Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,976
- 22,418
Mcheni Allah enyi watu!Mkuu umejinasibisha kwamba huna mihemko wala huendeshwi kwa mihemko ila hoja yako haishabihiani na Hilo.
Inaonekana kulalamikia ada ya kupokelewa shauri. Umewahi kujiuliza BAKWATA KATA wanaendesha ofisi kwa fungu lipi? Je kuna hesabu gani nyuma ya hiyo ada (deligation, mwendo wa kutoka ofisi za kata nk.,).
Kadhi anaendesha ofisi kwa mfuko upi? Analipwa mshahara na nani? Deligation inayoamua kesi hiyo Ina watu wangapi? Nk.
Hatuhalalishi wala kutete tozo, bali kila jambo huamuliwa kulingana na wakati na nyakati husika na kwa vigezo vile vile.
Mwanamke;
Anatoa wapi shilingi elfu 15,000 au 30,000? Nikidhani unazungumzia kwamba ananyanyaswa kingono katika HARAKATI za kuipata haki yake au anazungushwa kwa uamuzi usiosahihi na nk.
Hivi huyu mwanamke ambaye unadhani anahitaji talaka 45,000 inaweza kuwa kikwazo cha kutimiza ombi lake?
Unajua shauri likifika kule gharama ambazo mwanamke anatakiwa aziingie kisheria kuipata hiyo talaka (anatakiwa kurudisha mahari), je Kama aliolewa kwa 200,000/- unadhani atakuwa na uwezo wa kutafuta 200,000/ alafu akose 45,000/?
Usikubali kuwa mjinga kwa hiari.
Muungwana akivuliwa nguo huchutama.Nikuulize wewe ulianzisha hii mada ili kuwaponda BAKWATA au kuwatetea wanawake?
Maana umesema maneno ya haqi ukikusidia batili.
BAARAKALLAH FIYK. .. Kuna watu hapa baba zao wako bakwata roho zawauma...Mcheni Allah enyi watu!
Kwahiyo pasipokuwa na kesi hata moja hapo bakwata kata hiyo ofisi haitoendeshwa???
Kwahiyo mmekaa mnaombea watu wapate madhila ili watoto wenu waende vyooni?
Hivi ndivyo mtume alivyoendesha shughuli za uislam??? Kama mmeshindwa kuitengeneza bayt al maal mna faida gani sasa kwa waislam??
Hivi mnadhani matajiri wa kiislam wangeshindwa kutoa zaka zao kwa ajili ya kuendesha harakati za uislam kupitia bakwata ikawa ndio chanzo katika hiyo bayt al maal?? Kwanini matajiri hao hawatoi chochote kwa bakwata??
Semeni na mitumbo yenu hiyo kwani hakika adhabu za Allah ni kali
Kwahiyo ndugu ndio tuache kukemea kwa njia ambazo tunajua ujumbe utafika haswa kwa sababu hizo???DsmicSound itimilize haki ya Allah kwa kuwaelekeza watu waelekee kwake. Uovu hauondoshwi kwa uovu. Itangulize mbele huruma kutoka ndani ya moyo wako. Mtume rehma na amani ziwe juu yake alimkubalia Wahshi kuingia kwenye Uislam ijapokuwa Wahshi alimuulia Mtume uncle wake Hamza r.a ijapokuwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake alionelea ngumu kumtizama usoni pindi anasilimu. Hii nayo ni sunnah ya Mtume, tuifuate.
Ikiwa Allah anatuambia waja wake waliyokuwa na israfu ya madhambi wasikate tamaa kwenye rehma yake ni huruma ya namna gani hiyo? Tuwe na huruma na waliyopo chini, tutaonewa huruma na aliyepo juu.
Labda iwe ilipita kwa maelezo ya mdomo au maelekezo ya kiutawala ila siyo kwenye SheriaOoh nlikua sijui hii kitu.
Mara ya mwisho nilifatilia kama vile bunge lilipiga chini hii issue.
Mbona unakuwa na akili ndogo Maaskofu wanaingiaje hapa
Kuna sehemu huu uzi umetaja askofu?dogo acha kula kitimoto ni hatari kwa afya ya akili
Bakwata wanafeli sana.kusuluhisha magomvi ya wanandoa mpaka uwe na pesa?
Mtume amesema "zichengueni haki za madhaifu wawili hawa, nao ni wanawake
Ni wapi kwenye Uislam umeambiwa mtu akifanya maasi uwe mkali juu yake? Ni nini maana ya kauli ya nakusihi pamoja na kuisihi nafsi yangu?Mpuuzi wewe umekuja hapa kwa lengo la kujifanya una upole.. Kwenye Maasi juu ya Allah...
Mi sunni.Ndio mimi nipo njia salama kwa sababu kigezo changu ni Mtume na maswahaba zake.. . Wewe kabaki na quraniyyuun mwenzako faizafoxy na mashia wenzako. .. Achana na hii post kama inakuuma au kama baba yako yupo bakwata mpe ujumbe huu mwambie aache dhulma.. .
Tukumbushane labda!Unanisihi nini wakati ulikuwa unapinga. .. Baada ya kukwambia shahidi ni Allah na nikakwambia nikuletee docs za bank. .. Sasa unanisihi... Basi HUKUWA NA LENGO LA KUJUA UKWELI ILA ILIKUWA NI KUPINGA TU KWA MASLAHI YAKO...
KUTOKUJUA KAMA NI MSAFI AU KUTOKUWA MSAFI NDIO NIFUNGE MLANGO WA KUKEMEA MUNKARI. ..
UISLAAM HAUPO HIVYO.. .
LENGO LA HUU UZI NI KUWEKA BAYANA UBAATWIL WA GHARAMA ZINAZOTOZWA NA BAKWATA KWA WANAWAKE DHAIFU. .. NA KUUWEKA WAZI USITOE HIZO GHARAMA HAZIHUSIANI...
Kumbe unakubaliana namimi kuwa kuna pahala sahihi pa kupeleka malalamiko, sawa.Kwa mtazamo huu, hakuna kitakachoandikwa JF... Maana kila kiandikwacho kina pahala pa kupeleka.. JF SI PA MAMBO YASIYO NA KWA KWENDA PEKEE.... Wakati mwingine huko kunakotakiwa kupelekewa mambo fulani kuna tatizo linaoloathiri unachokipeleka
Sawa, huu ni mtazamo wako.Uhakika kwamba fulani yupo humu tunao kwa VERIFIED MEMBERS PEKEE.. eg Zitto etc.. sisi wengine hatujui kama na JPM yumo personally au la..!! hivyo bado naitazama kuwa ni sahihi kuandika humu...
UNAKUMBUKA WAKATI WA KIPINDI CHA PILI CHA JK, PIUS MSEKWA ALIITAJA JF KAMA SABABU YA KUPUNGUA KWA KURA ZA JK KWA KIPINDI CHA PILI...?? Kwani Pius Msekwa hadi atamke vile, alikuwe/yumo humu?
Nani alikwambia makosa au usahihi unapimwa kwa wengi wape?Muungwana akivuliwa nguo huchutama.
Kwani kuna ugumu gani mtu kukiri amekosea??
Sikuandika kuwa wasikemewe niliandika ni wa kuonewa huruma. Mleta Uzi akajibu hiki:Kwahiyo ndugu ndio tuache kukemea kwa njia ambazo tunajua ujumbe utafika haswa kwa sababu hizo???
Unawatetea maaskofu wala sadaka au maaskofu Gan au na wewe kipofu huonNashukuru Mungu maaskofu wetu wanajitambua na hawatumiki
Unanijazia threads kwa comments zako... Tunaacha kudiscuss mada ya msingi.. .Ni wapi kwenye Uislam umeambiwa mtu akifanya maasi uwe mkali juu yake? Ni nini maana ya kauli ya nakusihi pamoja na kuisihi nafsi yangu?
Ipi hekima ya maneno haya aliyoyasema Mtume "Msaidieni mwenye kudhulumu na mwenye kudhulumiwa" Mtume ndiye anayeujua zaidi, inakuwaje Mtume hakusema mwenye kudhulumu amefanya maasi juu ya Allah achukiwe na akasirikiwe?
“Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa
hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.”(Sura An-Nahl; 16:125).
Allah mwenyewe anawaambia waja wake wenye madhambi na madhambi wasikate tamaa kwenye rehma yake. Tena hakuwatenga kwa kuwagawanya kwamba wanafanya wema na hawa wanafanya maovu ni wenye dhambi! La! Allah alituita kwa kauli moja wote kwa kutuita "Yaa ibadii" enyi waja zangu...kisha akatuambia tusikate tamaa kwenye rehma zake. Hata uwe na makontena ya madhambi katuambie msikate tamaa kwenye rehma zangu. Huyu ndiye aliyetuumba sisi inakuwaje wewe ni mwenye hasira zaidi kwa wanaofanya maasi juu yake kuliko yeye?
Na Allah huwa ananadi usiku "ni nani mwenye madhambi nimsamehe! Ni nani mwenye shida nimtimilizie..." Bahari huwa inamuomba Mungu iwazamishe ndani yake wale wote wanaopita juu yake wale wote wanaomuasi Mungu na waliyomajeuri kwa Mungu. Mbingu humuomba Mungu kila siku iibamize sehemu ya ardhi ya hii dunia ya wale ambao wanao muasi Mungu. Na ardhi inamuomba ruhusa Mungu iwameze wote wenye madhambi kwa Mungu. Allah anawajibu wote kwa kuwaambia "Hamjawaumba ninyi! Laiti ninyi mngeliwaumba msingelisema hayo" Kisha muangalie Mtume aliishi vipi na wale waliyomkosea yeye na ukimkosea Mtume umemkosea Mungu, Mtume aliishi nao vipi! Hata kwa wale waliyomkosea Mungu Mtume alikuwa anaamiliana nao vipi!?
Na hii ndiyo iliyokuwa kazi ya Mitume na kazi ya waliyorithi Mitume. Kingine sina chuki na yeyote.