Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Aluta continua ,mpaka kieleweke .

Hii nchi haiwezi kuendelea kama uongozi wenyewe ndio huu uliopo kwa sasa .

Kuna haja ya kuliombea taifa kwani mambo haya ni ya ajabu kabisa sijui ni wapi iliwahi kutokea kitu kama hii hapa duniani.

Kama ni hivyo basi kuna haja ya kusoma kwa kina taarifa zote za serikali na kuna madudu mengi sana .
 
Mpaka kieleweke naomba sana kujua majina ya walio beza upinzani tupate kuyapitia tena upya mkuu jitahidi utuwekee hapa .Kesho wanatoa vitabu vipia wameviandaa lini ?
 
Mpaka kieleweke naomba sana kujua majina ya walio beza upinzani tupate kuyapitia tena upya mkuu jitahidi utuwekee hapa .Kesho wanatoa vitabu vipia wameviandaa lini ?

Kuna taarifa kuwa jana usiku walikaa kikao na watendaji wa wizara ya fedha wote,

Kuna ndege ilikuja hapa leo mchana ,sasa huenda imeleta vitabu ama laa hatujaweza kujua kwani imewasili jioni hii uwanja wa ndege hapa Dodoma .

Tusubiri kuona kesho asubuhi lakini jambo la uhakika ni kuwa kesho wataleta vitabu bingine.
 
halafu wabunge kibao waliunga mkono bajeti na kuisifia sana tuu, alieisifia kupita kiasi leo ni Ritha Mlaki.... kwi kwi kwi kwi kwi kwi.... kweli tumekwisha
 
Kudos to Dr. Slaa!!

.......mmmh but wait a minute......hivi ni lini wewe Dr.Slaa ulijua/ulizitambua hizi kasoro za bajeti?.......mwenye track record ya Dr.Slaa akiwa bungeni naomba atuwekee ili tuione hii consistency yake.......Inawezekana matatizo hayo ya ku-copy and paste yapo tangia wakati wa Hayati Tuntemeke Sanga na Amir Jamal!!......Just curious
 
waziri wa fedha muda mfupi uliopita amekubaliana na hoja ya Dr,slaa na wabunge wa upinzani kuwa ni kweli vitabu alivyowasilisha vya mapato vimekosewa na hivyo watawasilisha vitabu vingine.

Kwa mujibu wa taarifa zake ni kuwa amewapongeza wabunge wa upinzani kwa kuwa watu makini na wanaosoma na hivyo kuweza kuiamsha serikali.

Hii ni aibu ya hali ya juu. Kama nilivyowahi kusema hapa tuna sirikali iliyooza haipo makini kwa chochote kile ndani ya sirikali hiyo. Wabunge wachache wa upinzani wamefanya mengi bungeni yenye maslahi makubwa kwa nchi yetu kuliko wabunge zaidi ya 200 wa chama cha mafisadi ambao kazi yao kubwa ni kutetea mafisadi na chama chao cha mafisadi.
 
waziri wa fedha muda mfupi uliopita amekubaliana na hoja ya Dr,slaa na wabunge wa upinzani kuwa ni kweli vitabu alivyowasilisha vya mapato vimekosewa na hivyo watawasilisha vitabu vingine.

Kwa mujibu wa taarifa zake ni kuwa amewapongeza wabunge wa upinzani kwa kuwa watu makini na wanaosoma na hivyo kuweza kuiamsha serikali.

Huyu waziri anatakiwa kujiuzulu mapema sana, what an idiot, kama hataki kujiuzulu JK amwajibishe. Hatuwezi kupoteza pesa ya walipa kodi kwa uzembe kama huu. Je, ni nani atalipia hizi gharama mpya?
 
Kama mtakumbuka nilisha zi discredit hizi budgets kama mchezo wa redio.

The problem is deeper than apparent, the actual revenues and expenditures are nothing like presented in the budget.
 
Cha kushangaza hakuna uwajibikaji. Kutoa takwimu zisizo sahihi si nilikulidanganya Bunge? Au kosa hili ni kwa kambi ya upinzani pekee?
 
wabunge wa ccm hawawezi kumkosoa waziri wao,wao wanapoona kasoro ni lazima waipeleke kwenye chama,kwa hiyo tusiwaseme sana sio kosalao ila ni nidhamu ya chama
 
...... ujumbe huu una ashiria nini kwa wabunge wa CCM?

Ina maanisha kwamba, hata waziri hakujua anasoma pumba. Alikuwa kama robot. Hata yeye hakuisoma speech na kuona mapungufu yaliyokuwepo. He is a man of copy and paste. TO PROOVE THIS, AMEKIRI mwenyewe kwamba wapinzani wanasoma na kuchambua wanacho soma. Hawako bungeni kwa ajili ya allowances na kwenda kuchoma nyama mnadani. Shame to CCM!!! BRAVO OPPOSITIONS, KEEP IT UP!! Tuko na nyie.
 
sasa kama vitabu vimekosewa na wao walikuwa wanalijua hilo, waliwaachiaje watu wachambue na kuitia nchi gharama kwa kitu kisicho na ukweli?
bunge la tanzania ni aibu. wabunge wa ccm wamejazana lakini pumba tupu.
 
wabunge wa ccm hawawezi kumkosoa waziri wao,wao wanapoona kasoro ni lazima waipeleke kwenye chama, kwa hiyo tusiwaseme sana sio kosalao ila ni nidhamu ya chama

Bajeti imesomwa Bungeni, sasa hizo kasoro zinapelekwa kwenye Chama ili chama kifanye marekebisho au ili iweje? Hapo naona unawatetea tu kwa kuwa mwenzao (Mkullo) amewaumbua kwa kuwaita mazezeta/mbumbumbu mzungu wa reli na wapinzani walioichambua bajeti yake kwa kina akiwaita wabunge makini na wanaosoma neno kwa neno na hata yale ambayo yako impliedly wanaweza kuyaona.

Maneno aliyosema Mkullo ni matusi kwa wabunge wote wa CCM na hasa waliochangia na kuiunga mkono 100 kwa 100.

Mkullo ametoa picha halisi ya wabunge wengi wa CCM, ndiyo maana miswada yote ya sheria huwa inapeta na wala haipingwi matokeo yake tunaishia kuwa na sheria mbovu na zikishindwa kufanya kazi ndipo serikali inapokuja na excuse kwamba sheria zetu ni mbovu pamoja na sera. Pingamizi siku zote utasikia kutoka kambi ya upinzani na kwa kuwa wao walishapewa jina la kwamba wao ni pinga pinga wa kila kitu. Angalau kuna waziri amekiri kwamba huwa hawapingi tu bali wako makini na kweli wanasoma.
 
Sababu zaidi ya kuongeza wabunge wa upinzani bungeni.
 
Tunamsubiri Mkullo kwa hamu akiwa anawasilisha vitabu vingine.

Leo waziri mkuu hajaulizwa maswali ya papo kwa hapo kama kanuni zinavyosema ,siwaelewi.......
 
Aje na vitabu vingine na maelezo ya kutosha,kwa nini alikuja kusimama na kusoma bajeti iliyokua na makosa makubwa kiasi hicho? Ni kwa nini asiwajibishwe kwa hilo?
 
Aje na vitabu vingine na maelezo ya kutosha,kwa nini alikuja kusimama na kusoma bajeti iliyokua na makosa makubwa kiasi hicho? Ni kwa nini asiwajibishwe kwa hilo?

Because he is illiterate!
 
Back
Top Bottom