Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kitendo cha Waziri wa Fedha kupendekeza kodi ya majengo ikatwe kwenye manunuzi ya umeme kinapaswa kufafanuliwa vizuri ili wananchi waelewe vizuri.
Hii ni kwa sababu nyumba nyingi zina wapangaji na ambao ndio walipaji wa bili ya umeme kwa vile wao ndio wanaoutumia, ziko nyumba ambazo wenye nyumba hawamo kabisa, wanaokaa humo ni wapangaji tu, wanawezaje kulipishwa kodi ya jengo kupitia ununuzi wa umeme huku wakiwa si wenye nyumba?
Hata kama hela hiyo itakatwa kidogo kwa mtindo wa kudunduliza, lakini haipaswi kulipwa na wapangaji .
Hili lifafanuliwe au lifutwe tuweke utaratibu mwingine utakaowalipisha kodi ya majengo wahusika tu.