Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Mkuu umejinasibisha kwamba huna mihemko wala huendeshwi kwa mihemko ila hoja yako haishabihiani na Hilo.

Inaonekana kulalamikia ada ya kupokelewa shauri. Umewahi kujiuliza BAKWATA KATA wanaendesha ofisi kwa fungu lipi? Je kuna hesabu gani nyuma ya hiyo ada (deligation, mwendo wa kutoka ofisi za kata nk.,).

Kadhi anaendesha ofisi kwa mfuko upi? Analipwa mshahara na nani? Deligation inayoamua kesi hiyo Ina watu wangapi? Nk.

Hatuhalalishi wala kutete tozo, bali kila jambo huamuliwa kulingana na wakati na nyakati husika na kwa vigezo vile vile.

Mwanamke;
Anatoa wapi shilingi elfu 15,000 au 30,000? Nikidhani unazungumzia kwamba ananyanyaswa kingono katika HARAKATI za kuipata haki yake au anazungushwa kwa uamuzi usiosahihi na nk.

Hivi huyu mwanamke ambaye unadhani anahitaji talaka 45,000 inaweza kuwa kikwazo cha kutimiza ombi lake?

Unajua shauri likifika kule gharama ambazo mwanamke anatakiwa aziingie kisheria kuipata hiyo talaka (anatakiwa kurudisha mahari), je Kama aliolewa kwa 200,000/- unadhani atakuwa na uwezo wa kutafuta 200,000/ alafu akose 45,000/?

Usikubali kuwa mjinga kwa hiari.
Mcheni Allah enyi watu!

Kwahiyo pasipokuwa na kesi hata moja hapo bakwata kata hiyo ofisi haitoendeshwa???

Kwahiyo mmekaa mnaombea watu wapate madhila ili watoto wenu waende vyooni?

Hivi ndivyo mtume alivyoendesha shughuli za uislam??? Kama mmeshindwa kuitengeneza bayt al maal mna faida gani sasa kwa waislam??

Hivi mnadhani matajiri wa kiislam wangeshindwa kutoa zaka zao kwa ajili ya kuendesha harakati za uislam kupitia bakwata ikawa ndio chanzo katika hiyo bayt al maal?? Kwanini matajiri hao hawatoi chochote kwa bakwata??

Semeni na mitumbo yenu hiyo kwani hakika adhabu za Allah ni kali
 
BAARAKALLAH FIYK. .. Kuna watu hapa baba zao wako bakwata roho zawauma...

Tulieni ndivyo haki ilivyo huwa inapoingia inauma haswa. ..
 
DsmicSound itimilize haki ya Allah kwa kuwaelekeza watu waelekee kwake. Uovu hauondoshwi kwa uovu. Itangulize mbele huruma kutoka ndani ya moyo wako. Mtume rehma na amani ziwe juu yake alimkubalia Wahshi kuingia kwenye Uislam ijapokuwa Wahshi alimuulia Mtume uncle wake Hamza r.a ijapokuwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake alionelea ngumu kumtizama usoni pindi anasilimu. Hii nayo ni sunnah ya Mtume, tuifuate.

Ikiwa Allah anatuambia waja wake waliyokuwa na israfu ya madhambi wasikate tamaa kwenye rehma yake ni huruma ya namna gani hiyo? Tuwe na huruma na waliyopo chini, tutaonewa huruma na aliyepo juu.
Kwahiyo ndugu ndio tuache kukemea kwa njia ambazo tunajua ujumbe utafika haswa kwa sababu hizo???
 
Mtume amesema "zichengueni haki za madhaifu wawili hawa, nao ni wanawake

Mtume amesema "zichengueni haki za madhaifu wawili hawa, nao ni wanawake na mayatima".

DUUU!

WE NEED ELIMU DUNIA!
 
Mpuuzi wewe umekuja hapa kwa lengo la kujifanya una upole.. Kwenye Maasi juu ya Allah...
Ni wapi kwenye Uislam umeambiwa mtu akifanya maasi uwe mkali juu yake? Ni nini maana ya kauli ya nakusihi pamoja na kuisihi nafsi yangu?

Ipi hekima ya maneno haya aliyoyasema Mtume "Msaidieni mwenye kudhulumu na mwenye kudhulumiwa" Mtume ndiye anayeujua zaidi, inakuwaje Mtume hakusema mwenye kudhulumu amefanya maasi juu ya Allah achukiwe na akasirikiwe?

“Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa
hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.”(Sura An-Nahl; 16:125).

Allah mwenyewe anawaambia waja wake wenye madhambi na madhambi wasikate tamaa kwenye rehma yake. Tena hakuwatenga kwa kuwagawanya kwamba wanafanya wema na hawa wanafanya maovu ni wenye dhambi! La! Allah alituita kwa kauli moja wote kwa kutuita "Yaa ibadii" enyi waja zangu...kisha akatuambia tusikate tamaa kwenye rehma zake. Hata uwe na makontena ya madhambi katuambie msikate tamaa kwenye rehma zangu. Huyu ndiye aliyetuumba sisi inakuwaje wewe ni mwenye hasira zaidi kwa wanaofanya maasi juu yake kuliko yeye?

Na Allah huwa ananadi usiku "ni nani mwenye madhambi nimsamehe! Ni nani mwenye shida nimtimilizie..." Bahari huwa inamuomba Mungu iwazamishe ndani yake wale wote wanaopita juu yake wale wote wanaomuasi Mungu na waliyomajeuri kwa Mungu. Mbingu humuomba Mungu kila siku iibamize sehemu ya ardhi ya hii dunia ya wale ambao wanao muasi Mungu. Na ardhi inamuomba ruhusa Mungu iwameze wote wenye madhambi kwa Mungu. Allah anawajibu wote kwa kuwaambia "Hamjawaumba ninyi! Laiti ninyi mngeliwaumba msingelisema hayo" Kisha muangalie Mtume aliishi vipi na wale waliyomkosea yeye na ukimkosea Mtume umemkosea Mungu, Mtume aliishi nao vipi! Hata kwa wale waliyomkosea Mungu Mtume alikuwa anaamiliana nao vipi!?

Na hii ndiyo iliyokuwa kazi ya Mitume na kazi ya waliyorithi Mitume. Kingine sina chuki na yeyote.
 
Ndio mimi nipo njia salama kwa sababu kigezo changu ni Mtume na maswahaba zake.. . Wewe kabaki na quraniyyuun mwenzako faizafoxy na mashia wenzako. .. Achana na hii post kama inakuuma au kama baba yako yupo bakwata mpe ujumbe huu mwambie aache dhulma.. .
Mi sunni.
Kumfuata Mtume si kwa kusoma vitabu peke yake bali na kuyaishi. Napata tabu na waislam wa sasa hivi! Wanawachukia wenye maasi kana kwamba wao si wenye madhambi na hawatendi dhambi. Muda mwengine wanawaona wasiyo waislam nao duniani wamekuja kwa bahati mbaya.

Na napata tabu zaidi kumuona Muislam ambaye anayesema nafuata Quran na Sunnah lakini haamiliani na waislam wenzake vyema hata kwa njia ya mazungumzo. Hatari zaidi Muislam anajiona yupo safi kwa vile yeye ni Muislam. Halafu wanakuwa ni watu wa jazba!

Haya mafundisho yanatokea wapi? Ni Uislam wa namna gani huu?

Kwa nini usiwe na udhuru ukimuona ama ukitendewa sivyo! Kuna hadithi fupi ya kutungwa lakini ni yenye manufaa. Siku moja mbao ilimlalamikia msumari kwamba si mstaarabu na vurugu yake ni kubwa sana akimuingia. Msumari ukajibu kwa kumwambia; laiti ungiliiona dhoruba ninayopigwa nayo kichwani ungenipa pole.

Tuwape binadamu wenzetu udhuru! Na baba yangu hakuwa na hayupo Bakwata, baba yangu kipenzi alishafariki.
 
Unanisihi nini wakati ulikuwa unapinga. .. Baada ya kukwambia shahidi ni Allah na nikakwambia nikuletee docs za bank. .. Sasa unanisihi... Basi HUKUWA NA LENGO LA KUJUA UKWELI ILA ILIKUWA NI KUPINGA TU KWA MASLAHI YAKO...

KUTOKUJUA KAMA NI MSAFI AU KUTOKUWA MSAFI NDIO NIFUNGE MLANGO WA KUKEMEA MUNKARI. ..

UISLAAM HAUPO HIVYO.. .

LENGO LA HUU UZI NI KUWEKA BAYANA UBAATWIL WA GHARAMA ZINAZOTOZWA NA BAKWATA KWA WANAWAKE DHAIFU. .. NA KUUWEKA WAZI USITOE HIZO GHARAMA HAZIHUSIANI...
Tukumbushane labda!

Kipimo cha mwenye elimu kwa Shaytwaan yeye yupo juu, ni bora! Anajua yeye ni bora! Kipimo cha Mtume rehma na amani ziwe juu yake ni kuwa alikuwa ni mwenye elimu na ni mnyenyekevu.
 
Kwa mtazamo huu, hakuna kitakachoandikwa JF... Maana kila kiandikwacho kina pahala pa kupeleka.. JF SI PA MAMBO YASIYO NA KWA KWENDA PEKEE.... Wakati mwingine huko kunakotakiwa kupelekewa mambo fulani kuna tatizo linaoloathiri unachokipeleka
Kumbe unakubaliana namimi kuwa kuna pahala sahihi pa kupeleka malalamiko, sawa.

Halafu kusema kwa mtazamo wangu, hakuna kitakachoandikwa JF sio kweli, kwa sababu mimi sikujumuisha kila malalamiko yanayoletwa humu na mbona kuna mashirika yameanzisha thread za kupokea malalamiko na sikwenda kupinga.

Lakini kupinga kwangu kwa kukosolewa BAKWATA kwa staili hii, ni kwa sababu kuikosoa BAKWATA sio kama kuikosoa club ya simba au ya yanga.

BAKWATA ni baraza la dini, hata kama wanamahovyohovyo lakini wanaheshima yao, au labda kama ulioni hilo.

Na kama ulioni hilo basi usinilazishe niwe na mtazamo kama wako.
 
Uhakika kwamba fulani yupo humu tunao kwa VERIFIED MEMBERS PEKEE.. eg Zitto etc.. sisi wengine hatujui kama na JPM yumo personally au la..!! hivyo bado naitazama kuwa ni sahihi kuandika humu...

UNAKUMBUKA WAKATI WA KIPINDI CHA PILI CHA JK, PIUS MSEKWA ALIITAJA JF KAMA SABABU YA KUPUNGUA KWA KURA ZA JK KWA KIPINDI CHA PILI...?? Kwani Pius Msekwa hadi atamke vile, alikuwe/yumo humu?
Sawa, huu ni mtazamo wako.

Tuseme wahusika wapo humu na ujumbe umewafikia, halafu soma komenti za wale wasio wahusika uone wameupokeaje uzi na wameizungumziaje BAKWATA.

Ndio utajua faida ya kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Huwenda ukanielewa ninachokimaanisha.
 
Muungwana akivuliwa nguo huchutama.

Kwani kuna ugumu gani mtu kukiri amekosea??
Nani alikwambia makosa au usahihi unapimwa kwa wengi wape?

Kisicho sahihi kitaendelea kutokuwa sahihi hata kama dunia nzima watasema ni sahihi, na kinyume chake.
 
Kwahiyo ndugu ndio tuache kukemea kwa njia ambazo tunajua ujumbe utafika haswa kwa sababu hizo???
Sikuandika kuwa wasikemewe niliandika ni wa kuonewa huruma. Mleta Uzi akajibu hiki:

"Wenyewe waonewe huruma wakati ambao wao hawajamuonea huruma mwanamke...

Na hiyo ndio hekima yake.. ."
__-----------
Nilichomjibu ndicho wewe ulichonikoti. Pengine lugha niliyoitumia ni ngumu ama pengine uwasilishaji wangu haukuwa mzuri, naomba radhi kwa hilo.
 
Ni wapi kwenye Uislam umeambiwa mtu akifanya maasi uwe mkali juu yake? Ni nini maana ya kauli ya nakusihi pamoja na kuisihi nafsi yangu?

Ipi hekima ya maneno haya aliyoyasema Mtume "Msaidieni mwenye kudhulumu na mwenye kudhulumiwa" Mtume ndiye anayeujua zaidi, inakuwaje Mtume hakusema mwenye kudhulumu amefanya maasi juu ya Allah achukiwe na akasirikiwe?

“Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa
hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.”(Sura An-Nahl; 16:125).

Allah mwenyewe anawaambia waja wake wenye madhambi na madhambi wasikate tamaa kwenye rehma yake. Tena hakuwatenga kwa kuwagawanya kwamba wanafanya wema na hawa wanafanya maovu ni wenye dhambi! La! Allah alituita kwa kauli moja wote kwa kutuita "Yaa ibadii" enyi waja zangu...kisha akatuambia tusikate tamaa kwenye rehma zake. Hata uwe na makontena ya madhambi katuambie msikate tamaa kwenye rehma zangu. Huyu ndiye aliyetuumba sisi inakuwaje wewe ni mwenye hasira zaidi kwa wanaofanya maasi juu yake kuliko yeye?

Na Allah huwa ananadi usiku "ni nani mwenye madhambi nimsamehe! Ni nani mwenye shida nimtimilizie..." Bahari huwa inamuomba Mungu iwazamishe ndani yake wale wote wanaopita juu yake wale wote wanaomuasi Mungu na waliyomajeuri kwa Mungu. Mbingu humuomba Mungu kila siku iibamize sehemu ya ardhi ya hii dunia ya wale ambao wanao muasi Mungu. Na ardhi inamuomba ruhusa Mungu iwameze wote wenye madhambi kwa Mungu. Allah anawajibu wote kwa kuwaambia "Hamjawaumba ninyi! Laiti ninyi mngeliwaumba msingelisema hayo" Kisha muangalie Mtume aliishi vipi na wale waliyomkosea yeye na ukimkosea Mtume umemkosea Mungu, Mtume aliishi nao vipi! Hata kwa wale waliyomkosea Mungu Mtume alikuwa anaamiliana nao vipi!?

Na hii ndiyo iliyokuwa kazi ya Mitume na kazi ya waliyorithi Mitume. Kingine sina chuki na yeyote.
Unanijazia threads kwa comments zako... Tunaacha kudiscuss mada ya msingi.. .
 
Back
Top Bottom