Bakhresa muogope Mungu wako. Uwiano wa hasara ni mkubwa kuliko faida

Misaada yake mengine haiendani na haja halisi za watu.Na hana watu wazuri wa kumshauri.
Sijui ni nani aliyemshauri kujenga viwanja vya mpira badala ya kuwaunga mkono wafanyabiashara wa kiislamu kwanza au kuendeleza masuala ya kielimu.
Kwa nini aunge mkono wafanyabiashara wa kiislam tu? Unatenda dhambi ya ubaguzi
 
Kwa nini aunge mkono wafanyabiashara wa kiislam tu? Unatenda dhambi ya ubaguzi
Kwa sababu inajulikana waislamu walidhulumiwa sana kiuchumi wakati wa ukoloni na wakati wa Julius Nyerere raisi wa mwanzo wa Tanzania.
Yeye akianza nao atakuwa amefanya uadilifu wa mali zake.Na hakatazwi kuwafanyia wengine kwa yale yaliyo halali.Hata wakristo hapaswi kuwasaidia katika haramu kama mpira au kuwajengea mabaa.
 
Mengi ya hayo yanachochewa na matendo ya matajiri.Watu wanaiba na kucheza kamari ili wakashuhudie anachokitangaza Bakhresa kwa nguvu kwenye runinga.
hakuna kitu kama hicho.
Siku ya mwisho ya hukumu kila mtu atabeba msalaba wake huwezi ukawaambia malaika wa adhabu eti mimi nilishawishiwa na Bakhresa nikaibe na kucheza kamari haikuwa maamuzi yangu,haiingii akilini
 
Mkuu mbna unatumia mtandao wa makafiri?, mbna unatumia simu iliyotengenezwa na makafir?
 
Hizo dini za kuletewa zisitutoe kwenye njia za mafanikio

Kwa takwimu zangu Matajiri walio wengi Tz ji Waislam, why amkabe huyu tu.acha hizo mtoa hoja! Noma sana. Yaaji hutaki tuangakie mpira.
Jitahidi kuishi vema duniani uwwe na furaha na average pia ukaenjoy.
 
Halafu anawaua wananchi kwa kuwauzia bidhaa za kemikali kama vile juice na ukwaju vitu ambavyo havina uhalisia katika hali halisi. Anawatilia watu harufu za maembe na ukwaju kwenye vyakula jivyo ili kuwaua kwa makusudi. Mungu anamuaona.
 
KAMA KUNA MEMA KAMA KUJENGA MISIKITI NA KUTOA SWADAKA HUWEZI KUMHUKUMU,INAWEZEKANA YEYE HAHUSIKI NA MAMIPIRA WAHUSIKA WAKAWA NI WANAE MAANA MKUU WA MAKAMPUNI YOTE NI MWANAE.
Kama ni wanawe kweli na wamekuta mali za baba yao basi awakanye na ajitangaze kujitoa kwenye upuuzi wao.
Na aharakishe kabla siku haijafika.
 
hakuna kitu kama hicho.
Siku ya mwisho ya hukumu kila mtu atabeba msalaba wake huwezi ukawaambia malaika wa adhabu eti mimi nilishawishiwa na Bakhresa nikaibe na kucheza kamari haikuwa maamuzi yangu,haiingii akilini
Una uelewa kiasi.Sasa hapa tunajizungumzia wenyewe.Kwa sababu kila anayesaidia wema atalipwa sawa na wema utakaotendeka na pia ukisaidia uovu utalipwa kwa uovu utakafanyika,
Ukiwa na akili nzuri huwezi kumsaidia mwenzako kufanya matendo maovu.
 
Mkuu mbna unatumia mtandao wa makafiri?, mbna unatumia simu iliyotengenezwa na makafir?
Nani kakwambia kuwa mtandao ni wa makafiri au simu ni ya makafiri.Tumezungumza huko nyuma kuwa chanzo cha uelewa wa yote haya ni elimu iliyoratibiwa na waislamu.
Kwa maana hiyo elimu tuliyonayo ni milki ya Allah.Wazungu baada ya kusoma wameongozwa tu kujua kile Allah alichoridhia kijulikane na kwa hekima zake.Haya tunayoyajua leo ni madogo kuliko yatakayojulikana kesho yetu.Muda yawezekana yakapitia kwa wazungu wenye nia nzuri au kwa waislamu wenyewe watakapozinduka kutoka usingizini.
Mitandao na simu ni nyenzo za kupashana habari za Mwenyezi Mungu ili kila mmoja amjua na amuabudu.Hapo baadae kusiwe na kisingizio kuwa hakusikia au hakujua.
 
Una uelewa kiasi.Sasa hapa tunajizungumzia wenyewe.Kwa sababu kila anayesaidia wema atalipwa sawa na wema utakaotendeka na pia ukisaidia uovu utalipwa kwa uovu utakafanyika,
Ukiwa na akili nzuri huwezi kumsaidia mwenzako kufanya matendo maovu.
Hapana.
Statement yako ingekuwa na nguvu kiasi kama Bakhresa angekuwa anakufuata hadi nyumbani kwenu kisha anakushika mkono muende kwenye jumba la betting hapo sawa,lakini kama uliamka nyumbani kwako ukaplan mwenyewe kisha ukapanda gari hadi kwenye jengo wanalobet na ukalipia mwenyewe wakati huo Bakhresa hata hakuoni yuko nyumbani kwake na familia yake
 
Cha ajabu unatumia jamii forum ya kafiri tafuta hela mzee hizi kelele hazitokusaidia chochote maishani🤣🤣🤣
 
Hiyo Betting na kuwatia watu wazimu wa kupiga mayowe mabarabarani ni sehemu tu ya shida alizozileta.Nyengine ni kwenye majumba yetu.Namjua jirani yangu ambaye kawa kama kiwete kwa kukaa kuangalia michezo ya kituruki.
Namjua na mwengine kaenda hija kabisa lakini tangu arudi anafuatilia tamthilia tu badala ya kusoma Qur'an na kuswali kwa wakati vipindi vyote vya swala.Bakhresa ndiye sababu.
 
Ni akili yake tu haitafakari vizuri.
Unataka kuniambia na huko uturuki zilikotengenezwa hizo movies watu wa huko pia hawaendi kazini wanakaa ndani siku nzima kuangalia tv?
 
Ni akili yake tu haitafakari vizuri.
Unataka kuniambia na huko uturuki zilikotengenezwa hizo movies watu wa huko pia hawaendi kazini wanakaa ndani siku nzima kuangalia tv?
yawezekana wale wanaocheza wamelipwa tu wafanye kazi ya kuitangaza Uturuki kwa watu maskini . Hakuna hata anayewajua kule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…