Bwashee shida ya nyie vijana was CCM hamsomi.Kazi yenu kuungajuhudi tu. In hivi, kwa mujibu was Mkataba wa Ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki, hizi nchi zinashirikiana katika masuala kadhaa ya ya kodi, hususan lile la Common External Tariffs (CET) ambayo ni kodi inayotozwa kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje. No lazima kodi hizi zifanane kwa nchi zote. Makubaliano ya vuwango vya CET huwa yanafikiwa kutokana na vikao vya mawaziri wa fedha vinavyofanyika wiki kadhaa kabla ya bajeti. Maana yake ni kwamba lazima bajeti zisomwe siku moja. Ikiwa zitasomwa siku tofauti, wafanyabiashara wa nchi ambayo itachelewa kusoma bajeti yake watapata faida. Nadhani sasa umeelewa bwashee!