figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Baraza kuu la Waislam Tanzania, limetaka mfanyabiashara wa Casino Gaming kufunga mara moja kwani wanaleta Uaumbufu kwa makazi ya Viongozi. Casino ipo Palm Village Mikocheni.
Tatizo ni kwamba Casino ipo eneo lenye Wananchi wengi na hasa Viongozi Wastaafu kuanzia Familia ya BABA WA TAIFA NA RAIS WA AWAMU YA PILI
....kuwawekea Biashara ya Kamali kwenye Milango ya makazi yao ni ukosefu wa Nidhamu na Maadili. BAKWATA iliwafahamisha mapema kabla ya kujengwa na kufunguliwa kwa Biashara hiyo ya Kamali maana pia eneo hilo linakaliwa pia na Viongozi wengi wa Dini Wastaafu.
Inashangaza kwamba Mkurugenzi muhusika wa utoaji wa Vibali vya Kamali akaamua kuziba Masikio na kuruhusu Biashara hiyo inayokera sana kutokana na Wingi wa Watu kuingia na kutoka ndani ya jengo hilo Usiku kucha na kuwasumbua majirani na hasa Viongozi Wastaafu.
Ni muhimu sana Serikali ikaingilia sasa suala hili na kulitafutia ufumbuzi maana Biashara ya Kamali haifai kuwa kwenye maeneo ya makazi ya Wananchi.