Bajeti ya maji ya Rais Samia ni karibu mara tatu zaidi ya ile ya FY2020|21

Bajeti ya maendeleo ya maji sio budget in total soma vizuri nilichoandika
Andika mchanganuo ukionyesha fedha za maendeleo na matumizi ya kawaida!

Summary ya waziri wa maji:

MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/2022

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, ninaomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako
Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 680,388,976,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2021/22. Kati ya fedha hizo, Matumizi ya Kawaida ni
Shilingi 33,758,976,000 ambapo Shilingi15,273,812,000 sawa na asilimia 45.2 ni kwa ajili ya
kugharamia Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 18,485,164,000 sawa na asilimia 54.8 ni kwa ajili ya
kulipa mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na Chuo cha Maji.

Jumla ya bajeti ya maendeleo ni
Shilingi 646,630,000,000 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 346,630,000,000 sawa na asilimia 53.6 ni fedha za ndani na Shilingi 300,000,000,000 sawa na
asilimia 46.4 ni fedha za nje.
164.Mheshimiwa Spika, ninaomba tena nitoe shukrani zangu kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara www.maji.go.tz. 165.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.
 
Mafuta ya kupikia yamemshinda, siasa zetu za kutiana moyo sana kwakwel..
 
HATA UMEME TULIAMBIWA HIVYO HIVYO TENA ILIPOPATIKANA GESI NDIYO NGONJERA ZIKANOGEZWA ZAIDI. LEO JEEE TUMEFIKA WAPI.
 
expand...
Bajeti ya kuzingatiwa ni bajeti kuu,

Hizi bajeti za wizara huo ni mapendekezo kwa wizara ya fedha,

Soma hii kifungu 102 utaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…