusanyaji wa Kodi ili mwisho wa siku maiti za wajomba zenu zisizuiliwe uko mahospitalini, na madawa yawe ya kutosha, Bado tu mnaleta ujuaji mwingiiii
 
Kama kuna kitu kimenifurahisha ni hii namna mpya ya kulipia kodi kupitia Luku. Kuna baadhi ya wapangaji wamechikichia fedha za wenye nyumba waliowatumia ili walipe kodi hiyo. Ubunifu huu ni wa kupongezwa sana. Rejea sheria inasema u
Inatakiwa kulipwa na mwenye nyumba au anaeitumia. Wapangaji kuweni wapole anayeona anaonewa ajenge nyumba yake tuone kama hatailipa .
 
Hili ni tatizo, hapa mjini unakuta plot moja ya 20*30 in nyumba tano kila moja ina mita ya umeme, labda tatu kasajili kwa jina lake, moja la jina la mtoto, nyingine jina la mtoto mwingine. Hio Kodi ya jengo inakatwaje kwenye mazingira kama haya?
 
Kuna wakati unajiuliza hivi hawa tunaita wasomi wa uchumi wanajua uchumi wa wananchi wao kweli au wanajua kuwa wote wamejenga na wana uhakika wa kula Milo mitatu kama wao

Mungu awape akili mpya hizi zilizo tumika wazitupe kule
Ni kujitoa ufahamu tu kwani wana ndugu zao wengi tu ni mafukara lakini wamebaki kutetea matumbo yao.
 
Tunamsubiri msemaji wa serikali afafanue hapa
Ukweli huenda hii ni njia rahisi zaidi na ya uhakika ya kukusanya kodi hiyo kuliko nyingine. Ni ukweli kuwa kodi zote zenye biashara, mlaji wa mwisho ndiye hulipa hiyo kodi. Badala ya mwenye nyumba kuongeza shilingi elfu kumi kwa kila mpangaji kwa mwezi kisa kodi hiyo, afadhali ikatwe kwenye luku kwani ni elfu 12 kwa mwaka tu. Naunga hoja mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…