Bakhresa muogope Mungu wako. Uwiano wa hasara ni mkubwa kuliko faida

Bakhresa muogope Mungu wako. Uwiano wa hasara ni mkubwa kuliko faida

Leo tena viongozi wako wa dini ili kuyapa umaarufu, mwamko na mwitikio mashindano ya wanawake kusoma kuran wameona inanidi kuwashirikisha watu wa soka na kukamilisha hilo wamewaalika wasemaji wa Yanga, Simba na Azam.
Bado utataka kupinga?
Ndio tunaowaita masheikh ubwabwa hao.Wanatumia njia ndefu kufikisha ujumbe kumbe njia nyepesi kupitia vipaza sauti vyao wanayo.
 
Huna hoja kuhusu unaloliongelea.
Madhumuni ni ujumbe umfikie mlengwa kwa njia iliyo nyepesi.
Unataka nipeleke maombi kwa ajili ya kutoa mawaidha.Enzi zimebadilika kama yeye anavyoweza kuwapotosha mamilioni ya watu kwa dakika moja na kwa wiki nzima.Na mimi naweza kumfikishia ujumbe hata kama amejificha kwenye makasri yake.
Ukisoma kwenye surat Alaq kuwa Allah ni mkarimu basi ukarimu wake ndio kama huo.
Wewe ni mnafki, wacha unafki na roho mbaya! Ondoa uchafu huo shekhe. Unataka kukemea watu hali na wewe ni mwenye dhambi kibao basi mbona usiikemee nafsi yako?
Hakuna atakayeingia kwenye pepo ya Mwenyezimungu bali kwa Rehma zake, itakase nafsi yako ndo uje ukemee ya wenzako
 
Ni kweli pepo ni kwa rehma za Allah.Na hizo rehma nazo zina masharti kutokana na ulivyoishi hapa duniani.
Mtu mchawi na muuwaji mpaka dakika ya mwisho unadhani hizo rehma zitamfikia kihivi hivi tu.
 
Eti "unawanyonya kina mama kwa kuwanunulisha vifurushi vya king'amuzi" bro unauhakika afya yako ya akili ni nzima???? Arguments zako zimejaa chuki na wivu.
Fafanua vizuri tuone kama na wewe una akili kweli za kujadili mada nzito kama hii.
Kwani hujui kuwa akinamama ndio wateja wakubwa wa Bakhresa kwa tamthilia na wanaume ni mateja ya mpira na kubeti kunakosababishwa na yeye.
 
Sasa kuna aliyedhulumiwa hapo ? Your logic should also imply unaponunua muda wa maongezi umedhulumiwa? Kwamba atoe huduma za king'amuzi bure ili asidhulumu watu? Na huduma za mawasiliano pia ziwe bure?
 
Katika historia ya utajiri wako ulianza kwa kushona viatu. Baadae ukaanza kuuza karanga na mikate. Allah kwa shani zake akakuzia biashara zako mpaka sasa unamiliki makampuni yaliyotanda nchi kadhaa za kiafrika na unajulikana dunia nzima kama mmoja wa matajiri wakubwa wa Afrika.

Utajiri wa viwanda vya ngano na vyenginevyo halali umeona havikutoshi umejiingiza kwenye biashara ya mpira na kupotoa watu kwa michezo ya kuigiza ya kipuuzi kutoka Uturuki, Korea na kwengineko.

Unawanyonya sana akina mama kiuchumi kwa kununua visembuzi vyako na kujaza salio. Na kwa upande wa akina baba unawajaza kwenye viwanja na mabanda ya kuangalia vidio mpaka wanakuwa kama wendawazimu kuangalia ligi mwaka mzima zinazofadhiliwa mpaka na makampuni ya bia.

Nasikia wewe ndiye uliyefadhili ujenzi wa msikiti mkubwa wa Mtoro karibu na nyumbani kwako pale mtaa wa Livingstone. Kuna na misikiti mengine umejenga kimya kimya na hata pitalu huwa unagawa nyakati za alfajiri.
Kwa hesabu za kidunia wale wanaongia msikitini kuswali Mtoro na wale wanaoacha kuswali kwa kuangalia mipira ya dunia nzima basi wanaingia msikiti ni wachache sana.

Mezani ya wema unaofanya kujenga misikiti michache na kuwapotosha mamilioni ya watu havilingani kabisa.
Wacha biashara hizo haramu na urudi kwenye uchumi halali bado upo hai. Biashara haramu waachie makafiri wazifanye.
Watoto na mali ni fitna sana.
Allahu a'alam,

Acha huyo mungu wake ndiyo ata dili naye
Na wewe baki na huyo mungu wako
 
Sasa kuna aliyedhulumiwa hapo ? Your logic should also imply unaponunua muda wa maongezi umedhulumiwa? Kwamba atoe huduma za king'amuzi bure ili asidhulumu watu? Na huduma za mawasiliano pia ziwe bure?
Dhulma kwa muktadha wa mawaidha haya ni kuwashawishi watu kufanya kitu kiovu halafu wewe ukafaidika kwa njia ya kupata mali.
Wote wanaotoa pesa zao ili wasipitwe na mambo anayoyatangaz kwenye runinga yake wamedhulumia japo wengi hawajielewi.
 
Acha huyo mungu wake ndiyo ata dili naye
Na wewe baki na huyo mungu wako
Mungu wake ndiye huyo huyo Mungu wangu na ndiye aliyefafanua yepi ni laghwi za kidunia zinazoweza kumuingiza mtu motoni kama hatotubu.
 
when I was broke nobody advised me how to make money,now that am rich everybody advises me how to utilise my money.
I didn't change,you changed
 
mimi sikubaliani na mtazamo wa kidini wa mleta mada

LAKINI

ni kweli kabisa kwamba matajiri wakubwa walio wengi ni wadhulumishaji

Ubepari unaumiza wengi, ndo ulivyo.

Wamarekani wengi wanalalamika sana huko mitandaoni kwamba matajiri wao hawadhibitiwi na serikali, wanajikusanyia mali mwisho wa siku wanashikilia asilimia kubwa ya uchumi.

Fuatilia kuhusu 'wealth inequality'

Sijui hilo linapswa lichukuliwe vipi lakini kimsingi ni ukweli.
Sikia ndugu,wewe unamuona Bakhresa au Mo dewji ni mnyonyaji kwa vile tu ni watu maarufu ila kila mtu ana madhambi yake kwa kiwango chake nitakupa mfano.
Kwa mfano mitaani kuna vibaka wanaopora watu mali zao,kuna wanaovunja milango na kuiba je ni halali?
Haya mitaani kuna watoto yatima wewe uliwahi kuwakumbuka kuwapelekea hata kilo 3 za mchele?
Kuna watu mitaani wanakopa hela kwa mtu halafu wanapotea hawarudishi je hii ni halali?
Mifano iko mingi sema tu kwa vile Bakhresa ni tajiri unasahau kwamba na yeye ni binadamu unataka awe kama malaika
 
Una makasiriko sana tunajaribu kukuweka sawa au unataka tukupe baadhi ta matukio ya umafia yanayoyofanywa na matajiri ili ufunge kabisa vidole vyako visije tena kuandika hoja za kuwatetea?
Kwani kwa maskini ndio hakuna Umafia?
Kwa mfano uswahili mtu anakutoboa tumbo kwa bisibisi ili akukabe na kukupora simu yako huu sio umafia?
 
Back
Top Bottom