Zipo faida na hasara za kukopa WB na IMF na pia kukopa benk binafsi.
Of course, kila jambo lina faida na hasara zake...
Muhimu ni mizania!!
Hasara ya kukopa WB na IMF nikiwa wakopeshaji hawa wanakupangia fedha walizokukopesha uzitumieje na kuchunguza sana masharti wanayokupa ukiyafuata kama yalivyo huo mradi uliopanga kuutekeleza kwa fedha hizo hautakaa uje kukuletea tija. Kibaya zaidi uambatanisha na masharti ambayo hayahusu financial issues kwa nchi mkopaji. Mifano ipo. Riba inasemwa ni ndogo hatuelezwi udogo wake.
Mkuu TUJITEGEMEE... hiyo sio hasara bali ni faida!!!
From my experience working in financial sector, moja ya sababu inayofanya wafanyabiashara wengi ku-default ni kuelekeza mikopo "sekta" tofauti na ile uliyokopea...
As a private enterprise, ukienda benki kukopa lazima utawasilisha mchanganuo wako wa kibiashara!! Merits za mkopo uliopewa itatokana na loan appraisal uliyowaisilisha!!
Sasa ni kawaida sana unakuta Mfanyabiashara anapeleka mchanganuo wa biashara ya mahindi, akipata pesa anawekeza kwenye mpunga! Wengi huwa wana-default kwa ujinga huu!!
Tukija at a state level!!
Miradi mingi huwa inakwama kwa sababu ya kukosa close monitoring na mischannelling of loan funds!!! IMF lazima wahakikishe hakuna mischannelling kwa sababu mkopo ukishindwa kufikia malengo, hawana chochote cha kukufanya! Sana sana wataacha tu kukukopesha!!
On the otherhand, at a state level, benki binafsi wala hawana haja ya kukufuatilia unatumia vipi... kwanza hiyo jurisdiction wataitoa wapi! Lakini kubwa zaidi, wao wanachojali ni kurudi kwa pesa zao, na riba juu! Na wapo tayari kutoa hadi rushwa kuhakikisha wanakukopesha kwa saabbu serikali, hususani yenye resources and stability, ni less risk!!
They don't care kama umejenga hayo mashule au hapana kwa sababu it's none of their concerns!! Hawa kazi yao sio "elimu kwa wote" au "afya kwa wote" kama unavyoweza kukutana nayo hayo IMF... they're strictly FOR BUSINESS that turns into PROFIT...
Hasara ya kukopa benki binafsi nikuwa riba yao nikubwa ingawa hatuelezwi ukubwa wa riba hiyo. Mikopo ya hawa jamaa haina masharti zaidi ya kuelekezwa ulipe deni kwa wakati. Mifano ipo
Haina masharti kama you've something to offer kama nilivyosema hapo juu!!
Hawa hawawezi kukupa masharti sijui ya Utawala Bora, mara social liberty n.k lakini watakupa masharti ambayo purely ni commercial... na kubwa zaidi uwezo wa serikali husika kuweza kurejesha!! Kwa nchi yenye raslimali kama hii, wanajua hata usipolipa leo, utalipa kesho au hata mwakani! Kadri unavyochelewa, kwao ni faida kwa sababu riba inaongezeka!!!
Nadhani umeshasikia sana suala la Bandari ya Hambantota... maarufu kama Bandari ya Sri Lanka!!!
Serikali ilifikia uamuzi wa kuuza hisa za ile bandari baada ya kuona deni linaendelea ku-accumulate kila uchao... kutokana na riba!!
Sina hakika mkuu wangu, Chige hauyajui haya.
Nafahamu sanan
Pitia peer reviewed article hii inayofafanua vizuri hasara ya kutumia wb na imf.
Nikipata muda nitapitia lakini nikujuze tu kwamba, kwa yeyote aliyesoma uchumi at university level, anafahamu vema masuala ya Structural Adjustment Program kwa sababu tumesoma sana hayo!!!
Lakini labda nikung'ata sikio...
Structural Adjustment Programs sio mbaya kihivyo kama ambavyo watetezi wa serikali za kiafrika wanavyojaribu kuaminisha watu...
Hata hapa tulipofikia, ni matokeo ya Structural Adjustment Program, ingawaje ni kweli pia yapo maeneo ambayo hatukufanya vizuri!!
Of course, kuna mambo mengine am