Balaa tupu! Diamond, Ally Kiba wakutana ukumbini, wachuniana!

Balaa tupu! Diamond, Ally Kiba wakutana ukumbini, wachuniana!

diamond-667x500.jpg

Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.
Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi ya tamasha.
Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ‘ubuyu’, hatimaye muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.

Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.
Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.
Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.



Wadaku ndo wanayakuza haya, kwani pale palikuwa mahali pa kupeana mikono? Wao hawajawahi kusema kama wana bifu lakini watu wasiopenda mafanikio ya wenzao kila siku wanadakua !!!
We shall make it anyway!
 
Kuna sehem niliona wanawasema watu wanaopenda kusema tabia fulani mbaya ni ya kiswahili.. ie huyu mswahili sana...

waswahili tuna taabu sana, kila baya lisilofaa tunaambiwa ndio uswahili sijui tulikosa nini.
 
Mimi sioni tatizo lolote hapo. Mtu huwezi kushoboka wakati unajua wazi hampatani.
 
Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali
wawili wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond
Platnumz’ na Ali Saleh Kiba , limekwisha, basi umenoa
baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana .
Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye
mkutano .
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree
Hilton jijini Dar , juzikati ambapo wasanii mbalimbali
walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu
za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya
maandalizi ya tamasha .
Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya
kutaka ‘ ubuyu’ , hatimaye muda wa kuingia Kiba
ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu
wanne .
Alipofika , Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa
bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond
kutimba na timu yake kubwa .
Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu
yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha
yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya
kijamii .
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa
salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake , lakini cha
kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond
walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja
akiwa ameuchuna na kampani yake .
Hata hivyo , wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha
mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa
kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho
kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye
mkubwa zaidi kistaa .
Katika kujitambusha , Kiba ndiye aliyeanza huku kila
mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo
zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake .
 
diamond n kiba pichani
 

Attachments

  • 1421579199903.jpg
    1421579199903.jpg
    34.3 KB · Views: 1,699
ali kiba ni msanii local, diamond ni msanii wa kimataifa...
 
Hawa ni wapuuzi wanatakiwa kukemewa hivi leo hii kama mmoja ikitokea hayupo aliyebaki atamlilia mwenzie? Mimi bado namlaumu Kiba maana yeye ni mtu mzima kuzidi Diamond ..kutosalimiana ni upuuzi ulio pitiliza.

Haya mabifu ya kipuuzi sana! mabeef tuwaachie wakina Suge knight, wakina 50 cent wakina TI siyo hawa wajiga wanagombeana wananaume

nashangaa sana mi nawalaumu hivi ukijishusha unapungukiwa nini ?!!au ndo wanamuogopa shigongo ataandikiwa"A kamshobokea B"
wapumbavu sana hawa

Hawa jamaa wako kibiashara zaidi. Wala msishangae kawaida tu na hata hilo bifu lenyewe naona kama ni habari tu ya kuuza gazeti. Kwani ni wangapi hawakusalimiana hapo ukumbini ukiacha hao jamaa wawili.

Hizi stori tu ili shigongo auze, stuka.
 
Na wanaozikuza ni ninyi ninyi mnaosema hapa waache bifu za kijinga kwa kujidai Team Diamond Vs Team Kiba....

Mnachochea moto....moshi ukifuka mnalalama
 
Back
Top Bottom