chukuachako
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 1,209
- 817
salam si lazima aaaaah
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ali kiba ndio nani?
![]()
Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.
Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Diamond Platnumz na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi ya tamasha.
Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ubuyu, hatimaye muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.
Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.
Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.
Wana uswahili sana!
Kuna sehem niliona wanawasema watu wanaopenda kusema tabia fulani mbaya ni ya kiswahili.. ie huyu mswahili sana...
Kuna sehem niliona wanawasema watu wanaopenda kusema tabia fulani mbaya ni ya kiswahili.. ie huyu mswahili sana...
waswahili tuna taabu sana, kila baya lisilofaa tunaambiwa ndio uswahili sijui tulikosa nini.
Hawa ni wapuuzi wanatakiwa kukemewa hivi leo hii kama mmoja ikitokea hayupo aliyebaki atamlilia mwenzie? Mimi bado namlaumu Kiba maana yeye ni mtu mzima kuzidi Diamond ..kutosalimiana ni upuuzi ulio pitiliza.
Haya mabifu ya kipuuzi sana! mabeef tuwaachie wakina Suge knight, wakina 50 cent wakina TI siyo hawa wajiga wanagombeana wananaume
nashangaa sana mi nawalaumu hivi ukijishusha unapungukiwa nini ?!!au ndo wanamuogopa shigongo ataandikiwa"A kamshobokea B"
wapumbavu sana hawa
Msanii chipukizi