Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

waziri wa fedha muda mfupi uliopita amekubaliana na hoja ya Dr,slaa na wabunge wa upinzani kuwa ni kweli vitabu alivyowasilisha vya mapato vimekosewa na hivyo watawasilisha vitabu vingine.

Kwa mujibu wa taarifa zake ni kuwa amewapongeza wabunge wa upinzani kwa kuwa watu makini na wanaosoma na hivyo kuweza kuiamsha serikali.

...... ujumbe huu una ashiria nini kwa wabunge wa CCM?
 
Huyu Mkulo kweli kituko hii chini hapa kali ya mwaka!

Dkt. Slaa alitaja dosari nyingine ni kuwapo kwa kitu kilichoitwa Tanzania Habours Corporation na kuhoji ni kitu gani na kwamba kama Serikali haijui majina ya taasisi zake ni hatari.
 
Dr Slaa live long life!MUNGU azidi kukutia nguvu na kukupa maarifa zaidi na kukuongezea Hekima!asingekuwa slaa hiyo ingepita hivi hivi
 
Amedai kuwa vitabu hivyo vya matumizi na mapato sio sahihi kwani viliweza kuandaliwa mwezi mei.

Kesho asubuhi atatoa vitabu vingine kwa ajili ya kuviwasilisha .

Swali la kujiuliza ni je? wabunge walikua wanajadili kitu gani kwa wiki nzima?

kama kesho atawasilisha vitabu vingine je?wabunge wataweza kupewa muda wa kuanza kujadili upya bajeti?kwani walikua wanajadili kitu ambacho ni uongo.
 
Huyu ni taahira mkubwa,inatakiwa awajibishwe.Upinzani hawana haja ya pongezi wanataka kuona accountability.Huo uhayawani wake hauwezi kuishia hewani hivi hivi lazima ipelekwe hoja ya kum-discipline.Hilo gap hapo la billions lingewagarimu sana watanzania either directly or indirectly.it sounds bogus .Lazy minister!
 
Hii kali hata waziri kumbe anasoma kitu ambacho hakijui? Hayo alitakiwa ayaseme mwanzoni
 
Amedai kuwa vitabu hivyo vya matumizi na mapato sio sahihi kwani viliweza kuandaliwa mwezi mei.

Kesho asubuhi atatoa vitabu vingine kwa ajili ya kuviwasilisha .

Swali la kujiuliza ni je? wabunge walikua wanajadili kitu gani kwa wiki nzima?

kama kesho atawasilisha vitabu vingine je?wabunge wataweza kupewa muda wa kuanza kujadili upya bajeti?kwani walikua wanajadili kitu ambacho ni uongo.

Mod
Unganisha hii na hii
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=14538

Tuendelee
 
Amedai kuwa vitabu hivyo vya matumizi na mapato sio sahihi kwani viliweza kuandaliwa mwezi mei.

Kesho asubuhi atatoa vitabu vingine kwa ajili ya kuviwasilisha .

Swali la kujiuliza ni je? wabunge walikua wanajadili kitu gani kwa wiki nzima?

kama kesho atawasilisha vitabu vingine je?wabunge wataweza kupewa muda wa kuanza kujadili upya bajeti?kwani walikua wanajadili kitu ambacho ni uongo.

huyu mpuuzi lazima awajibishwe kwani taifa limeingia hasara kwa kugharamia vikao vingine visivyo na msingi
 
Ndio maana naamini kabisa Dr. Wilbroad Slaa ndie mtu anaefaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Uchaguzi wa mwaka 2010. Dr. Slaa ameonyesha upeo wa juuu katika kuchanganua hoja mbalimbali na pia kuwa makini katika kupitia miswada muhimu kwa taifa. Asilimia kubwa ya wabunge vichwa maji wa CCM walikuwa wanaisifia bajeti ilihali ilikuwa na makosa kibao. Again Dr. Slaa for President 2010 na hatutaki tena bunge kujazwa na asilimia kubwa ya wabunge vichwa maji kutoka Chama Cha Mafisadi (CCM)
 
Pamoja na mapungufu yooote na uongo wa vitabu bado wabunge wa chama changu wataendelea kuisifu bajeti na hotuba ya waziri pamoja na kuiunga mkono mia kwa mia
 
Mkullo kasema pia kuwa wabunge wa upinzani ni makini na wanasoma ,je?wabunge wa CCM sio makini?
 
Jamani ilikuwa ni bakhti mbaya, wasameheni CCM, hamtambui 31% ya Raia hawajui kusoma na kuandika?
 
Kesho asubuhi atawasilisha vitabu vingine, je?hili ni suluhisho?

Tafsiri ya hili jambo ni nini?

Ni kuanguka kwa serikali na bajet yake? ni kuwa walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea?

Je?wale wabunge waliokuwa wanaiunga mkono asilimia mia kwa mia wataendelea kusema kitu gani?

Wabunge waliowakebehi wapinzani wataweka wapi nyuso zao?
 
Jambo jingine ni kuwa Zitto ,alisimama na kutaka waziri aongezewe muda wa ziada ili kueleza bunge kwa kina ,ila waziri alikataa kuongezewa muda huo.

Kwa mujibu wa kanuni za bunge ni kuwa kinachopitishwa kama bajeti ni vitabu vya bajeti na sio hotuba ya waziri.

sasa waziri kasema kuwa hotuba yake ndio sahihi swali la kujiuliza ni kuwa je? bunge linaendelea kufanya kazi gani kama vitabu tayari kavikataa?

Kesho ni siku ya kumuuliza waziri mkuu maswali live ,hivyo patakuwa hapatoshi.
 
Kesho asubuhi atawasilisha vitabu vingine, je?hili ni suluhisho?

Tafsiri ya hili jambo ni nini?

Ni kuanguka kwa serikali na bajet yake? ni kuwa walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea?

Je?wale wabunge waliokuwa wanaiunga mkono asilimia mia kwa mia wataendelea kusema kitu gani?

Wabunge waliowakebehi wapinzani wataweka wapi nyuso zao?

Mkuu,not at all.Hilo sio suluhisho na lazima atoe maelezo kwa nini uzembe mkubwa kama huo ukafanyika na hapo ndipo tutakapoweza kujua suluhisho sahihi.Yaani hata kabla hela hazijaidhinishwa tayari madudu yameshafanyika? Je,zikiwekwa katika matumizi itakuaje? Huko wanako-spend hiyo bajeti basi kutakua na madudu makubwa sana kuliko haya.
 
Back
Top Bottom