BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe.

Akitoa maoni hayo Mwanasheria Mkuu wa BAKWATA, Hassan Fatihu alipowasilisha mapendekezo kwa Tume ya Kuangalia Jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini amesema sheria ya ndoa ibaki vilevile kutokana na ukinzani uliopo kati ya sheria ndoa na sheria ya mtoto pamoja na imani za dini.

“Sisi Waislamu tunaamini mtoto wa kike akishavunja ungo anaruhusiwa kuolewa, nami naruhusiwa kuoa haijalishi nina miaka 10, 12 au 13,” ameeleza Fatihu.

Ameongeza kuwa sheria ya mtoto inaeleza kuwa mtu yeyote aliye chini ya miaka 18 ni mtoto, na kwamba sheria ya ndoa imeruhusu mtoto kuanzia umri wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya mahakama ambapo itaangalia vitu vingi ili kuruhusu ndoa hiyo ikiwa ni pamoja na afya ya mtoto, mila na tamaduni za jamii husika.

Mjumbe asiuawe

=======

BAKWATA imependekeza kutoifanyia marekebisho Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15 au miaka 14 kwa kibali cha wazazi.

Mtazamo huo unakinzana na maoni ya wanaharakati wa haki za watoto na wanawake ambao wamekuwa wakipinga utekelezaji wa sheria hiyo kuwa inakinzana na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inayomtambua mtoto hadi umri wa 18.

Julai 8, 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ikikubali kwamba vifungu hivi vya sheria ya ndoa vinapingana na Katiba kwa kuweka umri tofauti wa kuoa/kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume.

Hukumu hiyo ilitolewa kufuatia kesi iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa Shirika la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi aliyekuwa akipinga kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Kwa mujibu wa BAKWATA, mtoto mwenye umri wa miaka 11, 12 au 13 aliyeingia kwenye kipindi cha balehe aruhusiwe kuolewa kwa uhalali wa mahakama utakaozingatia vielelezo vya kimazingira. “Mtoto wa kike ana miaka 11, 12 hajaendelea na elimu, kwa nini asiolewe? Ukimuacha huyu ni matokeo ya kupata mimba mtaani.

“Simaanishi kila mtoto wa umri huo aruhusiwe kuolewa ila mahakama itajiridhisha afya yake, mazingira na mengineyo,” alisema mwanasheria wa baraza hilo, Hassan Fatiu.

Chanzo: Mwananchi
 
Sikubalian nao kabisa binti wa 14 ni ubakaji wa watoto tena wafungwe maisha.

Watoto wahimizwe kusoma ili kuondoa ujinga kichwan na sio kuwaza waolewe tu ndoa zenyewe ngumu na mateso mtoto atawezaje kuhimili visa vya mama mkwe na wifi kama mimba tatizo tutawekea njiti
 
Ndio uislam ulivyo na sheria zake. Mume wake 4, mke mume 1 justificaion iko wapi?
Anyway Mkuu nisingependa nicomment kuhusia na imani za watu ila ni suala la akili ya kawaida hivi mtoto wa miaka 14 kweli yupo tayari kwa changamoto ya kusimama kama mama au mke?...naamini hakuna mzazi mwenye akili yake timamu yupo tayari kumuoza binti yake wa miaka 14..NEVER...
 
Back
Top Bottom