Maneno matakatifu yalivyosema kwa tajiri kuona ufalme wa Mungu ni rahisi ngamia kupenya tundu la sindano ni kweli. AZAM TV ina channel ya Sinema zetu inayoonesha movie za kibongo kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 2. Hii channel mtu amejipinda amelipia sh 12,000 kwa mwezi. Ni kipindi cha saa 1 moja movie 2, sasa kero kila baada ya dk 5 ni matangazo, hiki kipindi mtazamaji amelipia, kwanini mnadhulumu watazamaji muda wao walioulipia? Ktk dk 30 unakuta dk 10 ni matangazo ukizingatia wanajua ina watazamaji wengi. Bakhresa ukimwangalia ni mtu wa dini ila ni mdhulumaji tu km wengine, kweli tajiri haridhiki, anaona ni sawa kudhulumu hata hawa maskini!
TCRA wamelala, hawaoni huu ni wizi? Basi km mnapitisha matangazo yenu iwe bure km channel zinazorusha taarifa ya habari.