Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Huyo jamaa anaitwa sijui Mkuu lo!Alikuwa NSSF akawa na vidaladala vyake alikuwa akiviita Ushora Ndago alivipata kwa ufisadi akiwa huko. Akaenda Zimbabwe tunasikia leo kaibuka kawa Waziri wa madafu ya Tanzania. Kimsingi nina doubt kidogo uelewa wake kuhusiana na micro and macro economic challenges tulizo nazo hapa nchini like tourisim sector,Agricultural and Industrial sector, Mining Sector. Halafu pia Education huyu jamaa ni rubber stamp tu atahukumiwa siku ya mwisho.
 
waafrica!kama viongozi wao ndo hivi waongozwa je?he mi simo
 
maajabu wabunge wa CCM wanaunga mkono hoja kwa asilimia mia kumbe hajaui wanaunga mkono nini. mpaka PM amewashangaa na kusifia wapinzani
 
Spika apigwa kigugumizi juu ya wabunge kutokupewa vitabu vya mapato ya serikali ,anasema kuwa ataenda kuzungumza na serikali kwanza kitu ambacho ni kinyume na kanuni za Bunge.

Spika anabanwa na Zitto sasa kuwa kanuni hazionyeshi mapato na huwa wanakaa kama kamati ya matumizi, je? ni wakati gani bunge litapitisha mapato ya serikali kwani wakati wote wanapitisha matumizi bila ya mapato
 
Wabunge wa CCM wameanza kumpongeza waziri eti kwa kukubali makosa ,na sasa lawama zinaelekezwa kwa watendaji kuwa hawakuonyesha umakini katika utendaji wao ,sasa lawama zinaenda kwa watendaji wa serikali na kuwa watendaji hawakitakii mema CCM katika kutekeleza ilani yake.

Huyu ni mama Magreth Batenga, anaendelea
 
Ze comedy wakiwa mjengoni.

Hivi kama wakuu wanafanya makosa ya wazi namna hii what happening down there.

watu wanalipwa mishahara ya bure kabisa ndo maana hata leo ukimuliza mkulo bila vitabu kuwa ameongeza kodi kwenye soda kiasi gani hawezi kukueleza kwa kuwa anachojua ni kucopy na kupast.
 
Hivi wakuu haiwezekani tukapeleka waraka (kama ule wa sinclair) wenye maudhui ya 1. Kumtaka Mkulo ajiuzulu haraka iwezekanavyo
2. iwapo atakataa kufanya hivyo, Kikwete amwajibishe kwa kumwondoa haraka.
Hii ni kwa sababu alichokifanya Mkulo ni zaidi ya kuliabisha taifa, na sidhani kuwa inaweza kutokea sehemu nyingine yoyote duniani na ikavumiliwa kama tunavyoivumilia sisi
 
Mama Kilango awasha moto kuwa kama pesa za EPA hazitarejeshwa basi ni bora afe kuliko kuendelea kukaa kimya .

Awataka wananchi kukaa kimya kwani wabunge watazishughulikia hadi zirudi.

Asema kuna kuna bilioni 216 ambazo zinashikiliwa na mafisadi tangu 1992, ziko mikononi mwa watu wachache ,lazima zirudishwe hizo fedha .

April serikali iliwapa hawa watu muda wa miezi mitatu ila hadi leo hazijarejeshwa ,na kama wabunge wakikaa kimya na kutokutetea wananchi wake ni kuwa mbunge huyo hawapendi wananchi wake na kama hazitarudi basi bunge patakuwa hapatoshi.
 
Mama Kilango ametaja neno vitisho mara 7 wakati akiwasilisha mchango wake.

Spika naye kasema haogopi vitisho hivyo wabunge wasonge mbele.
 
Nakumbuka signature moja hapa JF; Bubu watasema na MOTO UTAWAKA!
 
Aibu hii ni ya rais wetu mheshimiwa.
wanamuaibisha sana, ina maana team yote iliyomuweka kikwete ni ovyo?
kuanzia wanasheria wake, wafadhili wake, wataalamu wake???
amtegemee nani??
kwakweli urais ni kiti cha upweke sana.
ni bora angeshuka kwa wananchi tungembeba kwani bado charisma anayo.
Ataanzaje lakini, labda kuna masharti fulani ya sangoma??
namuonea huruma sana.
Nadhani saa hizi yuko kwenye tafakari ya kuachia kiti awamu ya pili.

''kukubali udhaifu si udhaifu'' kutoka kwa bonge wa barabarani clouds fm.
 
Wabunge wameamua kuamka sasa na kama wangelikuwa ni kwa masilahi ya wananchi basi bunge lisingepitisha hiyo bajeti
 
Mimi haya yote yakiendelea siwashangai hao akina Mkulu kwa sababu kwa kweli ndivyo walivyo, serikali ya CCM chini ya Kikwete na umakini ni vitu viwili tofauti kabisa. Kwa wale wanaomjua Mkulo, ni miujiza wa ajabu kutegemea Mkulo afanye tofauti na anavyofanya.

Kwangu mie kinachonifurahisha na kunishangaza ni baadhi ya watanzania hapa ndani ya hii nyumba ya JF. Pamoja na umakini wote huu unaonyeshwa na wabunge mahiri wa upinzani, bado kuna watu hapa ndani ya JF (fulani na fulani na fulani) wanaoendelea kuwalisha sumu watanzania kwamba wapinzani bado hawajawa tayari kutawala. Kwa kweli Mungu atusaidie tuondokane na hii ndoa ya kikuria ambayo watanzania wanalazishwa kubaki nayo na ccm.

Kwa kosa kama hili ingekuwa nchi za wenzetu serikali inakosa sifa za kuwa serikali na kura za maoni zingeteremka na watu wangesubiri uchaguzi tu kumuua mnyama CCM kama wanaria vile. Lakini pundits wa JF watatuambia na kutuelimisha kuwa upinzani bado, CCM imekomaa, ina uzoefu, imeenea nchi nzima. Mwenyekiti wangu angesema ndio wana uzoefu, lakini uzoefu wa kuharibu, lakini ma-pundits wa JF watamuelewa? Wapi bwana!!
 
mama anna amaetumia neno vitisho mara 7 na sita pia katumia neno vitisho....nnacho shangaa ni kuwa hawasemi hivyo vitisho vinatoka kwa nani na wamepewa vitisho hivyo kwa njia gani.
nao wanataka kujifanya wako upande wa wananchi lakini i doubt.
 
Bajeti yazidi kupata wakosoaji yadaiwa ina mapungufu mengi

Waandishi Wetu, Dar
Mwananchi

WAKATI mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2008/09 ukitarajiwa kufikia tamati kesho, wanaharakati na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), wameikosoa bajeti hiyo wakisema kwamba imejaa ahadi nyingi ambazo ni ngumu kutekelezeka.

Licha ya kuikosoa bajeti hiyo kwa kuwa na ahadi nyingi pia wamesema bajeti hiyo haikumwangalia mwananchi wa kawaida hivyo kuwa sawa na kiini macho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nestory Ngulla, alisema bajeti hiyo imejaa maelezo mengi ya kisiasa badala ya kuelezea na kuonyesha takwimu zinazowezesha kufanyika tathmini yakinifu kuhusu kipato cha wananchi.

"Takwimu zinazotolewa na serikali kuhusu kukua kwa uchumi wa taifa (pato la taifa), bado hazitoshelezi katika kufanya tathmini yakinifu juu ya kukua, ama kushuka kwa kipato cha wananchi. Serikali bado haitoi takwimu zozote kuhusu mgawanyo wa pato la taifa ili kuwezesha wadau kutafakari kama kukua kwa uchumi huu kunawanufaisha wananchi wote," alisema Ngulla.

Alisema bajeti hiyo ni ngumu, kwa kuwa wembe wa kukata kodi bado upo palepale na kwamba, hakuna unafuu wowote kwa wananchi kwa sababu hata kima cha chini kinachosamehewa kodi ni cha mwaka 2007/08 cha Sh100,000.

"Hii ni danganya toto. Hakuna unafuu wowote. Kilio cha wafanyakazi kuhusu kodi inayotozwa kwenye mishahara yao, bado hakijazingatiwa hata kwenye bajeti ya 2008/09. Vyama vya wafanyakazi vimeitaka serikali kutotoza kodi kiwango cha chini ya mshahara unaokidhi mahitaji muhimu ya maisha, lakini hadi leo bado serikali imeng'ang'ania kukusanya kodi kutoka kwenye mishahara ya wafanyakazi ambao wameelemewa na kupanda kwa gharama za maisha, kwa vile tu ni rahisi kuikusanya," alisema Ngulla.

Alisema kiwango cha chini ya Sh100,000 ambacho ni kima cha chini cha serikali kilichotangazwa, kimesema kisikatwe kodi ni cha bajeti ya mwaka uliopita na wakati kuanzia mwaka huu wa fedha wafanyakazi wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kama Tume ya Rais ya Kuboresha Mishahara ya Wafanyakazi wa Umma ilivyoshauri.

Ngulla aliwataka wabunge kuishinikiza serikali kuhakikisha kima cha chini cha mishahara ya watumishi ambacho hakipaswi kukatwa kodi kiwe Sh150,000 badala ya 100,000 ya sasa.

Alisema pia kumekuwapo na upotoshaji wa muda kwa umma unaofanywa na serikali kuhusu takwimu za mishahara wanayolipwa watumishi wa umma.

Alisema katika bajeti za serikali, mishahara kwa watumishi huelezwa kama asilimia saba ya pato la taifa au asilimia 45 ya pato la ndani ya serikali.

Alifahamisha kuwa fungu hilo la mishahara kwa wafanyakazi wa umma, limejaziwa utitiri wa posho ambazo mfanyakazi wa kawaida hanufaiki nazo kwa kuwa zinazoingizwa katika fungu la mishahara na kwamba wanaonufaika ni viongozi na maofisa wa ngazi za juu katika utumishi wa umma.

Akizungumzia kuhusu uchangiaji wa mapato ya ndani ya serikali kwa njia ya kodi, Ngulla alisema katika eneo hilo, pia zinahitajika takwimu zenye mchanganuo unaoonyesha mapato ya makundi mbalimbali ya jamii yanavyochangia katika mapato ya ndani ya serikali kwa njia ya kodi.

Ngulla alisema suala la serikali kila mwaka kutenga fedha zaidi kwa ajili ya kuboresha miundombinu nchini, ni ufisadi wa hali ya juu kwa sababu sekta hiyo, imeshindwa kuonyesha kwa vitendo utekelezaji wa miundombinu na kwamba hauendani na hali halisi.

Alisema serikali imeshindwa kuonyesha dhamira yake ya dhati katika kupunguza na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuondoa matumizi yasiyo ya lazima na badala yake imeendelea kuongeza matumizi mabaya kwa kufanya ununuzi na utumiaji wa magari ya anasa (mashangingi).

Alihoji kwamba kwa nini viongozi wa kitaifa wanaendelea kutibiwa nje ya nchi kwa kutumia gharama kubwa, badala ya kutumia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kuokoa fedha za umma zinazotumika kutibia viongozi hao pamoja na maafisa wa serikali nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kupunguza fedha zinazotumika kulipa posho na semina kwa viongozi hao.

Baadhi ya wanaharakati waliozungumza katika Ukumbi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), walisema bajeti ya mwaka 2008/2009, siyo ya wananchi kama inavyodaiwa, bali ni ya viongozi waendelee kuishi maisha bora.

Walisema bajeti hiyo imekuwa ni mzigo kwa wananchi wanaoishi kwa kipato cha chini, kwani haijawasaidia zaidi ya kuwapa wakati mgumu wa maisha kwa mara nyingine.

Tulidhani hii bajeti ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, lakini naona inaendelea kutupa maisha magumu, wakati tulishaahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania. Sasa naona ni maisha bora kwa viongozi,� alisema Zainabu Msangi kutoka Chama cha Wanaharakati cha Hekima.

Kwa upande wake, Gemma Akilimali kutoka Shirikisho la Wanaharakati (FemAct) aliieleza bajeti hiyo kuwa, ni kwa ajili ya viongozi wala sio wananchi kutokana na kutoshirikishwa kwa wananchi katika upangaji wa bajeti hiyo.

Waliopanga bajeti hiyo ni viongozi wenyewe bila ya kuwashirikisha wananchi, hivyo wananchi wataendelea kuteseka huku viongozi wakiwa wanaendelea kuponda raha Masaki,�alisema.

Katika hatua nyingine, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema ina lengo la kupitia sheria ya biashara kwa lengo la kuweka viwango vipya vya kodi ya Sh400 kwa lita ya bia na vinywaji vikali Sh500 kwa kila sigara elfu moja zinazoingizwa Visiwani Zanzibar.

Hayo yameelezwa katika hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2008/09 katika Baraza la Wawakilishi jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayeshughulikia (Fedha na Uchumi), Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akisoma bajeti hiyo.

Dk Mwinyihaji alisema serikali imekusudia kuchukua hatua za kupunguza matumizi ya vinywaji vikali na sigara kutokana na vinywaji hivyo kukithiri matumizi yake.

Kutokana na athari za kiafya kwa matumizi ya bidhaa hizi, serikali imekusudia kuchukua hatua za kupunguza matumizi yake na sheria ya biashara, itapitiwa kwa lengo la kupunguza matumizi yake pia,� alifafanua Dk Mwinyihaji.

Waziri huyo alisema bajeti ya mwaka huu imepewa jina la Bajeti ya Maendeleo kutokana na fedha nyingi kutegwa kwa lengo la kuwaletea wananchi wa Unguja na Pemba maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.

Ni bajeti ya maendeleo kwa sababu, sehemu kubwa ya bajeti imeelekezwa kwenye matumizi ya maendeleo kuliko matumizi ya kawaida kama ilivyokuwa katika bajeti zilizopita, alisema waziri huyo.

Alisema kwamba katika mwaka ujao wa fedha, matumizi ya maendeleo yamekuwa makubwa ikilinganishwa na matumizi ya kazi za kawaida kwa Sh42.8 bilioni ikiwa sawa na asilimia 28.7

Alisema ukuaji wa uchumi wa Zanzibar ulifikia asilimia 6.5 na kupelekea pato la taifa kufikia Sh588.5 bilioni mwaka 2007 kutoka ukusanyaji wa asilimia 6.1 mwaka wa 2006 ikiwa ni sawa na kuwa, wastani wa pato la mtu binafsi umeongezeka kwa asilimia 13 kutoka Sh 459,000 na kufikia Sh518,000 kwa mwaka.

Dk Mwinyihaji alisema angezeko la asilimia 34.5 katika thamani ya shughuli za ujenzi kutoka Sh 38.3 bilioni mwaka 2006 hadi Sh 51.5 bilioni mwaka 2007.

Ni matarajio yetu kwamba kwa mwelekeo huu, kasi ya ukuaji wa uchumi itakuwa kubwa zaidi kwa mwaka ujao na hivyo hali za maisha za wananchi zitakuwa bora ,� alisema Dk Mwinyihaji.

Alisema vichocheo vingine vinavyochangia mapato ni kuongezeka kwa idadi ya watalii walioingia nchini kutoka 137,111 mwaka juzi hadi jumla ya watalii 143,265 mwaka 2007 sawa na ongezeko la asilimia 4.5.

Dk Mwinyihaji aliwaeleza wajumbe kwamba, sekta ya huduma ya jamii bado inaendelea kuongoza katika mchango wa pato la taifa, ambapo mchango wake uliongezeka kidogo kutoka asilimia 43.5 kwa mwaka 2006 hadi asilimia 43.9 kwa mwaka 2007.

Pia aliitaja sekta ya viwanda kuwa nayo iliongezeka kutoka asilimia 14.8 kwa mwaka 2006 na kufikia asilimia 15.4 kwa mwaka 2007 ongezeko ambalo limetokana na mchango wa sekta ya ujenzi ulioongezeka kidogo kutoka asilimia 7.5 mwaka 2006 hadi asilimia 8.8 mwaka 2007.

Kwa upande wa mchango wa sekta ya kilimo, Dk Mwinyihaji alisema umepungua kutoka asilimia 30 kwa mwaka 2006 kufikia asilimia 27 mwaka 2007 kutokana na ukuaji wake kwa mwaka 2006 kutokuwa wa kawaida kufuatia ukuaji mkubwa wa asilimia 19 kutoka mwaka 2005.

Katika hatua nyingine, Midraji Ibrahim anaripoti kutoka Dodoma kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo amekiri kutofautiana kwa takwimu kwenye vitabu vinne vya bajeti, huku akibainisha sababu mbalimbali.

Akitoa tamko la serikali bungeni jana usiku, Mkulo alisema, hatua hiyo ilisababishwa na vitabu hivyo kuchapishwa mwishoni mwa Mei, huku bajeti aliyowasilisha ikiidhinishwa na serikali saa mbili kabla ya kusomwa.

Pia, Mkulo alisema, kikao cha mawaziri wa fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilikuwa kifanyike mapema, lakini Kenya waliomba kusogezwa kwa tarehe kutokana na matatizo yaliyotokea na kilifanyika Juni 2, mwaka huu.

Alisema kutokana na vitabu hivyo kuchapishwa mapema, baadhi ya mambo mbalimbali ikiwemo utekelezaji umebadilika na hivyo kusababisha takwimu zilizomo kutofautiana na zile za bajeti aliyowasilisha.

Aliongeza kuwa, bajeti aliyowasilisha bungeni ilitoa hali halisi na kwamba, tayari marekebisho yamefanywa ili kugawiwa wabunge ambayo yataoana na kitabu cha bajeti.

Waziri Mkulo alisema, pia hisa za NMB nazo zimesababisha kutofautiana kwa bajeti hiyo kwa sababu, zilithaminiwa kwa bei ndogo, lakini thamani imeongezeka na kufikia Sh60 bilioni.

Sababu nyingine ni wafadhili kutothibitisha mapema kuunga mkono bajeti na kwamba, walichelewa na kuthibitisha mwishoni mwa Mei tofauti na miaka mingine wanavyofanya.

Aliwasifu wapinzani kwa kubaini kasoro hizo na kwamba, serikali ni sikivu huku akiwataka kuendelea kwa sababu, inaonyesha wanasoma sana.

Mbunge wa Karaatu (Chadema), Dk Willibroad Slaa juzi akichangia bajeti hiyo alisema, hataunga mkono hadi vitabu hivyo vitakaporekebishwa kwa sababu vinatofautiana kwa Sh130 bilioni.

Imeandaliwa na Tausi Mbowe, Hussein Issa, Fatma Aziz Dar na Salma Said kutoka Zanzibar.
 
Ni aibu kusikia kuwa nchi yetu ni ya tatu kwa madini ya dhahabu na tuna vito vya kutisha. Tuna mlima mkubwa kuliko yote Africa, tuna Mbuga kubwa kuliko zote duniani na Hifadhi ya Selous ambayo nayo ni kubwa sana. Tuna Ngorongoro crater ambayo ni unique na tuna ardhi kubwa na yenye rutuba! My God, what do we need to transform this economy? Nadhani wachumi wetu na wanasiasa wanatulet down. Tanzania ina vyanzo vya umeme kuliko nchi yoyote ile hapa Africa na imezungukwa na maziwa makubwa matatu, mojawapo likiwa la pili kwa ukubwa duniani. Why are we poor! Is it a curse? Dola bilioni sita kwa nchi kama hii ni utani. Nina imani dhahabu inayochimbwa bulyakhulu pekee kwa mwaka mmoja inafikia fedha hizo! CCM inatupeleka shimoni na watoto na wajukuu zetu watatuhukumu!

Mimi nadhani sababu za kuendelea kuwa masikini zinatokana na mipango hafifu na isiyo ya kweli ya kuleta maendeleo ya haraka. Upendeleo ulioutaja hapo juu ndugu yangu Jobo ni sehemu tu ya rasilimali nyingi tuliyonayo, ikiwemo watu, Bahari inayotuunganisha na nchi nyingi za Asia (Nzuri sana kwa Biashara) na kadhalika.

Inabidi nchi hii ijengwe kwa nguvu zote za wananchi wake. Sasa hivi tunategemea sana Misaada ya nchi wahisani na uwekezaji kutoka nje kabla hatujatumia kikamilifu nguvu za ndani na uwekezaji wa ndani. Ni vigumu na sidhani kama inawezekana kwa mwekezaji kuja Tanzania kuwekeza kwa munufaa ya Tanzania. Atafanya kila jitihada kupata manufaa yote kutoka kwenye nchi hii yenye rutuba ya rasilimali. Tutakapo amka ndipo tutakapoona maendeleo yakianza kuchukua kasi. Kuna mahitaji makubwa ya mabadiliko ya kimtizamo kuhusu uchumi wa nchi yetu na maendeleo yake.

Bajeti ya 2008-2009 sio mbaya sana. Inaanza kuonyesha mwelekeo wa kukidhi na kupunguza matatizo ya wananchi wa kipato cha chini na cha kati. Tukiendelea hivi tutaanza kufanikiwa kidogo kidogo. Inabidi kuanza kuweke msukumo wa ziada kwa waTanzania kuwekeza na kunufaika na uwekezaji kwenye nchi yao kabla mtu kutoka nje kuanza kunufaika na uwekezaji katika nchi yetu.

Naomba kutoa hoja.
 
Nimekuwa nikifananisha Bajeti ya Bwana Mkullo na udanganyifu unaofanywa na katika Bar mara unapoletewa bili ulipie kiasi ulichokunywa aidha wewe na rafiki zako au peke yako. Jambo la muhimu ni kuwa makini na siyo huduma bora ulizopata. Hivi karibuni Mh. Mustapha Mkullo tuliyemwamini sana katudanganya sisi wananchi katika bajeti ambayo kwanza imetuumiza sisi wananchi kwa yeye kuto shusha angalau kodi katika mafuta ili angalau kutupatia ahueni katika maisha haya ambayo kwetu sisi ni adhabu ya kudumu. Ni miaka miwili tu wabunge wameonja joto ya jiwe katika ada za magari yao kwa kulipa 330,000/= na leo hii wamepunguza hadi kufika 140,000/=. Hata hivyo tuwashukuru Kambi yetu tukufu ya UPINZANI kwa kuliona hilo. Na ni imani yetu wanatupigania sisi wananchi.

NDUGU YETU MKULLO

Hapa chini ni mfano wa kile ambacho Mkullo alikifanya BUNGENI BAJE TOFAUTI NA HALI HALISI KATIKA VITABU VINGINE VYA MAPATO. Angalia jinsi ambavyo hata mteja unavyoweza kudanganywa katika BILL ya pombe ukaamua kulipa bila hata kufanya mahesabu kwa usahihi. Mkullo alilipuka akasoma.


View attachment MKULLO.bmp
 
Last edited:
Hiyo bill ni ya kweli! Sasa kama mtu mmoja anatumia fedha hizo kwa siku, iweje mwananchi wa kawaida aishi kwa laki moja tu kwa mwezi?
 
Mwenye budget ya Tanzania aiweke hapa jamani, na ss wengine ambao hatujaipata tuweze kuiona.
 
Back
Top Bottom