Jamani wabunge, nyie ndio mliobaki kuliokoa taifa kwenye huu wizi wa mchana.
Stimulus package hela za serikali haziendi bure kwani hata hizo hela IMF walizoleta ni mkopo.
Serikali ikilipa madeni ya vyama vya ushirika na hayo makampuni makubwa ya kununua pamba, kahawa ya kina ELna RA lazima serikali ipate stake ya ownership kama ambavyo US govt imepata kwenye GM, AIG na kila sehemu hela za serikali zilipoenda.
Hayo makampuni yakipata faida uko mbeleni yanalipa hela back na stake inarudishwa.
Otherwise huu utakuwa usanii wa kusaidia wafanyabiashara wachache ambao wakipata faida wanakula, wakipata hasara serikali inawapa hela za bure.
Halafu lazima transparency ya hali ya juu iwepo, ili serikali itangaze imetoa hela kiasi gani kwa kila kampuni kwa majina ili wabunge na wananchi tuweze kuhakikisha hayo makampuni yapo na uko mbeleni yanalipa hizo hela sio usanii kama wa EPA hatujui nani karudisha hela wala nini.
Sasa wale wakulima kule Vijijini waliolima kahawa, mahindi, maharage wao watafidiwa vipi na hasara walizopata???