Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa vile Balali alipelekwa kwenye matibabu huko Marekani, matibabu ambayo yalisababisha alazwe kwa muda mrefu;
Kwa vile hali yake haikuwa nzuri na iliendelea kuwa mbaya hadi kumlazimisha amuombe Rais amruhusu aachie ngazi
kwa vile Rais hakukubali Balali ajiuzulu na baadaye kumtimua kazi akiwa mahututi kitandani;
Kwa vile Rais aliamua kuunda kamati maalumu ya kuchunguza wizi wa EPA na mhusika mkuu wa sakata hilo alidaiwa kuwa ni mahututi;
Kwa vile kwa muda mrefu sasa viongozi wetu wamekuwa wakituambia kuwa hawajui aliko Balali jambo ambalo limerudiwa tena hapo jana na Waziri Mkuu
Kwa vile Balali alikuwa mgonjwa mahututi, hana kazi, na serikali haijui alipo
Hivyo basi, madai ya serikali kuwa wakimtaka watampata hayana ukweli; Kuwa serikali ikimhitaji mtu wasiyejua alipo wataweza kumpata kwa haraka, kimsingi madai hayo ya serikali na kauli hizo hazina msingi wowote.
Kwa sababu,
Balali alishafariki na kuzikwa huko huko majuu baada ya hali yake kuwa mbaya. Na kwa vile serikali haijui alipo hawana njia yoyote ya kujua liliko kaburi lake na hawana ujuzi wowote kuwa ni mzima au ni marehemu.
Hivyo, basi anayesubiri kumuona Balali akirudi Tanzania mzima anasubiri mvua jangwani!!
RIP Balali!!
NB: Kama ni mzima bado, serikali imejuaje wakati hawajui aliko?
sasa kwanini serikali isiamue kusema tu ili tujue kuwa yameisha?
serikali haijui alipo na haijui kama ni mzima au mfu; jamaa alikuwa mgonjwa na hadi leo serikali haijasema kama alipata nafuu au anaendeleaje kwa sababu hawajui alipo; nimepitia sehemu mbalimbali ambako anadaiwa alikuwepo na kweli hayupo. Siyo Boston wala DC.. ila wanasema "yupo".
Tangu alipotoweka hajapigwa picha akiwa hospitali, hajazungumza na chombo chochote cha habari, na hakuna kiongozi (akiwemo waziri wa fedha) ambaye anajua alipo.
Sasa, mimi katika kupiga mahesabu yangu na kuangalia vyanzo mbalimbali inaonekana jamaa hayupo tena - amekufa. Sasa hilo haliwezi kuwa jambo la ajabu, ni bora tuambieane ukweli tu ili tukubali yaishe.
jamani balali hausiki kabisa na EPA au upotevu mwingine wa pesa za walalahoi,ndio maana serikali haiwezi kumtafuta juu ya hilo.kilichotokea ni serikali yenyewe ndio iliyochukua hizo pesa kwa manufaa ya viongozi wachache waliomadarakani na wengine wasiomadarakani.kutokana na hilo basi kuna watu wachache ambao walishuhudia huo mchezo na ndio naowakapatiapo ili kufungwa mdomo.
Kuna habari za kuaminika kwamba Balali amefichwa na watawala wa nchi hii. Inasemekana kabla ya kwenda US, jana yake alikuwa kwenye party na baada ya party asubuhi alikuwa anaumwa tumbo. Alipofika US airport alikuwa hoi bin taaban akakimbizwa hospitalini akiwa mahututi. Baada ya operation ililazimu madakatari kukata sehemu ya utumbo ilikuyokuwa imedhurika sana kwa sumu. Aipopata nafuu aliondolewa hospitali ya awali akapelekwa hospitali nyingine mafichoni ambako ni mke wake tu alikuwa anaweza kumwona. Sasa amepona lakini bado amefichwa.Hii yote ni kuhakikisha usalama wake. Inasemekana mafisadi walitaka afe ili kupoteza ushahidi. habari hii imetoka kwa ndugu wa karibu na Dr Balali
Tafadhali sijakuelewa! Serikali itachukuaje fedha BOT bila Balali kusaini? au unamaanisha nini unaposema Serikali? sioni namna yeyote ya kutohusika kwa balali katika sakata la wizi wa fedha zetu pale BOT na siyo hapo tu, pia Meremeta/Tan gold 160billioni and more. The Government must be responsible for Balali to appear before investigation team and finally pale high court.


Jamani wacheni story za uzushi, Balali yupo safi na anadunda hapa US. Kuna source zangu zinasema alikuwa kwenye condo yake huko Boston, kabla ya kwenda zake DC. Balali hajafa and i think its not fair kusema mambo yasio na evidence.
Kama amekufa please tuonyesheni evidence, picha za msiba, cheti cha kifo, anything kuprove the point. Other than that i think hili lina sound more Kasheshe au Udaku.
kama Balali alinyamzishwa kusema ukweli Tanzania kwa nini asiuseme sasa hivi? itamchukua dakika ngapi kujirecord akizungumzia kila kitu na kupost video youtube? Hapa Balali naye sio muungwana na hana uchungu na anachozushiwa uko Tanzania.
Duh!!! Ngoja nitafute popcorns na large drink nianze kuangalia movie...serikali haijui au haitaki tujue kuwa inajua?
Labda kwa kumzushia namna hii inaweza kuwasaidia wakawa a bit serious hawa akina Pinda. Lakini sina uhakika kama uzushi huu ni haki kwa familia ya Balal. Nafikiri ni mateso zaidi![/SIZE]