Balaa la kuazimisha gari!!!

Kweli mkuu heri nitembee kwa miguu/daladala kuliko kuazima gari la mtu
Bora upate ajali na gari lako utapaki kivulini mpk upate mkwanja wa matengenezo
Sasa ukute gari umeazima likaumia mby na mfukoni huna mapene
 
Mkuu unakuta gari umejichanga kwa shida alafu mtu anakuletea tena mateso ya nafsi na gari yako
 
Kweli mkuu heri nitembee kwa miguu/daladala kuliko kuazima gari la mtu
Bora upate ajali na gari lako utapaki kivulini mpk upate mkwanja wa matengenezo
Sasa ukute gari umeazima likaumia mby na mfukoni huna mapene
Kuna jamaa wanajiamin kweli,pamoja na kuwepo kwa ajari nyingi sahv huko barabarani lakin unakuta mtu anaazima gari la million zaidi ya 60 anaenda nalo mikoani huko
 
Mimi sitaki hata kukumbuka,
Kilichoniuma si mwamba kulipga mzinga ila ni kulipiga mzinga halafu akakana kuwa si yeye aliyelipga mzinga yani ikanifanya nionekane najaribu kumpiga. Nilijua pesa ya kulipa hana lakini akakana yani yule jamaa na ulokole wake sikuamini masikio yangu
 
Pole mkuu,kumpa mtu gari ni changamoto, Mara nyingi lazma litarudi na kasoro tu sivyo kama alivyochukua
 
Pole mkuu,kumpa mtu gari ni changamoto, Mara nyingi lazma litarudi na kasoro tu sivyo kama alivyochukua
Kabisa yan jamaa alilipga mzinga halafu likamwagka vioo vyote vya kushoto na taa ya mbele na nyuma upande wa kushoto, likachanika huo upande hadi linaonekana ndani. Halafu akaenda akalipaki baada ya siku 3 akanikana yule jamaa
 
Kanuni ya kwanza, usimuazime mtu gari ambaye hana gari. Yani hata kama atakuwa na Premio akakuomba umuazime Harrier yako we mpe kiroho safi. Kuna wale wauza sura mtu hana hata pikipiki ila anataka akaoshe kwa malaya wake aonekane anayaweza, kaotea ka laki 3 kake ka udalali anachukua gari yako kisela mwisho wa siku ni mimba. Huwa wengi wanaoazima magari hupenda masifa barabarani. Atakimbiza hovyo breki za hovyo kuovateki resi nyingi mara apige drift na Crown yako mwisho limemshinda kalibamiza ukutani balaa linakuwa zito na hana la kufanya.

Kanuni ya pili muhimu, mtu awe na hela yaku encounter any shortcoming. Barabarani kuna mengi kuna jamaa yangu huwa anaagiza gari na kuziuza baada ya kutumia kidogo tu. Jamaa hajawahi kuwa na gari chakavu hata siku moja, na gari zake kama sio mark x ni crown au brevis ndio huwa anatemebelea.. Kipindi flani akiwa anasubiria imports huwa mtu wa kusafiri safiri hivyo ana connection na wana wenye magari anaazimaga magari na watu wanam trust sababu ni smart sana. Kuna siku kachukua crown akapiga nayo Moro-Chuga kuna mahali alipiga jiwe akapasua gearbox. Aliagiza gearbox mpya akafunga na kuendelea na safari akarudisha gari ikiwa nzima kabisa. Ila sasa imagine angekuwa ni bishoo tu ana hela yake ya mafuta tu. Ndio unapigiwa simu ya breakdown unaanza kuumia tu na kujuta.

Kuna nidhamu flani kwa mtu ambaye anaujua uchungu wa gari na kulihudumia. Kuna watu smart unaweza muazima gari ila kama ni wale vijana jamii ya Chawa weka mbali na watoto.
 
Kabisa yan jamaa alilipga mzinga halafu likamwagka vioo vyote vya kushoto na taa ya mbele na nyuma upande wa kushoto, likachanika huo upande hadi linaonekana ndani. Halafu akaenda akalipaki baada ya siku 3 akanikana yule jamaa
Ulimpotezea/ulisamehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…