Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Hizi nasaha zako zingekuwa ni nzuri laiti kama ungelizifikisha mahali husika na sio kuja kulaumu mtandaoni.

Kwa BAKWATA hizi ni nasaha zako kwao, na kwa sisi wengine utatufanya tuzidi kuwaona wapigaji tu, kama ulivyosema.

Au ulitaka tujifunze nini kwa haya uliyoyasema?
Ungepita tu, mambo ni mengi kuna kuchukua fomu za kugombea.

SGR ,Stand ya Dodoma,Tanzania kuwa uchumi wa kati ...Kina Tale msiba na kuhamia kijijini.

Vitu vingi mno hukuona Heading ya uzi?
 
Hapa una uhakika napo kiongozi?
Mimi nazungumzia suala jingine wewe waleta mada nyingine. .. Kama sio wewe anzisha uzi wa hilo jambo tulidiscuss na uje na hoja za sio...
 
Moto Hakuna ..ni janja janja tu ya viongozi wa dini waliamua kutumia hivyo vitisho ili iwe kama trap ya kuwa kamata waumini kwa lengo la kuwatia hofu

Viongozi w dini wote wanalijua hilo ndio maana huwa wanatenda maovu kwa sababu wanajua hakuna masuala ya kuchomwa moto wala nini


All in all bandiko lako lina make senses
SISI WAISLAAM KUNA HOJA ZILIZO WAZI KABISA KUWA IPO SIKU TUTAFUFULIWA NA KUPEWA HESABU ZETU. .. WEMA PEPONI WAOVU MOTONI. ..

HATA HAO BAADHI WA BAKWATA NI MOTONI...
 
Nataka kufahamu kuwa huo ndiyo utaratibu rasmi wa Bakwata au ni utaratibu wa waliyomo Bakwata?
Kama suala lipo bakwata wilaya na wana bank account kwa ajili ya malipo, kwahiyo unataka ujifanye kipofu kumbe waona?
 
KUNA KAUTARATIBU KAPYA WAMEKAWEKA HAO BAKWATA. ..

KISHERIA NDOA YA KIISLAAM INAHITAJI MAMBO HAYA ILI IFANYIKE NA IPITE:-
1. Uwepo na KURIDHIANA kwa Muoaji na Muolewaji(Hakuna kulazimishwa katika dini ndio maana hakuna ndoa ya mkeka katika uislaam)
2. Uwepo wa Msimamizi wa Binti (Muolewaji) (tunaita WALII anaweza akawa Baba, kaka au IMAM)
3. MAHARI(Ni mali ya binti hiyo pekee yake)
4. MASHAHIDI ZAIDI YA WAWILI WA KIUME.
5. TAMKO LA KUOZESHANA("umekubali kumuoa? " " ndio nimekubali kumuoa au nimemuoa")

NDOA IKIKIDHI VIGEZO VYOTE HIVYO BASI MBELE YA ALLAH NA SHERIA YA UISLAAM NDOA HAPO IMEPITA HATA KAMA MPO WATANO TU.. .

Lakini ndoa inaweza ikakidhi vigezo vyote hivyo ILA BAKWATA WASIITAMBUE HIYO NDOA MPAKA UMPATE SHEIKH WAO AWEPO KWENYE NDOA NA LILE BANGO LAO LA NDOA(wanaita shahada)
Wakaweka na kautaratibu SHEIKH ATAKAYEKUWEPO ALIPWE SH. 50000/- NA LILE BANGO ILI UPEWE NALO 50000/-.

JE HAPO HUMKIMBIZI MTU KUOA KWA AJILI YA TAMAA ZENU ZA DUNIA... MAMBO AMBAYO KWENYE DINI HAYAPO NYIE MNAYASHIKIA KIDETE...
 
Nauliza hivyo ni kwa sababu Uislam unatutaka tujiepushe na baadhi ya dhana, kwani baadhi ya dhana ni dhambi.

Kwa sababu dhana ikiwa ni si ya kweli ni kuwa umemzushia mhusika uongo. Ni hatari vilevile kwa kuwa itakuwa imejengeka kwenye matamanio ya nafsi.

Waislam tunaifahamu Bakwata jinsi ilivyo! Lakini yanayosemwa haya ni ya kweli kuhusu Bakwata? Au ni utaratibu wa waliyomo ndani ya Bakwata?
VIZURI NIMZUSHIE ILI IWEJE WAKATI MIMI MWENYEWE NIMEFUATILIA KESI IMEANZIA BAKWATA KATA MPAKA WILAYA.. . WEWE NDIYE UNAYEDHANI SHARI BAADA YA KUKUJIA HOJA ZILIZO WAZI...
 
TANBIHI: Mods naomba uzi huu msiufute na mkiuhamisha basi nifahamisheni mmehamishia wapi?

Nayaandika haya nikiwa na uchungu mkubwa rohoni mwangu. .. Nikiangalia wale walio pewa mamlaka ya usimamizi wa sheria ya Allah wanafanya mambo mazito ya kumuasi Allah na kudhulumu watu...

Kwanza nibainishe MIMI SIO MTU WA KUENDESHWA NA MIHEMKO YA KIHARAKATI... SINA CHUKI JUU YA BAKWATA NA NAWAHESHIMU SANA KWA SABABU NDIO CHOMBO TEGEMEWA CHA KUWASEMEA WAISLAAM NCHINI NA KUISIMAMISHA SHERIA YA ALLAH. .. LAZIMA TUKITII NA TUKIHESHIMU BILA SHAKA. .. NA NAKITII NA KUKIHESHIMU CHOMBO HIKI. ..

Bakwata Mashaa Allah, Allah amejaalia lwa serikali hii kuruhusu WAISLAAM kujihukumia mambo yao msingi ya kijamii yenyewe na MIFUMO YA KIDOLA ikazitambua na kuzirasimisha sheria hizo(NDOA, TALAKA NA MIRATHI). . . NA HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA BAKWATA KWENYE MASUALA HAYO MAHAKAMA ZA NCHI HAZIWEZI INGILIA.. .

TUMSHUKURU ALLAH KWA HILO.. . Ni jambo mlilolipigania kwa muda mrefu kupata mahakama ya Qadhi, ili waislaam tujihukumie mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa kwenye ibada hizo. ..

Kumbe bhanaa wenzetu BAKWATA na BAADHI viongozi Wake waliliangalia kwa jicho la kimaslahi(LA KIUPIGAJI) . .. MCHENI ALLAH NYIE WATU.. . ADHABU YA ALLAH NI CHUNGU. ..HAMTOOKOKA NA VIREMBA VYENU WALA VYETI VYENU VYA THANAWY MLIVYOVIPATIA TANGA...

Mathalani. .. KWENYE MASUALA YA NDOA. .. SIKU ZOTE UKIONA SUALA HILO LIMEFIKA KWA QADHI UJUE MLETAJI NI MWANAMKE(MKE). ..

Kwa sababu Kisheria MWANAUME hapati shida amepewa Mamlaka, YAKIMKERA ANAACHA TU(TALAKA). ..

Ila mwanamke hana uwezo wa kutoa Talaka, Suluhisho lake ni kwa Qadhi...

Na kwa mfumo wenu wa uendeshaji QADHI MMEMUWEKA KUANZIA WILAYA kisha MKOA kisha TAIFA. ..

LAKINI wa kumpata huyo QADHI sasa ndio unaleta ukakasi. ..

Binti akiwa na tatizo kwenye ndoa yake na Mumewe anabidi aanzie shauri lake BAKWATA KATA ili lifike kwa QADHI WA WILAYA. ..

Huko KATA sasa ETI BINTI MASKINI ANATOZWA KUANZIA SH. 15,000/- Ili tu shauri lake lifunguliwe na lisikilizwe. ..

Tujue kabisa OFISI YA BAKWATA KATA HAINA MAMLAKA YA KUSIKILIZA NA KUIAMUA KESI ILI WATAPOTEZA TU MUDA WAKO ILA MWISHO WA SIKU UTAPEWA BARUA UENDE BAKWATA WILAYANI. ..

Ukifika BAKWATA WILAYA kabla hawajakusikiliza lolote... NENDA KADEPOSIT SH. 30,000/-...

ILA KUMBUKA MWENYE MAMLAKA YA KUSIKILIZA NA KUAMUA NI QADHI NA SI BAKWATA(Si sheikh wa wilaya wala katibu wake). . . Ila hela yako wanaitaka...

Kwahiyo mwisho wa siku lazima upelekwe kwa Qadhi. ..

Sijajua na hadi kufika huko kwa Qadhi nako inabidi utoe kiasi gani!

KINACHONIUMA ROHO SIO HELA WANAYOIPIGA. ..

Ila ni HUYU MWANAMKE aliyepeleka Kesi huko. .. KUMBUKA KISHERIA YA KIISLAAM MWANAMKE ANATAKIWA AKAE NYUMBANI NA WATOTO ALEE FAMILIA NA AMTII MUMEWE TU. .. Suala ya kufanya kazi limeruhusiwa kwa mwanamke ila INATILIWA NGUVU ZAIDI ASIFANYE KAZI. ..

ANAYEMHUDUMIA MWANAMKE NI MUMEWE. ..

SASA FIKIRIA Mwanamke amegombana na Mumewe anayemhudumia. .. Ikafikia hatua anahitaji msaada kutoka kwenu BAKWATA. .. LAKINI NINYI MNAMCHAJI OVER SHS. 45,000/- ILI APATE HUDUMA NA MSAADA WENU ILI APATE HAKI YAKE. ..

Sasa hiyo hela anaitoa wapi MDHAIFU HUYU. ..? BADALA YA KUMSAIDIA KUMPA HAKI YAKE MNAMUONGEZEA MATATIZO?

UISLAAM WENU MMEUTOA KWA SHEITWAANI GANI?

MBONA HATA HAMUMUOGOPI ALLAH... HIVI HATA MTUME ANGEKUWA ANAFANYA HUU UPUMBAVU WENU. .. HUU UISLAAM USINGEFIKA HAPA ULIPO. ..

MTUME AMESEMA "ZICHENGUENI HAKI ZA MADHAIFU WAWILI HAWA, NAO NI WANAWAKE NA MAYATIMA".

Lakini ninyi mnashiriki kuwakandamiza. ..

Mcheni Allah ndugu zangu. ..

MTAFANYA WAUKIMBIE UISLAAM NA WAULALAMIKIE UISLAAM KWA TAMAA ZENU ZA MAISHA YA DUNIA YASIYO CHOCHOTE. ..

MNATUPELEKA WAPI NYIE WATU MSIOMUOGOPA ALLAH. ..

MNA TOFAUTI GANI NA WAPIGA DILI WA RICHMOND NA WALA RUSHWA. ..

NYINYI MTACHOMWA KWA KUDHULUMU MALI ZA WATU KWA KUZILA PASIPO HAKI. ..

KAMA MLITAKA KIPATO MNGEKUWA NA SUBRA MKAMSIKILIZA HUYO DHAIFU ALAFU MWISHO MTWANGENI HIZO GHARAMA MWANAUME. .. ILA MWANAMKE MNAMUONEA ANAZIPATA WAPI?

AKIWA HANA MAANA YAKE AKAENDELEE KUMUASI ALLAH KWA ZINAA KWA MLOLONGO WENU KWA KUDHULUMU WATU. ..

mwisho:
NITOE TANBIHI NYINGINE... UISLAAM NA SHERIA ZAKE HAZINA SHIDA KABISA WALA HAZINA KASORO.. .

NA UKIZIFUATA NA ZIKASIMAMISHWA VIZURI KWA UADILIFU UTAUPENDA NA KUUFURAHIA UISLAAM. .. UTA ENJOY NA KUJIVUNIA KUWA MUISLAAM.

ILA HAWA WAPIGA DILI HAWA NDIO WANAOUCHAFUA UISLAAM...

NIMUOMBE MUFTI.. . BARAZA LAKO UNALOJITAHIDI KULISAFISHA NA KULIRUDISHA KWA UMMA... KUNA WATU WA MASLAHI WANAKUANGUSHA.. . WANALICHAFUA BARAZA KWA TAMAA ZAO ZA MATUMBO... MIJITU IMEJAZA VITAMBI NJAA ZIMEWAJAA HAWANA HOFU YA ALLAH... ADHABU YA ALLAH YAWANGOJA WASIPOTUBU. .. ALLAH AWAONGOZE. ..

NB: MODS TAFADHALI UZI HUU USIFUTWE MUHIMU SANA KWA UMMA...
ingekuwa busara kama ungefuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko au kero zako ktk ngazi inyayo husika, unacho kifanya hapa hakina tija yoyote kwako, kama kweli unania ya kujenga fuata utaratibu
 
Mkuu umejinasibisha kwamba huna mihemko wala huendeshwi kwa mihemko ila hoja yako haishabihiani na Hilo.

Inaonekana kulalamikia ada ya kupokelewa shauri. Umewahi kujiuliza BAKWATA KATA wanaendesha ofisi kwa fungu lipi? Je kuna hesabu gani nyuma ya hiyo ada (deligation, mwendo wa kutoka ofisi za kata nk.,).

Kadhi anaendesha ofisi kwa mfuko upi? Analipwa mshahara na nani? Deligation inayoamua kesi hiyo Ina watu wangapi? Nk.

Hatuhalalishi wala kutete tozo, bali kila jambo huamuliwa kulingana na wakati na nyakati husika na kwa vigezo vile vile.

Mwanamke;
Anatoa wapi shilingi elfu 15,000 au 30,000? Nikidhani unazungumzia kwamba ananyanyaswa kingono katika HARAKATI za kuipata haki yake au anazungushwa kwa uamuzi usiosahihi na nk.

Hivi huyu mwanamke ambaye unadhani anahitaji talaka 45,000 inaweza kuwa kikwazo cha kutimiza ombi lake?

Unajua shauri likifika kule gharama ambazo mwanamke anatakiwa aziingie kisheria kuipata hiyo talaka (anatakiwa kurudisha mahari), je Kama aliolewa kwa 200,000/- unadhani atakuwa na uwezo wa kutafuta 200,000/ alafu akose 45,000/?

Usikubali kuwa mjinga kwa hiari.
UISLAAM UMEWEKA UTARATIBU WA KILA KITU NA UISLAAM UNAENDA NA WAKATI...

Viongozi wanaosimamia dini wamewekewa utaratibu wa kujipatia kipato. .. Nao ni zakaa na swadaqah. ..

Lakini hawa hawaridhiki wakajiongezea na namna nyingine za upigaji na wala hazipo katika taratibu za uislaam

Wakati wa Mtume, kesi hizi zilikuwepo na pesa zilikuwepo, ila Mtume alipelekewa kesi na hakudai hata senti iwe kwa mume au mke... INA MAANA MTUME ALIKUWA HANA GHARAMA ZA UENDESHAJI?

Unatumia akili kwenye mambo ya dini. .. Eti mwanamke anayehitaji talaka hashindwi kutoa 45,000...HIVI UNAIJUA SHERIA YA DINI INATAKA MWANAMKE ATENDEWE NINI?

MWANAMKE MPAKA ADAI TALAKA KWA QADHI NI KWAMBA KWA MUMEWE HAITOKI NA KUNA MGOGORO. ..

CHUKULIA MWANAMKE NI MTU WA KUKAA NYUMBANI TU... HIYO HELA YA KUWAPA BAKWATA APEWE HAKI YAKE YA TALAKA ANAITOA WAPI...?

USILOPOKE LOPOKE USILOLIJUA UNAONGEA DHANA T. ..
 
Hivi mahakama za khadhi zimeshaihinishwa?

Naona mleta mada anazungumzia mabaraza ya usuluhishi ya ndoa.

Navyofahamu bado mamlaka ya kuvunja ndoa yapo kwa mahakama.
 
Hilo swali ungemuuliza mleta mada kwamba anao ushahidi wa hicho alichokisema??, baada ya majibu yake ndipo tutaenda mbele zaidi kujua je sheria za kiislamu zinaruhusu jambo hilo nk.
Ushahidi ninao wa malipo ya benki ya posta. ..
 
Naunga mkono aliyo yaandika mtoa mada, na hapa ngoja niseme machache kuhusu suala la "Kadhi". Katika soma soma yangu na kufatilia mambo ya dini, katika Uislamu hakuna sampuli ya majukumu ya kadhi kama yalivyo katika hizi mahakama za kadhi na sisi tulishawahi kuwashauri hata hizo mahakama za kadhi zisiwepo sababu kuwepo kwake tu kunaenda kinyume na Uislamu.

Na haya tunayo yaona ni matokeo ya wahusika kuuacha Uislamu.
Ahsante sana...
 
Kwa mfano wewe ukiwa ni kiongozi, utakapokuwa umekosea ungependa raia wako wakukosoe kwa namna gani.

Wasimame tu barabarani na kuanza kupayuka, kwa kuwa wanajua utasikia ilhali wanakuvunjia heshima, au wakufuate faragha na kukueleza makosa yako?

Tatizo sio kuwasema tatizo pahali gani anapowasemea.
KATIKA SHERIA KUNA KITU KINAITWA RADD... MTU ANASAHIHISHWA KWA KOSA ALILOLIFANYA HADHARANI.. .

YAANI UKOSEE HADHARANI KWA KUWAPOTEZA NA KUWADHULUMU WATU.. . ETI TUKUONYE KWA SIRI...
 
Kwa mfano wewe ukiwa ni kiongozi, utakapokuwa umekosea ungependa raia wako wakukosoe kwa namna gani.

Wasimame tu barabarani na kuanza kupayuka, kwa kuwa wanajua utasikia ilhali wanakuvunjia heshima, au wakufuate faragha na kukueleza makosa yako?

Tatizo sio kuwasema tatizo pahali gani anapowasemea.
Na je wao pia wamefungua mlango wa nasaha?

Watu wameitanguliza dunia mbele Je wataona umuhimu wa nasaha. . .
 
ANAYEMHUDUMIA MWANAMKE NI MUMEWE. ..
Kulalamika kwa waislam ni kawaida
Wewe kama muislam umetenga kiasi gani katika pato lako la mwezi kusaidia,yatima,wajane na watalikiwa?
Hao mashekhe pesa wanapata zaidi ya kupiga fatha na kupewa asante?
Mkiambiwa talaka katika uislam ni jambo gumu sana muelewe
 
Back
Top Bottom