Balali alishakufa hatukuambiwa?

Balali alishakufa hatukuambiwa?

Mtanganyika, kama yuko hai kwanini usilete picha, kutuambia nyumba alipo au kama alivyofanya chenge tumsikie sauti yake? Mtafutieni gazeti la leo leo apige nalo picha halafu mnitumie mwanakijijiatklhnews.com

I still stand on the original story ni mfu tu ambaye hasikiki, haonekani, na hajulikani alipo. The burden of proof is on him to show that he is alive. Otherwise, ushahidi wote wa kimazingira unaonesha kuwa alishatutoka. Serikali inawezekana inajua hilo na haijui ianzie wapi kuwaambia watanzania.
 
heshima mbele,hapa naona mwanakijiji hajathibitisha kuwa balali amekufa,ila anachosema yeye ni kutokana na ushaidi wa kimazingira.
KUNA MKUU HAPO JUU anadai kuwa balali anadunda US,wakati huo huo anataka ushahidi kama balali amekufa,haina maana kwasababu kama vyanzo vyako vinathibitisha balali anadunda kisela hapo US basi hii ndio nafasi yako kutupatia ushaidi kuwa balali hajafa.
 
MKJ sasa huwezi kufikia conclusion kwa kutumia Logic, huwezi sema kama A is equal to B and B is equal to C then A=B. No it's not that simple. Tumeshaona baadhi ya vigogo wengi huko African and America wanapotea for years mpaka watu wana conclude kwamba wamekufa. Kumbe wapo katika nchi nyingine.

I know it sound like dark, it smell like dark, and it look like dark, but guess what it is not dark. It just rain. Balali yupo fine anadunda kama kawaida. CCM wanajua Balali siku atakayo tua tuu airport that will be the end of CCM, Chama Cha Mapinduzi kitapasuka into two peaces.

Balali analawyer wake hapo Dar kwa nini CCM hawataki kwenye kuangalia document zake alizomkabidhi Lamwai wake? Balali know kabisa EPA=Uchaguzi wa uraisi wa 2005=Rostam=JK sasa JK anajivisha joho linaloitwa Mr clean, sasa ukiunganisha hiyo picha JK anasound Mr. Dirty, na yeye hawezi likubali hilo. Kwani siku Balali atakapo tua ndio AU and EU watajua who is JK.
 
serikali haijui alipo na haijui kama ni mzima au mfu; jamaa alikuwa mgonjwa na hadi leo serikali haijasema kama alipata nafuu au anaendeleaje kwa sababu hawajui alipo; nimepitia sehemu mbalimbali ambako anadaiwa alikuwepo na kweli hayupo. Siyo Boston wala DC.. ila wanasema "yupo".

Tangu alipotoweka hajapigwa picha akiwa hospitali, hajazungumza na chombo chochote cha habari, na hakuna kiongozi (akiwemo waziri wa fedha) ambaye anajua alipo.

Sasa, mimi katika kupiga mahesabu yangu na kuangalia vyanzo mbalimbali inaonekana jamaa hayupo tena - amekufa. Sasa hilo haliwezi kuwa jambo la ajabu, ni bora tuambieane ukweli tu ili tukubali yaishe.
 
Waache watuzuge tu, wataona maajabu
 
Nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu

ban.kijiji.jpg

M. M. Mwanakijiji

HADITHI moja ya utotoni inahusu jamaa mmoja aliyefanikiwa kumkamata ndege aliyekuwa anaharibu mazao yake, na ambaye kwa muda mrefu ilishindikana kumkamata.

Katika hadithi tunasimuliwa kuwa baada ya kumkamata ndege huyo, akawapa watoto wake wamuandae kuwa kitoweo. Hata hivyo, tunaambiwa ndege huyo wa ajabu alianza kuimba pale tu alipoanza kuchinjwa na kuwaimbia wale waliokuwa wanamchinja; "wewe nichinje tu utaona maajabu." Ndege huyo wa kwenye hadithi alipoanza kunyonyolewa aliendelea kuimba wimbo wake huo wa uchuro kuwa; "wewe ninyonyoe tu utaona maajabu." Ninajua wengi wetu mtakumbuka kisa hicho ambacho kinasimuliwa kwa namna tofauti sehemu mbalimbali. Mwisho wa kisa hicho ni pale ambako ndege huyo baada ya kugeuzwa mlo, basi anajiunganisha na baadaye kupeperuka na kuonyesha maajabu yake. Huyo ndege hakufaa kuliwa.

Na mimi leo najikuta kwa niaba ya Watanzania wengine nianze kuwalilia watawala wetu kama yule ndege wa ajabu wa kwenye hadithi. "Nyie tuzugeni tu mtaona maajabu." Watanzania tunazugwa, na uzugaji wenyewe wakati mwingine si tu wa kuudhi, bali wa kukera kweli kwani unatuchukulia sisi sote kama watu wasio na ufahamu wa aina yoyote na tusioweza kujua kuwa tunazugwa.

Nilipoandika mwishoni mwa mwaka jana katika salamu zangu za mwaka mpya kwako msomaji, nilisema mwakani (yaani mwaka huu) watawala wetu watakapojaribu kutuzuga wahakikishe kuwa wanatuzuga tukazugika. Kwa masikitiko makubwa naomba niwatangazie kuwa hawajafanya jitihada zozote za kutuzuga na badala yake wanatuzuga ‘alimradi' tu watuzuge. Matokeo yake ni kuwa, wao wanaendelea kutuzuga pasipo jitihada zozote za maana na hivyo inakuwa rahisi sana kuwashtukia

Wametuzuga vipi? Siku za hivi karibuni kuna matukio kadhaa ambayo yameendelea nchini na ambayo kwa hakika naweza kusema ni ya kizugaji mno. Nitayachambua kwa haraka haraka na kuonyesha kuwa ni kwanini matukio haya ni ya kizugaji na ambayo hatuwezi kuyapa majina mengine isipokuwa uzugaji wa daraja la kwanza

Siku ya Jumapili marais wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walikutana jijini Dar es Salaam katika jitihada za kutafuta usuluhishi wa migogoro waliyonayo, na ambayo inaweza kusababisha mapigano ya vikosi vyao kama yaliyotokea miaka michache iliyopita.

Marais hao Joseph Kabila wa DRC na Yoweri Museveni wa Uganda, walifanya mkutano wao na hatimaye kufikia makubaliano chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika.

Siku chache zilizopita, waziri wetu wa mambo ya nchi za nje, Bernard Membe ameshiriki vilivyo katika kufuatilia suala la mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Zimbabwe na wiki chache za nyuma watawala wetu walikuwa mbele kupeleka vikosi vyetu Visiwa vya Comoro kutafuta usuluhishi wa kumuondoa Mohamed Bacar aliyejivika urais wa visiwa vya Anjouani. Tulifanya hivyo baada ya kuombwa na rais wa shirikisho la visiwa hivyo. Hivyo ndivyo Rais Kikwete alivyosema

Kabla ya suala la Comoro, Rais Kikwete alishiriki na kufunga safari kwenda Nairobi kushiriki katika kutafuta suluhishi la kisiasa la matatizo ya Raila Odinga na Mwai Kibaki hadi kuwafanya watiliane sahini za makubaliano ambayo hatimaye yalisababisha Raila kumkubali Kibaki na yeye kupewa uwaziri mkuu.

Bila ya shaka unajua nakwenda wapi na hoja hii.

Sasa cha kusikitisha ni kuwa rais huyu huyu Kikwete na timu yake ya ‘upatanishi' wamechukua zaidi ya miaka miwili tangu ahadi yake ya kutafutia usuluhishi ‘mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar'. Kinachonishangaza mimi zaidi ni kuwa, Zanzibar ni kero za kisiasa na mambo ya chuki tu, lakini hawajafikia mahali pa kuchinjana kama Kenya, Comoro, au Zimbabwe. Yaani Rais Kikwete amefanya haraka kwenda kuzima moto kwa jirani wakati kwake kumeanza kufuka moshi.

Jumapili hiyo hiyo wakati kina Museveni wanatafuta usuluhishi, timu ya CCM ya mazungumzo ya muafaka wakaamua kwa jazba yote kutoa lawama rasmi dhidi ya CUF na kuwalaumu kwa jinsi wanavyoendesha mambo. Cha kusikitisha sana ni kuwa, wakati Rais Kikwete anajitahidi kuwapatanisha majirani, ameshindwa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani na hasa kuwaleta kwenye meza ya majadiliano Rais Aman Abeid Karume na uongozi wake na Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake kufikia suluhisho la kudumu.

Kwa mfuasi wa Mwalimu kama mimi, naomba nionyeshe kusikitishwa na uzugaji huu wa kushadadia mambo ya nje wakati watu wetu kutoka Pemba leo wanaanza kuwa na mawazo ya kujitenga kutoka jamhuri yetu. Nahuzunika zaidi kwa sababu badala ya kujifungia Ngurdoto na kutafuta suluhisho tumebakia kuwaita ‘wahaini' na kuwapiga mikwara kwa sababu wanajihisi wageni katika taifa lao wenyewe

Kama huu si uzugaji tuupe jina gani? Iweje tuwe kimbelembele kutatua ugomvi wa majirani wawili wakati watoto wetu wametiana kabari? Ni kitu gani kinamfanya Rais Kikwete kuwakaribisha wageni na kujihusisha yeye mwenyewe na usuluhishi wa matatizo yao wakati haya ya nyumbani amewaachia watu wasioweza kabisa kutafuta muafaka? Mimi hili naliita uzugaji tu. Tatizo la Zanzibar si kubwa kulinganisha na la Zimbabwe, Comoro, Kenya, Uganda na DRC au hata la Somalia. Tatizo la visiwani ni tatizo la nia ya kweli ya kuishi kama watu wamoja na wananchi wa taifa moja. Viongozi wa CCM na wa CUF wote hawana nia ya kweli ya kutafuta suluhisho la kweli. Maneno yao ni sumu pande zote mbili, wanamwaga sumu kila kukicha hata hatuelewi wanachojaribu kuthibitisha ni nini huko Zanzibar. Huyu anasema hili, mwingine anaibuka kesho na kusema lile kuhusu jambo hilo hilo.

Leo hii kwa kuonyesha ubabe wao wa nguvu za dola, wameamua kuwakamata watu ambao wameamua kuonyesha manung'uniko yao kwa kujenga hoja kuwa hawatendewi sawasawa katika taifa lao. Badala ya kukaa chini na kuwasikiliza kiini cha malalamiko yao, tunaamua kuwatia pingu. Hili suala la Pemba litatupeleka ambako hatukutaka kwenda, na sasa pole pole tunaanza kufika. Niwaachie wengine walizungumzie hilo.

Ujumbe wangu, Rais Kikwete aitishe mkutano wa dharura usiokuwa na masharti kati ya viongozi wa Zanzibar wa pande zote mbili na wadau wengine wa visiwa hivyo, kwani hatuwezi kuviachia vikundi viwili vya kisiasa kutatua matatizo na hatima ya wananchi wote wa Zanzibar.

Hili wazo kuwa CCM na CUF ndio wamiliki halali wa Zanzibar ni wazo duni, la kupingwa na wakati umefika kwa viongozi wa dini wa Zanzibar na wadau wengine kutaka wahusishwe katika mazungumzo ya muafaka ili hizi pande mbili zisije kufanya maamuzi ya kulinda maslahi ya vyama vyao na si maslahi au mustakabali wa sehemu ya taifa letu. Kwa hili hamtuzugi tena, kwani ‘nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu'!

Lakini uzugaji mwingine ambao tumeushuhudia siku chache zilizopita ni pale ambapo Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo alipotangaza wazi na kwa ujasiri mkubwa kuwa yeye mwenyewe alipokuwa Marekani muda si mrefu uliopita alijitahidi kumtafuta aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daud Balali bila mafanikio.

Na akasema kuwa ati mara ya mwisho waliambiwa amepelekwa kuuguzwa na hivi sasa hajulikani alipo. Kimsingi ujumbe uliotumwa kwa maelezo ya Mkulo ni kuwa Balali hapatikani.

Lakini hata hivyo kama sisi ni wakazi wa nchi ya kufikirika ambayo mfalme wake ni mfalme Juha, saa chache baadaye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu akaitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwatangazia watu kuwa; "serikali haimtafuti Balali, na ikitaka kumtafuta itampata kwani serikali ina mkono mrefu."

Sasa nina uhakika alikuwa ana lengo la kuonyesha kuwa serikali yetu inaweza kabisa kumtafuta inayemtaka na kumtia mikononi pale inapobidi. Sasa hili si la mjadala kwani serikali isiyokuwa na uwezo huo ni serikali ya nchi ya Wagagagigikoko ambako Bulicheka alikwama kwenye nyumba yake ya kwenye minazi na Wagagagigikoko hawakumfikia!

Sasa walichotuzuga hapa ni kwamba, huyu Mkulo si yuko kwenye serikali hiyo hiyo? Huyu Mkulo si ndiye Waziri wa Fedha na ambaye Benki Kuu iko chini yake kwa namna fulani? Sasa anapozungumza si anazungumza kama waziri wa serikali na maneno yake ni maneno ya serikali?

Sasa inakuwaje kesho yake Ikulu waseme serikali haimtafuti Balali wakati waziri mwenye dhamana ya fedha anasema yeye mwenyewe alimtafuta? Sidhani kama alimtafuta ili ampe pongezi ya kujiuzulu au kutimuliwa kazi!

Sasa kama waziri wa serikali anasema kitu ambacho serikali haifanyi sisi tuelewe nini? Jumatatu tumesikia kwenye taarifa ya habari ya TBC kuwa serikali imepiga marufuku ufunguzi wa vituo vipya vya kulelea yatima kwani vinatumiwa vibaya na kuwa wanataka mtu anayetaka kusaidia yatima basi apitishe misaada kwenye serikali.

Hayo tunaambiwa yalisemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo, Jinsia na Watoto Dk. Lucy Nkya. Sasa hilo lingetosha na tungepigia makofi, lakini cha kuzuga ni pale ambapo kwenye taarifa hiyo hiyo ya habari tukaambiwa kuwa Rais Kikwete kwenye ziara yake ya siku mbili huko Mwanza anatarajiwa kufungua kituo kipya cha kulelea watoto yatima!

Sasa hawa watu wako kwenye serikali moja au kuna serikali nyingine katika ulimwengu sambamba wa fizikia!?

Inakuwaje useme mmekataza kufungua vituo vya kulelea yatima halafu rais anafungua kituo kingine au vile vinavyofunguliwa na rais tu ndivyo vinaruhusiwa? Kama huku si kutuzuga tuite nini huku ndugu zangu? Nasema, nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu!

Lakini hayo hayakutosha yaliyonichanganya miye akili na kunifanya nidondoshe kibuyu changu cha ulanzi na kupaliwa hadi masikio yakaniuma ni pale watu wawili wa serikali waliposimama na kutuambia mambo ya ajabu.

Katibu Mkuu Hazina, Gray Mgonja ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Tangold alipodai kuwa yeye aliweka sahihi kwenye kampuni hiyo kama mkurugenzi, ‘akiamini' kuwa kampuni hiyo ni ya serikali. Ni kampuni hiyo hiyo ambayo mkurugenzi wake mwingine ni mzee wa ‘vijisenti' ambaye naye aliingia kulinda ‘maslahi ya serikali'.

Lakini cha kuchefusha roho ni pale ambapo Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu alipojitokeza saa chache baada ya Mgonja na kudai kuwa kampuni hiyo si ya serikali na akawakatalia waandishi kuihusisha benki hiyo kuu ‘iliyo chini ya utawala mpya' na kampuni hiyo ya Tangold. Kichwa mwenzenu kikaniuma na hamu ya chakula ikanitoka.

Nikabakia kushangaa, hii kampuni tuliambiwa ya serikali, ikaingia na kupata fedha nyingi toka Benki Kuu; mmojwapo wa wakurugenzi alikuwa waziri na mwingine bado ni Katibu Mkuu wa Hazina (yaani kule kunakosimamia kila senti ya shilingi yetu ya madafu). Sasa leo mtu ambaye kwa hakika anapaswa kujua kuhusu hii kampuni ambayo aliyemtangulia alikuwa gavana anaposema kuwa si kampuni ya serikali na sisi tunaendelea kuwafungulia milango kina Mgonja kwa imani yao kuwa ilikuwa ni kampuni ya serikali licha ya kusajiliwa nje ya nchi, zimo kweli au ndio tumepigwa ganzi ya ufisadi na hatusikii maumivu ya uzembe? Nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu! Mifano ipo mingi ya uzugaji wa daraja la kwanza ambao kwa hakika sasa unahitaji kutunukiwa shahada ya uzamili ya uzugaji uliotukuka. Hebu nimalizie na suala la mgodi wa Buhemba ambao tunaambiwa ni wa serikali.

Cha kushangaza ni kuwa mgodi huu unalindwa na askari wetu, lakini hakuna anayejua nani anaumiliki. Mkaguzi Mkuu wa Serikali Ludovick Utouh akajitokeza na kusema katika mafaili yake ya makampuni ya serikali mgodi huu haumo! Yaani haukaguliwi; hata Mbunge Nimrod Mkono ambaye naye ana tetesi kibao za madili ya ajabu ajabu anaposimama na kuhoji umiliki wake, sote tunashangaa.

Hivi kweli hii serikali ina mkono mrefu wa kumtafuta Balali? Huo mkono mrefu una uwezo wa kukurupuka kuwakamata watu waliotoa majina na sahihi zao kutoka Pemba, lakini umekuwa gutu kumkamata yule fisadi mwingine aliyeturusha rada, Saileth Vithlani ambaye tumeambiwa hadi mji alioko? Yaani anatafutwa na polisi wetu, lakini wanajua alipo?

Huu mkono mrefu wa serikali ulioweza kwa haraka kwenda kuwakamata watoto waliofanya vurugu chuo kikuu na kuwakimbiza kuwafikisha mahakamani kwa mbwembwe, lakini umekuwa na ‘kigugumizi' kuwakamata waliofanya vurugu katika akili, hisia na mioyo ya Watanzania kwa kujiuzia mali za Watanzania kinyemela?

Ukiwa umebakia kama mwezi mmoja tu kabla ya Kamati ya Mwanyika kumaliza kazi zake, wanathubutu kutuambia kweli ati ‘serikali haimhitaji Balali kwa sasa'?

Sasa gavana aliyehusika na ‘uhalifu' huu kweli hahojiwi, hajulikani alipo, lakini wana ujasiri wa kutuambia kuwa wakitaka watampata? Kweli uchunguzi wote utakuwa kamili bila Balali kuhojiwa?

Maajabu yanakuja; maajabu ambayo Watanzania wataendelea kuwazomea mafisadi sasa hadharani na kwenye magari yao wataanza kuandika majina yao; maajabu yanakuja pale ambapo mtaona watu wanatikisa vichwa kwa dharau pale mtakapowaambia kwa mbwembwe kuwa; ‘tuna mkono mrefu' halafu mkono unakurupuka kumkamata na kumfikisha mahakamani binti aliyepiga picha za utupu na kutangazwa Tanzania kana kwamba ndiye fisadi mkuu, lakini yule aliyewaacha wana na mabinti zetu utupu wa rasilimali zao huku akisindikizwa na ving'ora akiendelea kudunda tu.

Maajabu yapo kwa sababu watu wataanza kutambua kuwa haki ya mwanadamu haizimwi kwa vitisho au kwa ubabe. Manung'uniko ya ndugu zetu wa Pemba hayawezi kumalizwa kwa kuwatishia uhaini badala ya kuwasikiliza? Wahaini si waliojitokeza hadharani na kusema matatizo yao baada ya viongozi wa nchi yao kukataa kuwasikiliza na kuwapuuza kwa maneno ya kejeli.

Wahaini ni wale walioisaliti nchi hii na kuitakia mabaya kwa kutengeneza mikataba mibovu, kupitisha sheria za kuwalinda na walioamua kugawiana kama njugu rasilimali za nchi yetu. Ni wale ambao wameamua kugawiana viwanja vya jiji letu kana kwamba wanagawiana tende kiasi kwamba mtu akijaribu kupanga au kununua jengo unajikuta unaambiwa ‘limechukuliwa na Imelda Marcos'.

Watawala mjipendao na mnaopenda kupendwa, ipo haja ya kukaa chini na kujiuliza ni wapi mmekosea na mgeuke. Hamuwezi kuendelea kubadilisha Baraza la Mawaziri kila inapotokea kashfa mwisho itabidi tuombe Baraza la Mawaziri kutoka Japan na Waziri Mkuu kutoka China. Tusipoangalia tutaomba na Mwanasheria Mkuu kutoka Uingereza kwani kila anayepata nafasi ana kashfa nyuma yake.

Hata kama ni kutuzuga basi mjitahidi kidogo. Mtuzuge tusiwashtukie. Kwa mfano badala ya kuwaacha hawa jamaa wajiuzulu muwatimue; badala ya kufanya majadiliano na walioiteka nchi, mnawatia pingu na kuwapeleka Kisutu; badala ya kusema hamjui Balali aliko mnatuma watu kwenda kumtafuta badala ya kutuambia ati mkimtaka mtampata, ‘unless' mnajua alipo na hamtaki Watanzania wajue alipo.

Binafsi swali ambalo ningependa nijue jibu lake ni: "Hivi Balali yuko hai?" Maana kama hamjui aliko kama alivyosema Waziri Mkuu Jumatatu, mnajuaje kama yuko hai au alishakufa na kuzikwa Mississippi?

Ila kama mnajua yuko hai ina maana mnajua aliko na mnatuzuga kuwa hamjui. Haya bwana, nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu!

Siku moja, ndege mnayefikiri mmemkatakata vipande na mmemgeuza kitoweo ataruka na kuwa huru tena! Mmeonywa.

Mwanakijiji Chukua Tano Mkuu.
 
serikali haijui alipo na haijui kama ni mzima au mfu; jamaa alikuwa mgonjwa na hadi leo serikali haijasema kama alipata nafuu au anaendeleaje kwa sababu hawajui alipo; nimepitia sehemu mbalimbali ambako anadaiwa alikuwepo na kweli hayupo. Siyo Boston wala DC.. ila wanasema "yupo".

Tangu alipotoweka hajapigwa picha akiwa hospitali, hajazungumza na chombo chochote cha habari, na hakuna kiongozi (akiwemo waziri wa fedha) ambaye anajua alipo.

Sasa, mimi katika kupiga mahesabu yangu na kuangalia vyanzo mbalimbali inaonekana jamaa hayupo tena - amekufa. Sasa hilo haliwezi kuwa jambo la ajabu, ni bora tuambieane ukweli tu ili tukubali yaishe.

Serikali ilizusha mama wa mmoja wa council ya manispaa ya Kigoma anaumwa Malaria kali, ikamvisha na madrip kabisa kuonekana amezidiwa siku ya uchaguzi. Kumbe lengo lilikuwa asipige kura.

Serikali ya Tanzania kama iliweza kuwaita Jamboforums member ma gaidi itashindwa kusema Balali amezidiwa? Balali wasn't sick anyway. Ile ilikuwa ni strategic planning ya Jakaya and Lowassa na Rostam kuficha swala zima la EPA. Balali angetapika tuu ukweli, so swala likawa wewe potea na million zako kadhaa kisha tuachie sisi hii nightmare. And guess what, they were right. EPA will remain a mistry.
 
Balali kama uko hai jitokeze kama Mzee Vijisenti usalimie wananchi na uishangaze serikali kwamba we dume la mbegu unadunda ila serikali imeshindwa kukupata
 
Serikali ilizusha mama wa mmoja wa council ya manispaa ya Kigoma anaumwa Malaria kali, ikamvisha na madrip kabisa kuonekana amezidiwa siku ya uchaguzi. Kumbe lengo lilikuwa asipige kura.

Serikali ya Tanzania kama iliweza kuwaita Jamboforums member ma gaidi itashindwa kusema Balali amezidiwa? Balali wasn't sick anyway. Ile ilikuwa ni strategic planning ya Jakaya and Lowassa na Rostam kuficha swala zima la EPA. Balali angetapika tuu ukweli, so swala likawa wewe potea na million zako kadhaa kisha tuachie sisi hii nightmare. And guess what, they were right. EPA will remain a mistry.

kama Balali alinyamzishwa kusema ukweli Tanzania kwa nini asiuseme sasa hivi? itamchukua dakika ngapi kujirecord akizungumzia kila kitu na kupost video youtube? Hapa Balali naye sio muungwana na hana uchungu na anachozushiwa uko Tanzania.
 
na miye namba yangu wanayo... anaweza kupiga simu na kuacha ujumbe na kusema tarehe na kusema some of the current events kama earthquake ya China au kimbunga cha Mynmar 1 248 686 2010
 
na miye namba yangu wanayo... anaweza kupiga simu na kuacha ujumbe na kusema tarehe na kusema some of the current events kama earthquake ya China au kimbunga cha Mynmar 1 248 686 2010

ha ha wadau hawakawii kuhoji authenticity ya sauti...I think I will stick with a video idea na tarehe ya siku hiyo na awe amekaa mbele ya tv inayoonyesha kitu kinachoendelea kipindi hiki i.e NBA playoffs au mambo ya uchaguzi lakini again inaweza kuwa doctored vile vile... idea ya yeye kushika gazeti la siku hiyo ni nzuri zaidi.
 
Hakuna sababu ya kudai kuwa Balali amefariki bila ya kuwa na ushahidi. Ukweli ni kwamba Balali yuko tayari kufanya lolote ili asiweze kujibu mashtaka ya ufisadi yanayomkabili ikiwa ni pamoja na kufeki kifo. Nadhani hata huo "ugonjwa mahututi " aliodaiwa kuwa nao ilikuwa ni "exit strategy" ambao natural conclusion yake ulishapanga uwe ni "kifo" cha kuigiza.
 
kama Balali alinyamzishwa kusema ukweli Tanzania kwa nini asiuseme sasa hivi? itamchukua dakika ngapi kujirecord akizungumzia kila kitu na kupost video youtube? Hapa Balali naye sio muungwana na hana uchungu na anachozushiwa uko Tanzania.

Sijasema Balali ni clean, hawezi kwenda Youtube akasema jamani wa Tanzania haya ndio yaliyotokea. Balali alishachukua chake akanunua zake mansion huko ng'ambo kama wenzie.

CCM ilimwambia kwamba mzee potea kwenye ramani na kisha tuachie hili. Swala la kushangaza watu wengi hatujui kabisa ni nani huyu Balali.

Who is Balali? Jee huyu Jamaa ana ndugu? Alizaliwa wapi Balali? Jee wanae Balali wako nchi gani? CCM inaonekana iliweka mtu wa mazingaombwe pale Bank Kuu, mtu ambae hana ndugu wala marafiki wa kutambua alipo.
 
Usije ukashangaa siku wanatangaza tamati yake wakaongezea kuwa hakuwa Mtanzania.
 
MKJ sasa huwezi kufikia conclusion kwa kutumia Logic, huwezi sema kama A is equal to B and B is equal to C then A=B. No it's not that simple. Tumeshaona baadhi ya vigogo wengi huko African and America wanapotea for years mpaka watu wana conclude kwamba wamekufa. Kumbe wapo katika nchi nyingine.

I know it sound like dark, it smell like dark, and it look like dark, but guess what it is not dark. It just rain. Balali yupo fine anadunda kama kawaida. CCM wanajua Balali siku atakayo tua tuu airport that will be the end of CCM, Chama Cha Mapinduzi kitapasuka into two peaces.

Balali analawyer wake hapo Dar kwa nini CCM hawataki kwenye kuangalia document zake alizomkabidhi Lamwai wake? Balali know kabisa EPA=Uchaguzi wa uraisi wa 2005=Rostam=JK sasa JK anajivisha joho linaloitwa Mr clean, sasa ukiunganisha hiyo picha JK anasound Mr. Dirty, na yeye hawezi likubali hilo. Kwani siku Balali atakapo tua ndio AU and EU watajua who is JK.

Mkuu Mtanganyika hiyo ndo habari yenyewe ya kuwa yuko mafichoni.Na huenda hata akawa jijini anatembea na gari tinted kwa ulinzi maalum.

Sisiem wanatapatapa kweli maana kila risasi wanayolenga kuua sauti za wapenda maendeleo ya Taifa hili inaenda pembeni.Ufisadi wa EPA wameshindwa kuufunika,muafaka unakwenda mrama,Richmond watu wanasubiri maelezo,Mkapa anasubiriwa naye ajitetee,nyumba za serikali zirudishwe n.k.
Kwa hiyo kuonekana kwa Balali wanahisi itakuwa TSUNAMI humo chamani maana atataja wote waliokula
 
Sijasema Balali ni clean, hawezi kwenda Youtube akasema jamani wa Tanzania haya ndio yaliyotokea. Balali alishachukua chake akanunua zake mansion huko ng'ambo kama wenzie.

CCM ilimwambia kwamba mzee potea kwenye ramani na kisha tuachie hili. Swala la kushangaza watu wengi hatujui kabisa ni nani huyu Balali.

Who is Balali? Jee huyu Jamaa ana ndugu? Alizaliwa wapi Balali? Jee wanae Balali wako nchi gani? CCM inaonekana iliweka mtu wa mazingaombwe pale Bank Kuu, mtu ambae hana ndugu wala marafiki wa kutambua alipo.

I personally nawajua watoto wa Balali(Samahani siwezi kwenda in details)...kwa kifupi... serikali haijawahi kumtafuta Balali na sidhani kama itamtafuta kamwe....!!!
 
Mkuu Mtanganyika hiyo ndo habari yenyewe ya kuwa yuko mafichoni.Na huenda hata akawa jijini anatembea na gari tinted kwa ulinzi maalum.

Sisiem wanatapatapa kweli maana kila risasi wanayolenga kuua sauti za wapenda maendeleo ya Taifa hili inaenda pembeni.Ufisadi wa EPA wameshindwa kuufunika,muafaka unakwenda mrama,Richmond watu wanasubiri maelezo,Mkapa anasubiriwa naye ajitetee,nyumba za serikali zirudishwe n.k.
Kwa hiyo kuonekana kwa Balali wanahisi itakuwa TSUNAMI humo chamani maana atataja wote waliokula

Balali na EPA ni sawa na chanda na pete. Vinakwenda pamoja, sasa ukimpata Balali utajua nani alianzisha Kagoda na kwa sababu gani, ukimpata Balali utajua mkurugenzi wa kampeni ya 2005 (Hari Mpya Kasi Mpya slogan) Mr Rostam Azizi alichota shilingi ngapi kwa Kampeni. Ukimpata Balali utajua jee Richmond na Luwassa na Rostam ni cousins?

Balali ndio center point ya wizi wote wa 10 years ndani ya BoT. The worse part more than 50% ya wizi ulihusika na kumuweka muheshimiwa madarakani. So, you can't separate the good and the ugly. Balali akipatikana ndio the end of JK or the begining of the end of JK.

Ili kustop JK express we need Balali, yaani tukimpata hata kumoji kwa 10 mins kisha mahojiano yakawekwa kwenye youtube, ooohhh JK gonna like that. Sababu the unsolve puzzle itakuwa kamili kwa less than a minute.
 
I personally nawajua watoto wa Balali(Samahani siwezi kwenda in details)...kwa kifupi... serikali haijawahi kumtafuta Balali na sidhani kama itamtafuta kamwe....!!!

Labda nikuulize, hao watoto wao wanajisikiaje wakati baba yao ndio herufi I kwenye neno FISADI, we need him to get the meaning of the whole word.

Can you lobby them wamchimbe baba yao aongee kuhusu ukweli wa EPA and JK. Sababu tukipata huu ukweli kwa maneno yake mwenye Balali, i promise you Jaji mkuu ataongoza nchi, then we will start all over again. Tanzania will be kama December 9, 1961.

Please walobby hao watoto watupatie statement kutoka kwa baba yao, kuhusu ONLY EPA and JK campaign ya uraisi.

Honest sishauri Balali arudi Tanzania, because sisi public ndio msaada wetu. Yaani Balali ndio muokozi wetu. So, plz waombe wamchimbe baba yao atupe data, then hapa hapa JamiiForum tutafunga unend episode za hii nightmare.
 
Back
Top Bottom