Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Kusingekuwa na amani sidhani kama ungepata fursa ya kuandika thread hii ukiwa hapa Tanzania. Usalama wa Taifa nawatakia mafanikio hata kama kuna mapungufu fulani fulani hapo mbeleni mtayarekebisha. Ninachojua ni kwamba Usalama wa taifa wako makini san na kazi yao tatizo ni kwa wakubwa wetu kutozingatia maelekezo toka usalama wa Taifa. Pili idadi yao hawa jamaa ni ndogo sana ukilinganisha na wakati ule wa JK junior walikuwa wengi sana na ilikuwa ni rahisi sana kupata information before the right time to occur. Mie nawasifu sana hawa jamaa. Tendeni haki ili kupata support kwani bado mtahitaji support ya wananchi hata iweje.
 
bajeti ya nchi maskini kama ya kwetu haihitaji kuwa na mvuto!!! ikiwa na mvuto ujue ni ya kisiasa...

Bajeti ya kutuondoa kwenye janga la umaskini lazima iwe chungu... provided wakubwa hawajiwekei fedha nyingi
 
idara ya usalama wa taifa mbali na mapungufu yake uwepo wake nakazi wanzozifanya wanastahiki pongezi.

kuna mengi ambayo wameshindwa kuyafikia kutokana na uchache wa fedha na mengine ni uzembe hayo yanajadilika na yanapaswa kuongelewa kwa nia ya kuboresha sio kila kitu ni kupinga, yaani mtu akisema mungu yupo kwa vile ni mpinzani wako wewe ubadili useme hayupo.


karibuni tumeona jinsi wajanja walivyoila nchi yetu mpaka wakuu wakauliza usalama uko wapi ? mnafikiria kupambana na wanaoitafuna nchi yetu ni jambo rahisi? kuna hitaji kujiandaa na pesa kutumika kwa mafunzo na dhana na mengineyo.

changa moto kwa usalama wa taifa kujitahidi kuajiri waajiri wenye uwezo wa kulitumikia taifa ktk kulinda raia wake rasilimali zake na mipaka ya nchi yetu.

kuweka mbele maslahi ya taifa na kuacha maslahi binafsi kutokuwa tayari kufanya kazi za kuwalinda wachache kwa kuumiza taifa.

hayo machache ningeomba tujitahidi kujadili mapungufu ya idara hii na mapendekezo yatoweza kusaidia taifa letu
 
Tena wangeongezewa na MAJUKUMU mengine ambayo yanaelekea kuwaelemea Polisi wetu kama vile MADAWA YA KULEVYA. Warekebisha tu AJIRA zao ziwe za KITANZANIA zaidi kuliko kuwarithisha watoto na ndugu zao tu.
 
Nadhani Wameongezewa bajeti zaidi ili wa endeleze ile kazi yao ya kuwaua watu makusudi, kama washitakiwa hawa wanavyo elezwa!

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14 mwaka juzi, katika msitu wa Pande Luisi, Mbezi, Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinus Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Ahmed Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.

Nahiyo ndiyo kazi ya usalama wa taifa, bajeti lazima iongezwe
 
Nadhani Wameongezewa bajeti zaidi ili wa endeleze ile kazi yao ya kuwaua watu makusudi, kama washitakiwa hawa wanavyo elezwa!

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14 mwaka juzi, katika msitu wa Pande Luisi, Mbezi, Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinus Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Ahmed Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.

Nahiyo ndiyo kazi ya usalama wa taifa, bajeti lazima iongezwe

Mmh! Wewe kweli ni Savimbi mfufuka. Hawa ni POLISI sio USALAMA WA TAIFA. Au uko Angola?
 
Sidhani kama hawa TAKUKURU walikuwa hawafanyi kazi zao kwa kuwa na bajeti finyu, bali mafisadi ndiyo wanaongoza taasisi hiyo na wanajaribu kila njia kuukwepa ufisadi unaoiangamiza nchi maana kuna uwezekano unaweza kabisa ukamgusa boss aliyewateua na wao wenyewe ndani ya TAKUKURU.
 
huyu hapa waziri wetu wa fwedha
hakikp.jpg
 
Tangu wiki iliyopita nimekuwa natafakari Bajeti ya Nkhulo US$6billion. Hii bajeti inaweza kutukwamua kweli? nikajaribu kuangalia bajeti ya majirani zetu Kenya ambao nchi yao ni ndogo nikakuta ni mara mbili ya ya kwetu! Hivi kweli bajeti hii inaweza kutusukuma mbele au ndo tunasindikiza siku tu? Balozi wa Uingereza amesikika akiikosoa bajeti hii na kutoa matusi, je tumlaumu kwa hilo? Wataalam wana JF na Wachumi nisaidieni kwa hili. Naona kama tunapiga mark time kwa kwenda nyuma! What is your view?
 
Kwa mtizamo mmoja naweza kusema bajeti imejitahidi kutoa kipaumbele kwenye sekta nyeti ambapo kimtizamo hapo panaleta matumaini na ndiyo maana baadhi y wabunge hasa wa chama dola wameishabikia sana.

Hata hivyo naungana mkono na wale wote wanaoiona bajeti hii kuwa haina jipya.Mbunge wa masasi kutoka chama dola juzi alisimama bungeni na kueleza kuwa uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya kurudi nyuma.Hii ni zaidi ya kupuga mark time.

Achilia mbali ufinyu wa bajeti hii ukilinganisha na nchi kama kenya, bado kwa kweli hatujaelewa nini maana ya kuwa na vipaumbele katika harakati za kukuza uchumi.Kusema kuwa sekta ya elimu imetengewa trilioni kadhaa siyo hoja.Suala siyo elimu inapewa kiasi gani bali tunafanyia nini hizo trilioni kukuza elimu nchini.

Tunatakiwa tufike mahali tuwe na vipaumbele maalumu mfano katika elimu.Imewahi kuelezwa kwa mfano kuwa elimu ya ufundi stadi ni kichocheo kikubwa cha kukua kwa uchumi kwenye nchi za dunia ya tatu.Huu ni ukweli.Kwa kutambua hilo inatakiwa tuweke malengo ya kuboresha maeneo kama hayo kusudi tupate ushahidi wa maana kusema kuwa bajeti ijayo tunaweka vipaumbele vingine.

Bajeti hii imekaa kimtegomtego, haioneshi kwa uwazi tutafanya nini kwenye hivyo vipaumbele na kwa nini hasa tumevifanya elimu kuwa kipaumbele.Hoja kubwa ni kuwa kuna ongezeko kubwa sana la wanafunzi na mahitaji ya elimu pia.Tunapima kukuwa kwa elim ukwa kuangalia idadi ya wanafunzi tunaowarundika kwenye shule nyingi zisizokuwa na mahitaji muhimu.Hili halitoshi, hebu tutizame na mwelekeo wa uchumi unavyokwenda na mahitaji ya uchumi kwa wakati na mazingira tuliyonayo.

Vinginevyo hatutapiga tu mak time tutaendelea myuma kwa kasi ya kutisha
 
Bajeti yetu siku zote ni mazingaombwe. Ndiyo sababu kuna mtu alisema ni ya kucopy na kupeste. Hakuna hakili inayotumika. Bajeti za nchi ndogo tu kama Namibia na Botswana ni kama nusu ya bajeti yetu wakati wao wako kama 2 million people tu. Kwa Serikali hii mekenge tusha ukwaa!!!!!!!!!!!!!
 

Attachments

Halafu check hiyo, Budget ya Namibia ni N$ 17.8 billion 2007/08 (US$ 2.5 billion); Cape Town City Rand 21 billion (US$ 3.0 billion), soma bajeti hapo chini. Sasa ukilinganisha population ya Nimibia (2 million) then ya CT (3 million) halafu ya bongo 38 million, utaona kweli bajeti ya US$ 6 billion is nothing na haitatufikisha popote. Halafu cha aibu zaidi kwenye hiyo budget 34 % ni za wafadhiri.....Uwiiiii yesu na maria..............!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Attachments

Botswana:

Budget : US $ 4.0 bn
Mining Revenue : US $ 1.63 bn per yr (40% of GDP).
Population: 2 million

Tanzania:
Budget : US $ 6bn
Mining Revenue: ????
Population : 40 mn

You make a call....
 
Ni aibu kusikia kuwa nchi yetu ni ya tatu kwa madini ya dhahabu na tuna vito vya kutisha. Tuna mlima mkubwa kuliko yote Africa, tuna Mbuga kubwa kuliko zote duniani na Hifadhi ya Selous ambayo nayo ni kubwa sana. Tuna Ngorongoro crater ambayo ni unique na tuna ardhi kubwa na yenye rutuba! My God, what do we need to transform this economy? Nadhani wachumi wetu na wanasiasa wanatulet down. Tanzania ina vyanzo vya umeme kuliko nchi yoyote ile hapa Africa na imezungukwa na maziwa makubwa matatu, mojawapo likiwa la pili kwa ukubwa duniani. Why are we poor! Is it a curse? Dola bilioni sita kwa nchi kama hii ni utani. Nina imani dhahabu inayochimbwa bulyakhulu pekee kwa mwaka mmoja inafikia fedha hizo! CCM inatupeleka shimoni na watoto na wajukuu zetu watatuhukumu!
 
Akichangia mjadala wa Bunge juzi jioni, Zitto alibainisha kwamba katika kitabu cha mapato ambacho hugawiwa wabunge, serikali inasema inatarajia kupata sh bilioni 42 kutokana na mauzo ya hisa za NMB, huku kitabu cha bajeti alichokisoma Mkulo kikionyesha kuwa serikali ilikuwa ikitarajia kukusanya sh bilioni 58.
“Wakati kwenye bajeti Waziri wa Fedha anasema kwamba tutakusanya sh bilioni 58 kwa mauzo ya hisa za NMB, kwenye revenue book zinaonekana sh bilioni 42. Ni takwimu zipi tuzichukue?” alihoji Zitto.
Hata hivyo kumbukumbu za Tanzania Daima zinaonyesha kuwa, wakati akisoma bajeti yake, Mkulo alisema serikali ilikuwa ikikusudia kukusanya shilingi bilioni 60 kutokana na mauzo ya NMB.
Mbali ya Zitto kasoro nyingine ya kitakwimu katika bajeti hiyo ilibainishwa pia na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP), wakati akichangia bajeti hiyo hiyo jana.
Cheyo katika mchango wake alisema amebaini kuwapo kwa tofauti kubwa ya kimapato inayofikia sh bilioni 120, katika kitabu cha mapato, ambacho wabunge hukitumia kuidhinisha matumizi ya serikali.
Kwa mujibu wa Cheyo, takwimu zilizotolewa na Waziri wa Fedha na Uchumi, katika hotuba yake ya bajeti ni kubwa kuliko zilizoandikwa katika kitabu cha mapato .
Alisema katika hotuba yake Mkulo alieleza kuwa, katika mwaka 2008/2009, matumizi ya serikali ambayo yanatokana na mapato ya ndani yatakuwa ni sh trilioni 4.729, wakati takwimu hizo ni tofauti na zilizomo katika kitabu cha mapato ni pungufu kwa shilingi bilioni 60. .
Aidha, alisema kwa upande wa fedha zinazotolewa na wahisani ambazo katika hotuba ya waziri zimetajwa kuwa ni sh trilioni 2.249, zimetofautiana na takwimu zilizomo katika kitabu cha mapato.
Alisema katika kitabu cha mapato, fedha zinazotajwa zinaonyesha tofauti ya sh bilioni 60 kama ilivyo kwa fedha ambazo ni mapato ya ndani.
Ukokotoaji huo wa Cheyo ulibainishwa pia na Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa (Chadema), ambaye katika mchanganuo wake alisema Waziri wa Fedha na Uchumi atapaswa kutoa maelezo ya kina kuhusu makosa hayo, vinginevyo hataunga mkono bajeti hiyo.
 
Sekunde chache zilizopita:Mkullo awapongeza Slaa, Zitto na Cheyo; aseme wenzetu wanasoma kila kitu. Asema kilichosahihi ni hotuba yake kwa kuwa ilipitishwa na serikali masaa mawili kabla. Vikao vilichapishwa mwezi Mei. Kati ya Mei mpaka hotuba inasomwa maamuzi mengi yamefanyika ikiwemo kikao cha mawaziri wa Fedha wa Uganda, Kenya na Tanzania kukabaliana maeneo. Kikao kilifanyika Juni 2 kwa kuwa Kenya waliomba kutokana na matatizo walichukua muda mrefu kukamilisha bajeti yao. Lakini lingine baada ya vitabu kuchapishwa kumekuwa na maamuzi mengine serikalini ambayo yameongeza au kupunguza mapato na hivyo takwimu za Mei zinatofautina na Juni. La tatu mwaka huu kwa sababu zinazoeleweka wahisani walichelewa kuthibitisha kiwango cha michango yao. Wamethibitisha mwishoni mwa mwezi wa tano. Hotuba yangu imechukua yaliyoizinishwa mwezi wa tano. Thamani ya NMB imeongezeka kuliko zile ambazo zimewekwa mwanzoni mwa mwaka. Kutoka 42 imekuwa 58, mpaka sasa wataalamu mwishoni wametuambia bilioni 60. Kwa hiyo figure hasa ni bilioni 60. Kuna mapendekezo mengine yaliyotolewa na vitabu vya serikali ambayo itabidi yaingizwe baadaye, ndio maana nimeweka kwenye hotuba yangu. Mwisho hatutegemei mapendekezo ya wabunge wote kama yataingizwa, baadhi yatabadilisha sura nzima; yale yatakayokubaliwa, tutasababisha yarekebeshwe. Amewasifu kwa umakini wabunge wa upinzani na kusema kwamba serikali iko tayari kufanya marekebisho. Sisi wenyewe tulishayaona na tutaleta marekebisho kama addendum. Muda ulikuwa umekwisha, Zitto akaomba mwongozo wa Spika muda uongezwe kwa nusu saa Waziri amalizie kutoa maeleozo yake. Lakini waziri akakimbilia kusema amemaliza na kuondoka.

Maswali ya kujiuliza:
-Kwanini serikali haikuweka toka mwanzo addendum kuonyesha hayo marekebisho? (Inaelekea hawakuwa wanajua mpaka wapinzani waliposema).
-Kwanini Waziri amesubiri dakika chache za mwisho kukwepa maswali?
-Kiutaratibu, nyaraka zote nne si zinakwenda pamoja?
-Mbona hajajibu hoja ya Dr Slaa ya baadhi ya kodi kufichwa na serikali kwenye vitabu lakini kwenye hotuba ya waziri hazijajitokeza?
 
waziri wa fedha muda mfupi uliopita amekubaliana na hoja ya Dr,slaa na wabunge wa upinzani kuwa ni kweli vitabu alivyowasilisha vya mapato vimekosewa na hivyo watawasilisha vitabu vingine.

Kwa mujibu wa taarifa zake ni kuwa amewapongeza wabunge wa upinzani kwa kuwa watu makini na wanaosoma na hivyo kuweza kuiamsha serikali.
 
Back
Top Bottom