Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Mkuu,,,hivi watu wote waliopo humu unawajuwa kwa majina halisi na shughuli zao? pamoja na hayo ,,wapo watu sio members na wana uwezo wa kusoma,,,kinacholetwa humu,, pia kama hujuwi fuatilia nyuzi nyingi za kero zinazoletwa humu,,baadae ya muda zinafanyiwa kazi na wahusika ,,na watu wanaleta marejesho,,,,,hivi mkuu unajuwa kwann members wengi wa humu wapo nyuma ya keyboard?na kuficha I'd zao?ni sababu mtandao huu unasomwa na known na unknown people,,,, je unajuwa Mimi nine chat na wewe ni nani?na nashughulika na nn? wewe. Usihangaike na hizo comments za member kum dis huyo jamaa mleta Uzi,, kuna watu wapo kazini,,,wata mdis lakini vitafanyiwa kazi,,amini maneno yangu,,,,
 
Mkuu umejinasibisha kwamba huna mihemko wala huendeshwi kwa mihemko ila hoja yako haishabihiani na Hilo.

Inaonekana kulalamikia ada ya kupokelewa shauri. Umewahi kujiuliza BAKWATA KATA wanaendesha ofisi kwa fungu lipi? Je kuna hesabu gani nyuma ya hiyo ada (deligation, mwendo wa kutoka ofisi za kata nk.,).

Kadhi anaendesha ofisi kwa mfuko upi? Analipwa mshahara na nani? Deligation inayoamua kesi hiyo Ina watu wangapi? Nk.

Hatuhalalishi wala kutete tozo, bali kila jambo huamuliwa kulingana na wakati na nyakati husika na kwa vigezo vile vile.

Mwanamke;
Anatoa wapi shilingi elfu 15,000 au 30,000? Nikidhani unazungumzia kwamba ananyanyaswa kingono katika HARAKATI za kuipata haki yake au anazungushwa kwa uamuzi usiosahihi na nk.

Hivi huyu mwanamke ambaye unadhani anahitaji talaka 45,000 inaweza kuwa kikwazo cha kutimiza ombi lake?

Unajua shauri likifika kule gharama ambazo mwanamke anatakiwa aziingie kisheria kuipata hiyo talaka (anatakiwa kurudisha mahari), je Kama aliolewa kwa 200,000/- unadhani atakuwa na uwezo wa kutafuta 200,000/ alafu akose 45,000/?

Usikubali kuwa mjinga kwa hiari.
 


Hilo swali ungemuuliza mleta mada kwamba anao ushahidi wa hicho alichokisema??, baada ya majibu yake ndipo tutaenda mbele zaidi kujua je sheria za kiislamu zinaruhusu jambo hilo nk.
 

Wewe ni mgeni wa JF inaonekana hujui nguvu ya JF au yawezekana wewe ni muhusika mmoja wapo huko Bakwata, wewe unafkiri yeye ataenda kusemea wapi?vyombo kibao vinasemwa kupitia JF na vinajirekebisha.
 
Naunga mkono aliyo yaandika mtoa mada, na hapa ngoja niseme machache kuhusu suala la "Kadhi". Katika soma soma yangu na kufatilia mambo ya dini, katika Uislamu hakuna sampuli ya majukumu ya kadhi kama yalivyo katika hizi mahakama za kadhi na sisi tulishawahi kuwashauri hata hizo mahakama za kadhi zisiwepo sababu kuwepo kwake tu kunaenda kinyume na Uislamu.

Na haya tunayo yaona ni matokeo ya wahusika kuuacha Uislamu.
 
Wewe ni mgeni wa JF inaonekana hujui nguvu ya JF au yawezekana wewe ni muhusika mmoja wapo huko Bakwata, wewe unafkiri yeye ataenda kusemea wapi?vyombo kibao vinasemwa kupitia JF na vinajirekebisha.
Kwa mfano wewe ukiwa ni kiongozi, utakapokuwa umekosea ungependa raia wako wakukosoe kwa namna gani.

Wasimame tu barabarani na kuanza kupayuka, kwa kuwa wanajua utasikia ilhali wanakuvunjia heshima, au wakufuate faragha na kukueleza makosa yako?

Tatizo sio kuwasema tatizo pahali gani anapowasemea.
 
Mleta mada kwani mahakama ya kadhi iliyokua inapiganiwa imeshapitishwa? Lini?
 
Vizuri ni vema ukawekwa uovu wazi ili iwe ni serious case waweze kujirekebisha... Baada ya kugundua umma umewafahamu uovu wao.. .
 
SISI KWENYE UISLAAM MWANAMKE ALIYEACHWA KWA MATATIZO YA MUMEWE ILIBIDI NDIO AANGALIWE NA APEWE SWADAQAH... BADALA YAKE WAO NDIO WANAMTOZA PESA YA LAZIMA. .. TABU JUU YA TABU...
 
Vizuri hebu nisaidie kulifikisha hili wewe.. .

WAAMBIE KULE JF KUNA MTU KAKUANDIKENI.. .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…