BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

Hili ndo tatizo la waafrika kuukataa ukweli hata kama wanaushudia.

Ukweli ni kwamba hao mabinti wenye huo umri mnao waita watoto huku mtaani wanafanya ngono sana tena na watu wazima kama baba zao.
Mitaa imejaa rundo la mabinti wa miaka 13 ,14 mpaka 15 walio pewa mimba na kuzalishwa alafu wakatelekezwa sasa si bora waolewe kuliko kuwa wanafanyiwa hivyo?

Mabinti wa siku hizi wame jaa uhuni mwingi mno sasa hivi kukuta binti wa hiyo miaka 14 ambao ww unamuita mtoto ana mmiliki wanaume 3 na wote anaeahudumia kingono ni jambo la kawaida.
SIKU UKIZAA NDIO UTAELEWA.

ENDELEA KUKUA KUA KWANZA, WE BADO MTOTO.
 
Ndugu Hassan Fatiu ana kabinti kweli ka umri huo nataka niendenkukaposa ili bintie awe wa mfano..
Nenda kwake, kama hana yeye atakupatia kwa wengine.

Yanini kuandikia mate na wino upo?
 
SIKU UKIZAA NDIO UTAELEWA.

ENDELEA KUKUA KUA KWANZA, WE BADO MTOTO.
Mkuu kuzaa kwako na kutozaa kwangu hakutabadilisha ukweli.
Kwahiyo unakataa kuwa mitaani hakuna rundo la mabinti wa umri wa 14 mpaka 15 walio zalishwa na kutelekezwa?

Unakataa kuwa mabinti wa umri 14hawafanyi ngono na watu wazima kama baba zao?
Ww kama una binti yako mwenye umri huo na bado unamuita mtoto bila shaka hata yeye atakuwa anakucheka kimoyo moyo ila anayo yafanya mitaani anayajua mwenyewe.

Ww utakataa ila ukweli na uhalisia ndo huo binti kama hasomi na ana umri huo huna haja ya kumkataza kuolewa maana kinacho kufanya umkataze kuolewa anakifanya mitaani na katika mazingira hatarishi.
 
Sikubalian nao kabisa binti wa 14 ni ubakaji wa watoto tena wafungwe maisha.

Watoto wahimizwe kusoma ili kuondoa ujinga kichwan na sio kuwaza waolewe tu ndoa zenyewe
Kwani alie olewa awezi kusoma?uwezi pingana na maumbile alie muumba kamfanya aingie kwenye siku zake akiwa na miaka 14 wewe unasema mtoto wewe na Mungu nani zaidi au mtoto wakike kuona siku zake kila mwezi maanake nn?
 
Nikweli anakuwa mkubwa sana......kama huyu 11 tayari
Screenshot_20230324-182838.png
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limependekeza kifungu cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu msichana wa umri wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama kisiondolewe.

Akitoa maoni hayo Mwanasheria Mkuu wa BAKWATA, Hassan Fatihu alipowasilisha mapendekezo kwa Tume ya Kuangalia Jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini amesema sheria ya ndoa ibaki vilevile kutokana na ukinzani uliopo kati ya sheria ndoa na sheria ya mtoto pamoja na imani za dini.

“Sisi Waislamu tunaamini mtoto wa kike akishavunja ungo anaruhusiwa kuolewa, nami naruhusiwa kuoa haijalishi nina miaka 10, 12 au 13,” ameeleza Fatihu.

Ameongeza kuwa sheria ya mtoto inaeleza kuwa mtu yeyote aliye chini ya miaka 18 ni mtoto, na kwamba sheria ya ndoa imeruhusu mtoto kuanzia umri wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya mahakama ambapo itaangalia vitu vingi ili kuruhusu ndoa hiyo ikiwa ni pamoja na afya ya mtoto, mila na tamaduni za jamii husika.

Mjumbe asiuawe

=======

BAKWATA imependekeza kutoifanyia marekebisho Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15 au miaka 14 kwa kibali cha wazazi.

Mtazamo huo unakinzana na maoni ya wanaharakati wa haki za watoto na wanawake ambao wamekuwa wakipinga utekelezaji wa sheria hiyo kuwa inakinzana na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inayomtambua mtoto hadi umri wa 18.

Julai 8, 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ikikubali kwamba vifungu hivi vya sheria ya ndoa vinapingana na Katiba kwa kuweka umri tofauti wa kuoa/kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume.

Hukumu hiyo ilitolewa kufuatia kesi iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa Shirika la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi aliyekuwa akipinga kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Kwa mujibu wa BAKWATA, mtoto mwenye umri wa miaka 11, 12 au 13 aliyeingia kwenye kipindi cha balehe aruhusiwe kuolewa kwa uhalali wa mahakama utakaozingatia vielelezo vya kimazingira. “Mtoto wa kike ana miaka 11, 12 hajaendelea na elimu, kwa nini asiolewe? Ukimuacha huyu ni matokeo ya kupata mimba mtaani.

“Simaanishi kila mtoto wa umri huo aruhusiwe kuolewa ila mahakama itajiridhisha afya yake, mazingira na mengineyo,” alisema mwanasheria wa baraza hilo, Hassan Fatiu.

Chanzo: Mwananchi


Inashangaza kuona huyu mwanasheria anajikita katika makatazo. Kwanza, ytumuulize kama yeye ataridhia mtoto wake aolewe akiwa na miaka 14. Nina hakika sheria ya ubakaji haina kinga kidini. Na pia hata ruhusa ya mzazi haina kinga katika ubakaji. Yeye mmwana sheria atateteaje ubakaji? Ina maana mzazi sasa anaweza kutoa ruhusa kwa binti yake aliyemaliza darasa la saba akaolewa na muoaji akajitetea dini haikatazi/inaruhusu. Hili itabidi lipingwe na watu wa imani zote. Dunia itatucheka kuona tunatetea ujinga kama huu kwa mwavuli wa dini.
 
Watafungwaje wakati Serikali na dini zimekubali?

Mtaani kwangu kuna darasa la 6 mapepe vibaya mno
Tatizo baadhi ya watu ujitoa akili heti mtoto miaka 14 anae ingia kwenye siku zake heti mtoto[emoji12][emoji2957]
 
Ila binti huyo analiwa na bodaboda
Kuliwa na bodaboda hakuwezi kuhalalisha kubadilisha sheria. Ina maana wizi ukizidi dawa yake ni kuhalalishi wizi. Mbona wanawake wa kuoa wengi tu, kwa tuenda kwa vitoto vidgo vinavyonuka mkojo?
 
Kwahiyo, mapepe mmoja afanye kundi zima lipotee..!!??? Vipi kama mtaani kwenu kuna mashoga..!!???
Ludia kusoma sheria ya ndoa mbona haija futika hapo juu au ulikuwa usingizini ukakometi bila kusoma?
 
Yaani mtu amesoma sheria mpaka kuwa mwanasheria mkuu wa Bakwata haoni aibu kuongea Upumbavu kama huu...?...anajua mtoto wa miaka 14 alivyo? Kweli ataweza kubeba majukumu ya kuwa mke achilia mbali kuwa mama? Na shule je?.

Aisee...inasikitisha sana.
Wewe unachuki na huyo mwanasheria sio bule yeye kanukuu kifungu cha sheria ya ndoa hiyo sheria akutunga yeye chuki ni ugonjwa mbaya zaidi ya ukimwi
 
Nafikiri mengine ni conventional. by the law of nature mtu akibarehe anaweza kuelewa kwa mwili upo tayari. Oooh bado ni mtoto....mtoto ni nini? Kwani mtu anakuwa mtu mzima miraculously akifika 18? Mazingira yachangia namna gani mtu anaweza kustahimili majukumu hususani malezi. Zamani waliolewa wadogo na waliweza. Kwa sasa Hata 30 hajui kupika...lazima awe na dada wa kazi etc. So ukomavu ni mazingira kuliko age
 
Inashangaza kuona huyu mwanasheria anajikita katika makatazo. Kwanza, ytumuulize kama yeye ataridhia mtoto wake aolewe akiwa na miaka 14. Nina hakika sheria ya ubakaji haina kinga kidini. Na pia hata ruhusa ya mzazi haina kinga katika ubakaji. Yeye mmwana sheria atateteaje ubakaji? Ina maana mzazi sasa anaweza kutoa ruhusa kwa binti yake aliyemaliza darasa la saba akaolewa na muoaji akajitetea dini haikatazi/inaruhusu. Hili itabidi lipingwe na watu wa imani zote. Dunia itatucheka kuona tunatetea ujinga kama huu kwa mwavuli wa dini.
Lakini hiyo sheria ni kwamujibu wa sheria ya Tz na sio dini hivyo acha kukurupuka.
 
Anyway Mkuu nisingependa nicomment kuhusia na imani za watu ila ni suala la akili ya kawaida hivi mtoto wa miaka 14 kweli yupo tayari kwa changamoto ya kusimama kama mama au mke?...naamini hakuna mzazi mwenye akili yake timamu yupo tayari kumuoza binti yake wa miaka 14..NEVER...
Bibi yako aliolewe akiwa na umri gani?taja sababu ya mtoto wakike kuanza kuingia kwenye siku zake kila mwezi
 
Back
Top Bottom