Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Mcheni Allah enyi watu!Mkuu umejinasibisha kwamba huna mihemko wala huendeshwi kwa mihemko ila hoja yako haishabihiani na Hilo.
Inaonekana kulalamikia ada ya kupokelewa shauri. Umewahi kujiuliza BAKWATA KATA wanaendesha ofisi kwa fungu lipi? Je kuna hesabu gani nyuma ya hiyo ada (deligation, mwendo wa kutoka ofisi za kata nk.,).
Kadhi anaendesha ofisi kwa mfuko upi? Analipwa mshahara na nani? Deligation inayoamua kesi hiyo Ina watu wangapi? Nk.
Hatuhalalishi wala kutete tozo, bali kila jambo huamuliwa kulingana na wakati na nyakati husika na kwa vigezo vile vile.
Mwanamke;
Anatoa wapi shilingi elfu 15,000 au 30,000? Nikidhani unazungumzia kwamba ananyanyaswa kingono katika HARAKATI za kuipata haki yake au anazungushwa kwa uamuzi usiosahihi na nk.
Hivi huyu mwanamke ambaye unadhani anahitaji talaka 45,000 inaweza kuwa kikwazo cha kutimiza ombi lake?
Unajua shauri likifika kule gharama ambazo mwanamke anatakiwa aziingie kisheria kuipata hiyo talaka (anatakiwa kurudisha mahari), je Kama aliolewa kwa 200,000/- unadhani atakuwa na uwezo wa kutafuta 200,000/ alafu akose 45,000/?
Usikubali kuwa mjinga kwa hiari.
Kwahiyo pasipokuwa na kesi hata moja hapo bakwata kata hiyo ofisi haitoendeshwa???
Kwahiyo mmekaa mnaombea watu wapate madhila ili watoto wenu waende vyooni?
Hivi ndivyo mtume alivyoendesha shughuli za uislam??? Kama mmeshindwa kuitengeneza bayt al maal mna faida gani sasa kwa waislam??
Hivi mnadhani matajiri wa kiislam wangeshindwa kutoa zaka zao kwa ajili ya kuendesha harakati za uislam kupitia bakwata ikawa ndio chanzo katika hiyo bayt al maal?? Kwanini matajiri hao hawatoi chochote kwa bakwata??
Semeni na mitumbo yenu hiyo kwani hakika adhabu za Allah ni kali