Bakhresa muogope Mungu wako. Uwiano wa hasara ni mkubwa kuliko faida

Ukute kwenye familia wewe ndio tegemezi wa kutoa muongozo.

Yani umekaa chini kabisa ukaona hiki kinafaa kuandikwa.

Sijui unatambua kuwa nchi hii ina watu imani tofauti na ya kiislam?
Ndio maana nikamshauri.Hizi biashara nyengine hazimfai yeye.Aache uroho wa mali.
Mali na watoto ni fitna lazima ujilinde.
 
Na mimi nakubaliana na wewe
 
Hivi mkuu unashindwa kuelewa kuwa huo mpira umepatia ajira maelfu ya watu!?
Hivi mkuu unashindwa kuelewa kuwa hivyo visimbuzi vimepatia maelfu ya watu ajira??
Hujui kama kuna channel za kiislam ndani ya kisimbuzi hiko hiko??
Mkuu umewaza pafupi sana.
 
Hakuna watu wenye utajiri wa shirk kama watu wa iman ya akina tajiri huyu. Bila shirk na majini hakuna kitu nawe unalijua vizuri jambo hilo. Sasa unapomwambia huyu tajiri aache fedha haramu atawezaje wakati fedha yake inapatikana kwa kuwalisha majini damu za watu?
 
Kila mtu afanye anachoona kwake kina mashiko ilimradi havunji sheria za nchi. Dhambi au wema vinamhusu yeye na Mungu, vinginenevyo ni kuingilia yasiyokuhusu.

Hao wanaoangalia nani kawalazimisha? Nani kakwambia kujenga msikiti ndio tiketi ya kwenda mbinguni?

Acha Bakheresa anachoona kinamfaa.

Vipi kama hana mpango wa kwenda mbinguni, mbona unamchagulia bhana.
 
Shida ni kwamba watu wanaojikuta wanaijua sana dini na Mungu mnawachagulia watu dhambi za kufanya.

Una dhambi zako hauna utakatfu na mzee wa watu mwache na dhambi zake alizochagua zifanya.

Kila mtu hapa duniani ana dhambi zake basi tusichaguliane dhambi za kufanya.

shinda mechi zako na mzee ashinde zake, Kuni tutakutana nazo huko zituchome wote.
 
Acha wivu.Mambo ya Bakhresa na Mungu wake waachie wao.Fanya yako
 
Ukiwa na kifikra za kuwachukia baadhi ya watu sababu haupo nao imani moja basi moja kwa moja wewe una fikra za kimaskini we endelea kupambana na makafiri wewe ulie mnyoofu (Ama kweli Nyani haoni kundule)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…