SHIDA YA HAO BAKWATA NAO ELIMU YA DINI NI CHACHE...
SASA NINAKUPA MAJIBU AMBAYO NI KWA MUUJIBU WA SHARIYA YA KIISLAAM... WEWE NA DADA YAKO MTAANGALIA MTAFUATA AU LA.
1. Hongera ndoa imevunjwa na Qadhi(kwa sababu huenda Mume alikuwa mbishi kutoa talaka na mapenzi yaliisha au mateso yalikithiri).
2. Pole ndoa imevunjwa na Qadhi( kwa sababu ndoa iliyovunjwa na Qadhi huwa hamna kurudiana milele, bora Mume utoe talaka tu una mlango wa kurudiana hata kwa kuoana tena). HAYA UNABIDI UYAJUE BINAFSI... USISUBIRI MPAKA QADHI AKUSIMAMIE HILI.
3. Kuhusu watoto, SHERIA inaelekeza pale ambapo wanandoa wametengana... Malezi ya watoto yatazingatia maslahi ya mtoto kutoka kwa mzazi husika... Sio lazima wabaki kwa baba au mama tu... Ila katika uislaam WATOTO NI WA BABA... Ndio maana kwa mke aliyeachwa anaweza akadai MALIPO YA KUNYONYESHA MTOTO WAKE... Japo wengi wanafanyaga kwa mapenzi na huruma kwa watoto wao tu.
Kama mtoto bado ananyonya na maadili yapo vizuri basi atakaa na mtoto mpaka akimaliza atamrejeshea baba yake, nalo vilevile litazingatia maadili ya baba, anaweza asipewe vile vile baba au mama kama maadili ni mabovu.
4. Kuhusu mali, katika sheria ya kiislaam tunatambua mali halali aina tatu za wanandoa;-
- Mali ya Mume(itabaki kuwa ni ya mume ndani ya ndoa mpaka nje ya ndoa haibadiliki.)
- Mali ya Mke( itabaki kuwa ni ya mke kwenye ndoa na baada ya ndoa)
- Mali ya Mke na Mume-wote ( hii ni partnership, kwamba kila mmoja amewekeza mchango wake moja kwa moja iwe ni MTAJI WA MALI, NGUVU AU JITIHADA - NA HII HUGAWANYWA KULINGANA NA KIASI CHA MCHANGO ALIOUTOA KWENYE UTAFUTAJI WA MALI HIO.)
[emoji324]Uislaam hautambui mali zifuatazo;-
- Mali inayotajwa kuwa "AMEIPATA NIKIWA NAE KWENYE NDOA" (Wewe sema unataka kumdhulumu mwenzio) MDHULUMU TU.
- Mali inayotajwa kuwa imepatikana "BAADA YA MUME KUMRUHUSU MKE AFANYE KAZI" - HII NI DHULMA.
*ZOTE ZINAZOENDA KINYUME NA ZILE AINA TATU NILIZOTAJA KUWA UISLAAM UNAZITAMBUA... HIZO NI DHULMA.
MWISHO ZINGATIA;-
NI KWELI KUWA KATIKA UISLAAM... UKAHUKUMIWA KWA SHERIA SAHIHI ZA KIISLAAM ALAFU WEWE UKAONA SHERIA YA KIISLAAM HAIJAKUTENDEA HAKI... UKAENDA KUTAFUTA HAKI NJE YA UISLAAM... BASI UMETOKA KWENYE UISLAAM AUTOMATICALLY (Utasilimishwa upya).
Hilo haliwi pale ambapo Qadhi amekuhukumia suala lako kimakosa tofauti na sheria sahihi inavyotaka... Unaweza kutafuta wataalam wengine wa sheria ya kiislaam au Qadhi wa juu yake aipitie upya sheria na suala lako...
KWAHIYO DADA YAKO ATAPIMA KUPITIA MAELEZO HAYA... KAMA NI MCHAMUNGU ATACHAGUA KUNYOA AU KUSUKA INSHAA ALLAAH...
Ukitaka ufafanuzi zaidi njoo inbox nikupe namba nikuelekeze cha kufanya taratibu Inshaa Allaah.
ALLAAH ATUONGOZE.