Balcony inachukua nafasi kubwa ya eneo, unaweza kujenga ghorofa bila balcony

Balcony inachukua nafasi kubwa ya eneo, unaweza kujenga ghorofa bila balcony

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nimeona hii nyumba na kutafakari. Kwa wale wapenzi wa ghorofahii ni plan ni ya bei nafuu. Juu Ina vyumba vitatu vya kulala a family bathroom.

Chini ina jiko, choo, sebule na dining. Katika kiwanja cha kawaida cha 1/4 eka unaweza kujenga hii nyumba na nyuma ukapata nafasi ya banda la kuku 200.

Ulishawahi kuwaza kujenga nyumba bila balcony

1610423738815.png
 
Raha ya ghorofa ni balcony bwana, majirani watajuaje una ghorofa bila balcony!?
Wengine wanapenda ghorofa kwakuwa wageni si rahisi kupanda juu na family inakua na privacy.
 
Hiyo ni plan ya nyumba za nchi za baridi.

Kule balcony ni kujitesa, balcony ya nini wakati kuna baridi ya kuua mtu.

Njoo bongo bwana, upepo mwanana, bila balcony hujafaidi breeze ya the Indian Ocean.
 
Hiyo ni plan ya nyumba za nchi za baridi.
Kule balcony ni kujitesa, balcony ya nini wakati kuna baridi ya kuua mtu.
Njoo bongo bwana, upepo mwanana, bila balcony hujafaidi breeze ya the Indian Ocean.
Lakini kutoweka balcony unaokoa pesa nyingi pia eneo.
 
Hio balcony inachukua nafasi gani kwenye hio 1/4 eka kiasi cha kushindwa kuiweka kwenye ramani? Halafu balcony si iko ghorofa ya juu sasa inamalizaje nafasi?
 
Lakini kutoweka balcony unaokoa pesa nyingi pia eneo.
Balcony inakaa juu inamaliza eneo gani?

Balcony inaokoa pesa nyingi kwa bajeti ya ghorofa? Balcony inaweza kuwa within footprint ya jengo, kuta za chumba/vyumba zinaingia ndani tu.
 
Hio balcony inachukua nafasi gani kwenye hio 1/4 eka kiasi cha kushindwa kuiweka kwenye ramani? Halafu balcony si iko ghorofa ya juu sasa inamalizaje nafasi?
Katika ramani hii, ilipo sebule chini juu ni chumba cha kulala sasa balcony ingekuwa ni extension.
 
Lakini kutoweka balcony unaokoa pesa nyingi pia eneo.
Ni kweli lakini ukiwa na nafasi lazima kuishi kwenye nyumba in style.
Enzi za baba zetu nyumba zilikuwa NHC style, korido kati na vyumba kila upande(Temeke, Ilaka, Magomeni)

Baadaye zikaja Sinza style(Sinza, Tabata)

Zikaja nyumba balcony za mlango mmoja na dirisha.

Sasa hivi vijana ni balaa!
Bacony with a covered patio(Mbweni,Mbezi Beach)

Hata hivyo nyumba zinaendana na wakati.
 
Dada unajenga vipi ghorofa bila balcony? Yaani ushindwe kuangalia mandhari ya nje ukiwa nje na kupunga upepo? Wengine hufanya hadi sherehe hapo kwenye balcony
Pia nyumba bila balcony haiwezi kuonekana nzuri
 
Nyumba za kizamani za Europe hizo. Ghorofa bila balcony ni bure kabisa. Aidha umuhimu wake ni katika kufanya Usafi na Maintanance
 
Katika ramani hii, ilipo sebule chini juu ni chumba cha kulala sasa balcony ingekuwa ni extension.
Ramani za kwenye baridi, tangu awali hawakuplan balcony. Wangetaka ingepatikana bila extension.
 
Dada unajenga vipi ghorofa bila balcony? Yaan ushindwe kuangalia mandhari ya nje ukiwa nje n kupunga upepo? Wengine hufanya hadi sherehe hapo kwenye balcony
Pia nyumba bila balcony haiwezi kuonekana nzuri
Maintain eye gani hapa kama ni kusafisha madirisha kwa nje unapanda na tractor la Kijiko.
 
Maintain eye gani hapa kama ni kusafisha madirisha kwa nje unapanda na tractor la Kijiko.
Gharama ya kukodi kijiko kwa siku ni 700,000/- bado hujamlipa Operator kwa siku 50,000/- yote ya nini kwanini usiweke balcony sasa
Kingine Tanzania bado tuna ardhi kubwa sana sioni haja ya kubana hizo nafasi
 
Wapo wasafisha madirisha unawakodi. Wana vifaa maalum.
Sawa ndugu unajua michango ya watu wengi humu kila mtu anachangia kutokana na maisha yake ndio maana mimi naweza kujiuliza mara zote za kufanya usafi atakuwa na pesa? Hii yote niumasikini wetu.
 
Back
Top Bottom