Balali alishakufa hatukuambiwa?

Balali alishakufa hatukuambiwa?

You mean ata nduguze watakuwa wameuchuna ata kutoa chozi ili waandishi wapate cha kuandika.It cant be ?
Uyo jamaa atakuwa mzima tuu ila kurudi tz itakuwa ndoto atafia uko uko!
 
Labda kwa kumzushia namna hii inaweza kuwasaidia wakawa a bit serious hawa akina Pinda. Lakini sina uhakika kama uzushi huu ni haki kwa familia ya Balal. Nafikiri ni mateso zaidi!
 
jamani balali hausiki kabisa na EPA au upotevu mwingine wa pesa za walalahoi,ndio maana serikali haiwezi kumtafuta juu ya hilo.kilichotokea ni serikali yenyewe ndio iliyochukua hizo pesa kwa manufaa ya viongozi wachache waliomadarakani na wengine wasiomadarakani.kutokana na hilo basi kuna watu wachache ambao walishuhudia huo mchezo na ndio naowakapatiapo ili kufungwa mdomo.
 
Kwa vile Balali alipelekwa kwenye matibabu huko Marekani, matibabu ambayo yalisababisha alazwe kwa muda mrefu;

Kwa vile hali yake haikuwa nzuri na iliendelea kuwa mbaya hadi kumlazimisha amuombe Rais amruhusu aachie ngazi

kwa vile Rais hakukubali Balali ajiuzulu na baadaye kumtimua kazi akiwa mahututi kitandani;

Kwa vile Rais aliamua kuunda kamati maalumu ya kuchunguza wizi wa EPA na mhusika mkuu wa sakata hilo alidaiwa kuwa ni mahututi;

Kwa vile kwa muda mrefu sasa viongozi wetu wamekuwa wakituambia kuwa hawajui aliko Balali jambo ambalo limerudiwa tena hapo jana na Waziri Mkuu

Kwa vile Balali alikuwa mgonjwa mahututi, hana kazi, na serikali haijui alipo

Hivyo basi, madai ya serikali kuwa wakimtaka watampata hayana ukweli; Kuwa serikali ikimhitaji mtu wasiyejua alipo wataweza kumpata kwa haraka, kimsingi madai hayo ya serikali na kauli hizo hazina msingi wowote.

Kwa sababu,

Balali alishafariki na kuzikwa huko huko majuu baada ya hali yake kuwa mbaya. Na kwa vile serikali haijui alipo hawana njia yoyote ya kujua liliko kaburi lake na hawana ujuzi wowote kuwa ni mzima au ni marehemu.

Hivyo, basi anayesubiri kumuona Balali akirudi Tanzania mzima anasubiri mvua jangwani!!

RIP Balali!!

NB: Kama ni mzima bado, serikali imejuaje wakati hawajui aliko?

Mwanakijiji, huu habari ni hoja au ni taarifa kuwa huyu jamaa hatunae tena duniani? isije ikawa ni uvumi wa hawa jamaa katika kumwaga propaganda iliwananchii waamini Balali amekufa na tusipige kelele za kurudishwa nchini kuja kutoa siri zao?
 
Kuna habari za kuaminika kwamba Balali amefichwa na watawala wa nchi hii. Inasemekana kabla ya kwenda US, jana yake alikuwa kwenye party na baada ya party asubuhi alikuwa anaumwa tumbo. Alipofika US airport alikuwa hoi bin taaban akakimbizwa hospitalini akiwa mahututi. Baada ya operation ililazimu madakatari kukata sehemu ya utumbo ilikuyokuwa imedhurika sana kwa sumu. Aipopata nafuu aliondolewa hospitali ya awali akapelekwa hospitali nyingine mafichoni ambako ni mke wake tu alikuwa anaweza kumwona. Sasa amepona lakini bado amefichwa.Hii yote ni kuhakikisha usalama wake. Inasemekana mafisadi walitaka afe ili kupoteza ushahidi. habari hii imetoka kwa ndugu wa karibu na Dr Balali
 
serikali haijui alipo na haijui kama ni mzima au mfu; jamaa alikuwa mgonjwa na hadi leo serikali haijasema kama alipata nafuu au anaendeleaje kwa sababu hawajui alipo; nimepitia sehemu mbalimbali ambako anadaiwa alikuwepo na kweli hayupo. Siyo Boston wala DC.. ila wanasema "yupo".

Tangu alipotoweka hajapigwa picha akiwa hospitali, hajazungumza na chombo chochote cha habari, na hakuna kiongozi (akiwemo waziri wa fedha) ambaye anajua alipo.

Sasa, mimi katika kupiga mahesabu yangu na kuangalia vyanzo mbalimbali inaonekana jamaa hayupo tena - amekufa. Sasa hilo haliwezi kuwa jambo la ajabu, ni bora tuambieane ukweli tu ili tukubali yaishe.

Hebu nijaribu kuvaa viatu vya Balali

Ninavita na ni vita ya mto mmoja na vingi tena wenye uwezo.

Vita hii mimi ndio niushahidi wa info ambao kwa adui zangu nai hatari sana kwao

kwa sasa hivi wanahangaika sana kunichanfua mbele ya umma ili kufucha machafu yao

adui zangu ni wauwaji nawanauwezo wa kunitafuta na wakaniua kwa mtindo wowote mara moja



Je ni vizuri nijitokezo ili iwe raisi kwao kunipata ili waniue kiuraisi?
Je nisijifiche ati kwa sbb mimi ninasiri nyingi hivo ni silaha kwangu?


VITA YEYOTE INAPIGANA KWA TACTICS, naona ni sawa kwa balali kujificha na kunyamaza kwa sasa hata kama anahusika

siamuni kama jamaa kafa na si vizuri kuvumisha hivyo, itapoteza muelekeo wa vitu vingi
 
jamani balali hausiki kabisa na EPA au upotevu mwingine wa pesa za walalahoi,ndio maana serikali haiwezi kumtafuta juu ya hilo.kilichotokea ni serikali yenyewe ndio iliyochukua hizo pesa kwa manufaa ya viongozi wachache waliomadarakani na wengine wasiomadarakani.kutokana na hilo basi kuna watu wachache ambao walishuhudia huo mchezo na ndio naowakapatiapo ili kufungwa mdomo.

Tafadhali sijakuelewa! Serikali itachukuaje fedha BOT bila Balali kusaini? au unamaanisha nini unaposema Serikali? sioni namna yeyote ya kutohusika kwa balali katika sakata la wizi wa fedha zetu pale BOT na siyo hapo tu, pia Meremeta/Tan gold 160billioni and more. The Government must be responsible for Balali to appear before investigation team and finally pale high court.
 
Kuna habari za kuaminika kwamba Balali amefichwa na watawala wa nchi hii. Inasemekana kabla ya kwenda US, jana yake alikuwa kwenye party na baada ya party asubuhi alikuwa anaumwa tumbo. Alipofika US airport alikuwa hoi bin taaban akakimbizwa hospitalini akiwa mahututi. Baada ya operation ililazimu madakatari kukata sehemu ya utumbo ilikuyokuwa imedhurika sana kwa sumu. Aipopata nafuu aliondolewa hospitali ya awali akapelekwa hospitali nyingine mafichoni ambako ni mke wake tu alikuwa anaweza kumwona. Sasa amepona lakini bado amefichwa.Hii yote ni kuhakikisha usalama wake. Inasemekana mafisadi walitaka afe ili kupoteza ushahidi. habari hii imetoka kwa ndugu wa karibu na Dr Balali

Hii habari inaweza kukaribia kile ninachokifikiria mimi. Tunapokuja kutofautiana ni hapo 'watawala'. Ni watawala gani hao? Watawala ni wepi na mafisadi ni wepi? Mimi nadhani kunaweza kuwa na ukweli kwamba mafisadi walitaka kumuua Balali na bado wanataka iwe hivyo ili kuficha ushahidi.

Hata hivyo swali linabaki pale pale mafisadi ni wepi? Ila bado pia ninaamini kwamba kuna mtu au watu wanaojitahidi kuokoa maisha ya Balali (nadhani yupo hai). Watu hao wananguvu sana ndiyo maana wamefanikiwa kuifumba mdomo Serikali isitamke alipo balali.

Naungana na wewe kwa sehemu ila napiga kabisa assumption yako kwamba watawala wanamlinda Balali ili usidhuriwe na mafisadi. Watawala = Mafisadi. Ushahidi kujiuzuru kwa mawaziri nk
 
Tafadhali sijakuelewa! Serikali itachukuaje fedha BOT bila Balali kusaini? au unamaanisha nini unaposema Serikali? sioni namna yeyote ya kutohusika kwa balali katika sakata la wizi wa fedha zetu pale BOT na siyo hapo tu, pia Meremeta/Tan gold 160billioni and more. The Government must be responsible for Balali to appear before investigation team and finally pale high court.

labda niseme wenye nchi yao,balali yeye aliwekwa pale na wenye nchi sio wananchi kama mimi na wewe,muda wake ulipokwisha kwa maana ya mkataba wake wa ajira basi wenyewe wakamwambia sasa tufanyie hii kazi.yeye alipewa amri tu na kutekeleza matakwa ya wakubwa wake.
 
Mimi natoa mchango wa mbwa wawili ambao hutumika kutafuta hata harufu ya mtu aliepotea.

Ntakachoomba ni viza kwa mbwa hawa kwa ajili ya kuingia Tanzania kwanza ili waweze kupelekwa ofisi alikokuwa akifanya kazi bwana Balali na tupate samples za scent yake, halafu tuendelee na nyumbani alikokuwa akiishi, magari alokuwa akitumia na hata pengine hoteli alizokuwa akipitapita hata kwa kunywa maji ya matunda tu.

Baada ya kazi hiyo itabidi tuombe viza ubalozi wa Marekani ili tuingie nchini humo na tumtafute kwa kufuatilia taarifa ambazo zimekwishawekwa humu jamvini kwamba huenda akawa yupo katika miji fulanifulani nchini humo na hasa hospitalini alikolazwa.

Ili hayo yote yaweze kutimia ninapendekeza mbwa wawili aina ya Springer Spaniel ambao ni maarufu katika shughuli za upekuzi wa kiuchunguzi.

Kwa wale ambao ni wasafiri wa mara kwa mara na hupita katika viwanja vikubwa vya ndege duniani bila shaka mtakuwa mmewahi kuwaona mbwa hawa ambao kwa umbo ni wadogo.

EnglishSpringerimg021.jpg

Huyu anaitwa Emil

EnglishSpringerSpaniel1multipartxF8FF2IMG0124Copy.jpg

Huyu anaitwa Essex Marshal


Mbwa wa aina hii wana sifa zifuatazo:

Wanakuletea ishara kwamba wameona au kunusa kitu mahali.

Wanafanya upekuzi katika mtindo wa "zigzag" huku wakinusa kila itu baada ya kunusishwa ile sample ya scent ya kitu au mtu.

Wakigundua kitu hutikisa mkia na kutulia mahali hapo mpaka mwongozaji awasili mahali hapo.

Wana uwezo wa kufuatilia ishara za mikono wapi inawaelekeza.

Wanaishi miaka 12 mpaka 14.

Napenda kuona kila mtu anapata wito wa kumtafuta bwana Balali na aje ajibu tuhuma.

Vinginevyo tunao Springer Spaniels!
 
Jamani wacheni story za uzushi, Balali yupo safi na anadunda hapa US. Kuna source zangu zinasema alikuwa kwenye condo yake huko Boston, kabla ya kwenda zake DC. Balali hajafa and i think its not fair kusema mambo yasio na evidence.

Kama amekufa please tuonyesheni evidence, picha za msiba, cheti cha kifo, anything kuprove the point. Other than that i think hili lina sound more Kasheshe au Udaku.

Nakubaliana na wewe 100% Mtanganyika. Sidhani kuwa ni jambo jema kuzusha habari zisizo na ukweli uliothibitishwa. Hata kama Balali anasemekana kuhusishwa na upotevu wa fedha za Watanzania. Ni vyema tuseme ukweli kila inapowezekana. Ukweli utasaidia kutoa elimu bora kwa wanaosoma habari hizi.

Ikiwa yuko hai, ni vyema serikali ifanye kila linalowezekana ili arudishwe Tanzania na kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili. Ukimya utazaa mazoea. Watazuka wengine watakaoiba fedha zetu na kukimbilia mataifa mengine kujificha. Ni lazima fundisho la kudumu litolewe, na litolewe mapema.
 
Hivi Balali Amekuwa Kama Osama Bin Laden, Walioko Iringa Waende Mafinga Kwenye Mashamba Ya Chai, Kuna Wadogo Zake Manamba Kule Wanaweza Kutuletea Nyeti, Manake Huyu Bwana Aliletwa Kama Tx Kutokea Huko States Kuja Kuwa Gavana, Kalammba Michuzi Na Kurudi States Hakuwahi Hata Kwenda Home Mafinga!!!!
 
balali ni muujiza wa mungu, mtu hai aliyekuwa kafa. anasiyejuulikana wapi alipo lakini akitakiwa atapatikana upesi, anayehusika moja kwa moja kwenye ufisadi lakini asiyehitajika kwenye uchunguzi wa EPA.
huyu ni miuzija ya mungu
 
kama Balali alinyamzishwa kusema ukweli Tanzania kwa nini asiuseme sasa hivi? itamchukua dakika ngapi kujirecord akizungumzia kila kitu na kupost video youtube? Hapa Balali naye sio muungwana na hana uchungu na anachozushiwa uko Tanzania.

Heshima Mkuu. Tangu lini Balali alikuwa MUUNGWANA na ana UCHUNGU wa Tanzania. Balali ni FISADI period, hakuna cha uchungu wala utamu......... ni FISADI PERIOD
 
Yaani Osama Bin Laden alipozuliwa kuwa amekufa kwa sababu ya matatizo ya figo.. guess aliamua kufanya nini? Binafsi niko tayari kutembelea aliko Balali na kutoa habari kama nimekuta lundo la mchanga au ni mzima...

Vinginevyo, naamini Balali hayupo hai, na serikali haijui cha kuwaambia Watanzania kwa sababu hawajui waliko.
 
Labda kwa kumzushia namna hii inaweza kuwasaidia wakawa a bit serious hawa akina Pinda. Lakini sina uhakika kama uzushi huu ni haki kwa familia ya Balal. Nafikiri ni mateso zaidi![/SIZE]



You are right Kitila.

Sometimes we need to admit kwamba tumekuwa selfish, we do not care msg zetu zitaumiza vipi watu baki kama ndugu, jamaa na wengineo walio attached na yeye (Balali).

Let us put ourselves into their shoes, kwana mtu anaibuka na kudai Baba, Mama, rafiki ama ndugu yako AKEKUFA, na hali ww unajua yupo hai!, I mean it really hurt.

Hizi siasa na mambo ya serikali sio wote tunayajua (Especially me), labda they have their own way in dealing with this issue, kwa siri kubwa, na vile hawataki siri ivuje, then no need telling us wamefikia wapi katika upelelezi or whatever you call it, na vile hawataki kudisclose how they deal with the issue, they can say anything kuepuka maswali, like hatujui alipo and stuffs like that.

Bado hainiingii akilini kwamba serikali haijui Balali alipo, never jamani. Wanajua zaidi ya tunavyofikiria. But the question is do they need to disclose his whereabout and how they are dealing with the matter? Will it help us tukijua yupo sehemu flani? Wangapi tunajua walipo, na tunawaona kila siku wenye issue kama zake and we kama wananchi, have done nothing?

Huu uhuru wa kuongea sasa duh, haya bwana......................BALALI ALISHAKUFA HATUKUAMBIWA.
 
Hapana... ndugu za Osama wanajisikiaje mtoto, baba, na kaka yao anapoimbwa kuwa Ghaidi?

Kila mtu anabeba mzigo wake mwenyewe na kama Balali anaona kuwa haya yanaumiza familia (kitu ambacho naamini familia zinaumia) ana uwezo wa kufanya alichofanya Chenge kutuliza mioyo ya watu.

Ukiangalia mimi sijasema ajitokeze kusema kuhusu EPA au Benki Kuu, nimesema kama kweli yupo hai basi afanye kitu angalau tujue kuwa yu hai; Ndugu zangu na familia wanaweza kusaidia kwa kumpiga picha na gazeti la leo leo ili kuonesha kuwa ni mzima. Vinginevyo, maumivu ya hisia ni sehemu moja ya maisha yetu kama wanadamu, na hatuwezi kuacha kusema, au kufanya mambo fulani kwa sababu tutaumiza watu hisia.

Hisia zilizoimizwa za Watanzania kuhusu nchi yao ni nani anawajibika kutuponya?
 
Back
Top Bottom