Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Jana kwenye bajeti iliyopendekezwa na Serikali, wamependekeza tozo ya shilingi 1000-3000 kwenye ving'amuzi kulingana na kifurushi mtu ananunua. Serikali tayari inakusanya kodi kwenye haya makampuni na pia inakusanya VAT kila mteja anaponunua king'amuzi au kifurushi, kumuongezea tozo itakuwa kumfanyia 'double taxation'.
Pia si afya Serikali kuamini tozo kutimiza majukumu yake, inamuumiza mwananchi lakini zinadumaza sekta na matumizi ya teknolojia.
KICHEKESHO
Mkurugenzi wa DStv anaishauri Serikali hadharani jinsi ya kuwaumiza wateja, labda wanaona wanapitwa na wanaoachia free chanels lakini ile ni biashara na kila mtu ana namna yake ya kuendesha biashara yake.
Kuzisabotage kampuni nyingine zifanye kama wao kukata free chanels kifurushi kinapoisha haijakaa njema. Kama wao wameshindwa waache wanaoweza.
Kwa Serikali kufanya hivi watajichonganisha na wananchi, lipo kundi kubwa haliwezi kulipa na ving'amuzi vitakuwa mapambo na biashara ya wateja wapya itashuka.