Cathy Diwani
Senior Member
- Feb 13, 2016
- 120
- 185
Salaam wakuu,
Mdogo wangu ndoa yake imevunjwa na baraza kuu la Waislamu(Bakwata) kupitia kwa kadhi wa baraza hilo mkoa fulani huku Bara.
Baada ya kuvunja ndoa hiyo baraza hilo linataka mdogo wangu na mtalaka wake watafute watathmini wakakague mali walizochuma kwenye ndoa ili baraza hilo ligawe hizo mali. Wakati huo mwanaume amezuia documents zote zinazohusiana na hizo mali, na analiambia baraza hilo kuwa hizo mali amepewa na baba yake, wakati ni nyumba na viwanja na mashamba ambayo wamefanya biashara wakajenga na kununua akiwa na mke wake.
Na wamehukumu pia watoto wabaki kwa baba kwani watoto ni wakubwa na mke hana uwezo kiuchumi wa kuwalea. Wametoa hiyo hukumu huku hawajawahi kujadili chochote kuhusu watoto baada kuvunja ndoa hiyo.
Mdogo wangu ameomba apewe barua aende mahakamani ili mahakama ikasimamie mgao wa hizo mali pamoja na malezi ya watoto, baraza hilo linamzungusha, kuwa kama hataki baraza ligawe hizo mali atahukumiwa kuwa amekataa maamuzi ya mahakama ya kadhi na hivyo si mwislamu tena.
Anaomba asaidiwe, je wanachofanya Bakwata kutaka kugawa mali za wanandoa hao na kuhukumu kuhusu malezi ya watoto ni sawa?
Kama ni sawa, akikataa baraza hilo kugawa hizo mali aende mahakamani afuate utaratibu gani? Ana hati ya kuvunjwa ndoa kutoka Bakwata, lakini hawataki kumpa fomu namba tatu aende mahakamani.
Afanye nini mpaka hapa?
Natanguliza shukrani.