KakindoMaster
JF-Expert Member
- Dec 5, 2006
- 1,356
- 88
Mkuu MKJJ,
Yaani hapo umechokonoa penyewe kabisa...bado kuongezea kachumvi na pilipili tu pakianza kuwasha watasema wenyewe...wametugeuza kama vinyamkera wao kuwa mtu wao haalafu hawajui aliko....Lazima watakuwa hamnazo kabisa si bure..
Balali lina kula kuku wake Argentina,hajafa wala nini,mmelala sana wabongo.
Kwa uhakika kwa kutumia mantinki ya kikawaida tu, akili haikubali kwamba kwa mtu ambaye SERIKALI inamtuhumu kwa hujuma kubwa na nzito kama hizo, eti mpaka sasa wanapata hata nguvu za kutuambia hawajui alipo. Akili hata ile ya kawaida haikubaliani na ukweli kama huu. Nadhani labda kwa kujiuliza kwako huko mwanakijiji, inawezekana akili ikatengeneza mantiki kidogo. Lakini tuna jadi ya marehemu..bila ya kujali alikufa katika hali gani..kumuenzi kitaifa..labda tungeona taifa likienzi mazishi au msiba wa mtu huyu. Inatatiza kichwa!!Mkandara, ni katika kufuatilia habari ambazo zimekuwa zikiminywa kwa muda mrefu; katika kujiuliza uliza ndiko nimehitimisha kuwa Balali alishakufa, kwani ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa haiwezekani akawa hai; tatizo ni kuupata mwili.
Balali hana haja ya kufanya hivyo,why?wake yeye anajipumzisha na mijipesa yake?Why aanze malumbano ya mimi na wewe?Hivi kwa hatua aliyokuwa amefikia balali kwa kutosikika mpaka sasa, na jinsi alivyokuwa kuwa anapenda kutoa ushirikiano na waandishi wa habari mbali mbali na kwa maswala yaliyotokea tangia alipo ugua kweli mtu akisema sasa amekufa mimi sioni cha ajabu hata kidogo.
Huyu bwana anajua kujieleza sana ni either alipokuwa anaumwa ndo basi ilitoka au kuna kikubwa kilicho msibu zaidi ya tunayoyaona. Nafikiri Balali atakuwa na Mtandao, kwa hizi post karibia 70 ambazo bado zinatafuta zinamtafuta huku na huko kama kweli ni mzima angalau arushe tu neno BBC au chombo chochote cha habari vinginevyo tukubaliane kuwa ndo yamekwisha.
Balali hana haja ya kufanya hivyo,why?wake yeye anajipumzisha na mijipesa yake?Why aanze malumbano ya mimi na wewe?