Mbona kodi yenyewe ni ndogo sana...Buku tu kwa mwezi or elfu 12 kwa mwaka hii nayo tutoe mishipa kuijadili humu?
Km nyumba ina wapangaji wa 5 hio ni 200 kwa mpangaji, hii kweli nalo la kujadili kweli...mpangaji analipa kodi ya 50k-150k anashindwaje kuchangia 200 km kodi ya Jengo.
Kuna watu tunakatwa 30% PAYE na kuna watu wanakatwa 8% na kuna watu hawakatwi kabisa, hili ndo tuliongelee ila sio issue ndogo ndogo km hizi unless tumekosa kazi za kufanya.
Na km tuna taka ku protest kuhusu hii kodi then tuanze na ushuru wa magari ulioingizwa kwenye mafuta unaowafanya ht wasio na magari waulipie, mtu unanunua petrol ya jenereta unalipia na ushuru wa magari.
Watanzania tupende kulipa kodi...kuna mchangiaji hapo juu kazungumzia kushuka kwa gharama za kuunganishiwa umeme kutoka 300k mpaka 27k, haya ni mapato yamepungua ila hamlalamiki, ila buku tu kwa mwezi tunatoka mapovu...tunataka maendeleo ila hatutaki kuyachangia, then serikali ikikopa kufidia nakisi napo tunalalamika deni la taifa...kila kitu kwetu ni lawama, hatuna jema.