Balaa la kuazimisha gari!!!

Mwana alipona wala sikumlipisha na ni mshkaj kiroho Safi bado!!
Ulifanya vyema, nilishaazimwa gari sijui ilikuaje akaja ndugu yake na alieniazima akaniambia kaagizwa nikamuamini kwakuwa nilishawahi kumuona na jamaa. Picha linaanza ajui kuwasha ni push to start, akaniita anaomba funguo ya gari πŸ˜‚ nikaona sio kesi nikamuelekeza kuwasha huyo akawasha akaondoka bila hata kutoa hand break(nikajisemea watajua wenyewe huko). Zikapita kama dakika 7 hivi mwenye gari huyu hapa ananiambia gari iko wapi nimepata dharura naomba, nkamwambia si umemtuma fulani aje achukue? Akahamaki sijamtuma mtu gari na yule amelewa na gari hajui kuendesha we ulishawahi kuona nimempa gari au akiendesha? Acha mambo ya kisΓ—nge nataka gari. Nilimind, simu ya jamaa ikaita kupokea anaambiwa ndugu yake kagonga bajaji kwa nyuma awahi kabla mamwela hawajafika, tukauma boda adi eneo la tukio ikabidi nisimamie mambo yakae sawa nikampooza dogo wa bajaji tukaondoka. Gari ilivunjika taa jamaa hakunidai chochote ila kiuungwana nilimchangia kidogo. Siji azima gari tena
 
Mwamba umlimuazimisha akapandishwa mizuka ili amalize kisahani atambe[emoji16]
 
Duuh watu wengine wanazingua sanaa
 
Siku Baada ya kuazimiaha gari.....Toka Nampa nilikuwa na wenge ......but nkampa si ushikaji tu


Jioni hii jamaa haleti kwenye simu hapatikani ..... after while...kapiga simu akisema " broo naomba tuongee""[emoji24][emoji24] pale pale nguvu ziliisha
 
Pale mkuranga karibu na mskiti au karibu na traffic wanapokaa nyuma au baada ya mzani Kuna jamaa alipeleka gari ioshwe asubuhi .Yeye akarudi kazini kwake siikumbuki ni mkwalia hospital au halmashauri.Akaacha funguo ila aliwasisitiza walioshe tu hata kulisogeza wasilisogeze.Wakajidai wameelewa.Jamaa aliwambia likiwa tayari awaambie .Muda ukapita mrefu akapata wasiwasi akapanda boda kwenda kufuatilia gari lake.Kufika gari halikuwepo.Alipowaluza wakamuambia utumbo kuwa Fulani alitoka na gari limepata ajali mkuranga mjini.Sijui kilichofuata Mimi niliondoka.
 
Hivi ngono ni nuksi au utamu? NB UKIMWI umekaa kimya kama haupo
 
Ila urafiki ni mgumu sana kuna rafiki yangu anabrother yake alikuwa akiniazima gari lazima lirudi na dosari yaani lazima nikaja kujua jamaa huwa akishalewa umakini unakosekana nai lazima gari akwaruze au lijrudi na dosari yoyote toka nilipojua nimkumzungusha tuu.
 
Man katope daah hatari na nusu
 
Nawashauri rafiki yoyote yule kabla hujampa dhamana ya urafiki mmulike ni mwenye nafsi gani, na roho gani, mfano chuki, choyo, unafiki, uchawi na ushirikina wa pesa pesa
 
Tabia hii ndo ninayo mimi

Mimi uwezo wa kuazima gari sina ila piki piki huwa ndo naazima sana sababu uwezo wa kununua mpya ninao hata kama nitaipaki sehemu kisha ikaibiwa

Pia ninapoazima piki piki ya mtu nahakikisha mfukoni nina ka 100k kwa ajili ya dharula

Samahani kwa kuchangia uzi unaowahusu wenye magari
 
Ndo yaafaa ivyo niliwahi angusha boxer ya jamaa katika kupaki ikapasua kioo cha dashboard, chaap nikamwekea kipya alikuja jua baadae Sana kwa kumwambia
 
Mwaka 2017 nilifungua salon ya kiume mitaa yetu kipindi hicho hapakuwa na salon nyingine Kwa zaidi ya Mita 700 kutoka pale ambapo nafanya biashara.
Sasa ikija ishu ya kinyozi kufanya NGONO ndani ya salon na alikuwa analala Hadi asubuhi na wanawake nakumbuka biashara ilikuwa Kwa kipindi kifupi Sana cha miezi 8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…