Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Mbona unauliza maswali ya kizandiki mzee ? Kwamba unakataa hili halipo ?

Soma surat al Ahzab, mambo mengine msiwe mnauliza sababu mnakuwa mnautukana Uislamu.
Hii ndiyo hekima ya Quran na Sunnah uliyojifunza kutoka kwa Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake ya kuwa mmoja wenu akiuliza swali (mfano hapo la kidini) yakupasa na yampaasa ajibiwe kama ulivyojibu?

Ikiwa kama mwanamke ni mtu wa kukaa nyumbani vipi kama akiumwa hospitalini statistiwa na akina nani? Madaktari wa kiume ndiyo waushike shike mwili wake?
 
Kwanini Allah kupitia mtume wake SAW asiisambaratishe BAKWATA kama haiendani na matakwa yake yeye Allahu Akbar?
 
Sahihi kabisa, na Uislamu kadhalika unakataza kuwafanya watu wakudhanie vibaya. Unalijua hili ?
Ulichokiandika ni sahihi isipokuwa umemithilisha pasipokiwa sahihi. Nilichouliza kwa mleta Uzi ni kupata uhakika kwa sababu zifuatazo:

Bakwata si ya mtu mmoja mmoja bali ni Taasisi kama zilivyo Taasisi nyengine isipokuwa yenyewe ni ya kidini. Taasisi inakusanya watu wa aina tofauti tofauti ili kufikia na kutimiliza haswa lengo la Taasisi yenyewe, watu hao iliyowakusanya ni wafanyakazi.

Kwa mazingira ya Taasisini itatokelezea tu miongoni mwao ni wa tiifu na wengine ni watovu wa nidhamu. Ndiyo maana nikamuuliza mleta Uzi kuwa; Ndiyo utaratibu rasmi wa Bakwata au ni utaratibu wa waliyomo Bakwata? Kwa sababu yeye ameishutumu Bakwata nzima.

Sikutaka kuingia moja kwa moja kwenye Uzi mpaka anithibitishie hilo kwanza. Nisije nikahukumu Taasisi nzima kwa maana watu wote kumbe inawezekana wapo wengine wema wanaopambana kuweka mazingira mazuri ijapokuwa inafahamika historia yake ipoje.
 
Kama sio utaratibu hao kadhi wanaomba pesa za nini?mtoa post ndy hayo anayoyakemea
Usome vizuri tena Uzi. Alichokiandika ni hatua za awali alizopitia, huko kote ameambiwa atoe pesa. Yeye akasema kama hali ndiyo ipo hivi mpaka kufikia kwa Qadhi kiasi kingi cha fedha kitatoka.......
 
Kwahiyo nimebuni hapo hata hizo gharama au nikuletee risiti ya malipo ya benk.. . .?
Hakuna mahala nilipoandika nimebuni, hakuna mahala nilipoandika uniwekee risiti ya malipo ya bank! Bali nilichokihitaji kutoka kwako ni yakini.
 
Bakwata ni wahuni tu. Waislam inatakiwa tujipange ili tupate taasisi ya waislam.
 
Kama suala lipo bakwata wilaya na wana bank account kwa ajili ya malipo, kwahiyo unataka ujifanye kipofu kumbe waona?
Kama hali ipo hivyo si vyema kutupa shutuma. Ni vyema kuwa nasihi na kuwapa ushauri. Quran imetupa sifa ya tunaoneana huruma na Quran yenyewe inatutaka tuaidhiane kwa hekima.
 
VIZURI NIMZUSHIE ILI IWEJE WAKATI MIMI MWENYEWE NIMEFUATILIA KESI IMEANZIA BAKWATA KATA MPAKA WILAYA.. . WEWE NDIYE UNAYEDHANI SHARI BAADA YA KUKUJIA HOJA ZILIZO WAZI...
Usiwe ni mwenye ghadhabu.

Usiwe ni mwenye kuhukumu watu! Umejikita kuhukumu watu, haujajikita kuogopa kwa unachokifanya bali umejipa yakini kwa unachokifanya. Dini yetu ni ya Mungu tuwe na heshima na viumbe vyake.
 
Usome vizuri tena Uzi. Alichokiandika ni hatua za awali alizopitia, huko kote ameambiwa atoe pesa. Yeye akasema kama hali ndiyo ipo hivi mpaka kufikia kwa Qadhi kiasi kingi cha fedha kitatoka.......
Uzi nimeusoma na kuuelewa sana tu
 
Hii ndiyo hekima ya Quran na Sunnah uliyojifunza kutoka kwa Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake ya kuwa mmoja wenu akiuliza swali (mfano hapo la kidini) yakupasa na yampaasa ajibiwe kama ulivyojibu?

Ikiwa kama mwanamke ni mtu wa kukaa nyumbani vipi kama akiumwa hospitalini statistiwa na akina nani? Madaktari wa kiume ndiyo waushike shike mwili wake?
Soma kwanza aya uelewe kisha uulize maswali ya msingi,tatizo hata aya zenyewe hamsomi. Aya iko wazi, sasa nashangaa unavyouliza swali au kujenga hoja mufilisi namna hii.

Ahsante.
 
Bakwata ni wahuni tu. Waislam inatakiwa tujipange ili tupate taasisi ya waislam.
Wapalestina walimuendea Sheikh mmoja(nimemsahau jina) humo humo Palestina na kumwambia "Ya Sheikh! Tumemuomba na tunamuomba Mungu atupatie msaada dhidi ya utawala wa Wazayuni lakini hali ndiyo mbaya zaidi."

Sheikh akawajibu "Mbona msaada ulishakuja! Usipokuwa ulishindwa kuwatofautisha baina ya wanaodhulumu na wanaodhulumiwa kwa hiyo ukarudi kwa Mungu"

Taasisi ya Usilam ni sisi wenyewe Waislam. Ikiwa tunahitaji Bakwata iliyobora tubadilike sisi wenyewe kwanza na nusra ya Allah itakuja.
 
Kama suala lipo bakwata wilaya na wana bank account kwa ajili ya malipo, kwahiyo unataka ujifanye kipofu kumbe waona?
Swali la Hammaz kwamba tuna uhakika huo ndio utaratibu rasmi tusilichukulie kiurahisi! Hata serikalini kwenye, hususani ngazi ya kijiji na mtaa, na hata huko kwenye kata, wananchi huwa wanatozwa tozo hizi na zile lakini kimsingi sio utaratibu rasmi. Kwa mfano ukienda kutaka barua ya utambulisho, utaambiwa utowe kiwango fulani cha pesa lakini hilo suala halipo kisheria. Kuna wakati nilishtuka kidogo nilipoambiwa hata zile 10% wanazotaka mathalani unaponunua kiwanja, na wenyewe ule wala sio utaratibu rasmi. Ingawaje sina uhakika nalo sana hilo jambo lakini nakumbuka siku tumeenda kununua kiwanja Kigamboni, tukaanza ku-bargain hiyo 10% hadi tukaafikiana. Kuwauliza stakabadhi, jamaa hawana nasi tukagoma kutoa na hawakutufanya chochote. So, kwamba huo ndo utaratibu sahihi ama hapana lisiwe jambo la kupuuzwa manake kwenye taifa hili lolote lawezekana.
 
Back
Top Bottom