Bakwata, tani 50 ya Tende zilizotolewa kama msaada na Saudi Arabia zimepelekwa wapi?

Bakwata, tani 50 ya Tende zilizotolewa kama msaada na Saudi Arabia zimepelekwa wapi?

Kuna msikiti mmoja alitokea mfadhili anataka kuujenga ,

Sasa akaongea na mashehe wa.pale wakakubaliana kuwa atawapatia fedha ili wao ndio wasimamie ujenzi.

Mfadhili kabla ya kutoa fedha akaona awapine viongozi wa msikiti kama watakuwa waaminifu,

Akatoa ngombe kadhaa kama zawadi wachinjwe na nyama zigawanywe Kwa waumini akawapa jukumu Hilo viongozi wasimamie yeye akakaa kuangalia namna watavyofanya.

Basi baada ya kuchinja tu, mfadhili akawa anaona namna migao inavyokwenda yaani mifuko tu inapita kupelekwa Kwa viongozi waumini wakaachwa kama walivyo.

Baada ya kuona namna viongozi wa msikiti walivyojipendelea kwenye swala dogo tu la kusimamia mgao wa nyama, mfadhili akaona asitishe nia yake ya kuwapatia viongozi fedha Kwa ajili ya ujenzi wa msikiti.

Kilichotokea katika msikiti huo hakina tofauti sana na ishu hii ya tende.
 
Huku unaponda na kule unapongeza.
Mudy jangwani kala tende kwa kudra ya ALLAH, tende tunda lililo barikiwa kuliko matunda yote mti wake unastawi jangwani kuliko mparachichi, muembe na mzabibu
Unajua apple wewe,adam mwenyewe alisalimu amri alivyopewa na hawa sijui eva,tende sio tunda ni mbegu
 
Dah! Umaskini ni shida. Hadi tende imekuwa issue kwa mwananchi na aliyekabidhiwa 😁
 
Tende ni kitu gani,Bakwata wanapiga mpaka ardhi ndo itakua tende!?,na sio Bakwata tu taasisi chingi za dini ni wapigaji tu.
Kwa kifupi watanzania upigaji ndo hulka yetu.
 
1624518066000.jpg
 
Waumini wana Haki ya kuoji Tende. Mbinu nyingine imetumika kuhoji hizi tende majibu yamekosekana kutoka kwa viongozi wao.
Mtu sahihi wa kufikisha shida zao kwa BAKWATA ni Rais
Tuwaache Waislamu wenyewe. Maana uislamu ni Dini ya Haki
 
Ndiyo hizo zinazouzwa na wamachinga kwenye kingo za barabara...
 
Mkuu, huwa inakuwa hivi, panapofanyika ibada ya Hijja kuna sehemu katika ibada hiyo kipengele cha kuchinja, sasa tafakari ule mjumuiko woote kila mmoja ni lazima achinje hebu nambie kutakuwa na nyama kiasi gani? jibu ni kuwa kutakuwa na tonnes za nyama na haiwezekani kwa saudia peke yao kula kiasi chote cha nyama hiyo na ndio maana zinagawanywa katika baadhi ya nchi kama sadaka na si kama wanazidump huku kwetu, ninaamini safari hii hazitokuwapo kwa kuwa hijja imezuiwa kutokana na covid.
Ni kwa dhana hiyo mkuu na si vinginevyo
Kati ya zinazobaki, grade one huwa zinauzwa ,hawazigawi bure, zile reject ndio zinagawiwa bure Afrika. Pia hao ng’ombe hununuliwa na mahujaji wenyewe, sio Saudi
 
Kati ya zinazobaki, grade one huwa zinauzwa ,hawazigawi bure, zile reject ndio zinagawiwa bure Afrika. Pia hao ng’ombe hununuliwa na mahujaji wenyewe, sio Saudi
Sawa mkuu, nimebase zaidi kwenye nyama, ni kweli kabisa mahujaji hununua wenyewe mifugo lakini baada ya kufanya ibada ya kuchinja kichinjwa hubakia kule na serikali ndio hushughulikia na mwisho wa siku nyama hugawanywa katika mataifa mbalimbali nasi ni wamojawapo mkuu, tatizo ni walokuwapo mbele.
 
Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, mwenye kuijua vizuri historia ya nchi yetu na amani yake, HAKUNA CHOMBO AMBACHO KINASTASTAHILI HESHIMA KAMA BAKWATA. MUNGU AENDELEE KUWALINDA NA KUWAONGEZEA HEKMA VIONGOZI WA BAKWATA

Huenda sifahamu, Nielezee yapi ambayo Kama BAKWATA imefanya kwa ajili ya manufaa ya Umma wa kiislam
 
Hadi issue ya tende mama ndio asuluhishe? Hebu kuweni serious kidogo. Malizaneni huko huko misikitini. Mama ana kazi kubwa za kitaifa, hizo petty issue mpelekeeni mufti.
Huyu si muislam aloandika,watu wa humu wanajulikana sana
 
Ilikuwaje hao waarabu wakaleta tende? Yani waliombwa msaada huo au?
 
Wangeomba masaada hata wa kujengewe hospitali ama shule ili angalau wapunguze wajinga kwenye familia ya mudi..lakni wanawaza tende..daah kweli dini ni ulaibu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom