Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Zuzu mwingine (in Assad voice).

Hivi unadhani mabeberu ata kwa kupitia private banks yanakopesha nchi maskini bila ya IMF na WB kufanya stress test kama unaweza kulipa madeni yako huko mbele based on your tax collections.
Kwa nini mnalazimisha mtu atawale kama Magu? Nyie jamaa vipi? Unadhani walioweka ukomo wa uongozi ni wajinga? Miaka yako 10 tawala vile unaamini, ikiisha unapisha mwingine atawale anavyoamini, mazuri yako atayaendeleza and mabaya yatapigwa chini, na itaendelea hivyo!!

Samia siyo Magu na hawezi kutawala kama Magu, huo ndiyo ukweli!! Na baada ya Samia atakuja mwingine naye hatatawala kama Samia!! Huu upuuzi wenu wa kumgeuza Magu SI Unit ya kutawala TZ hakuna ataufuata!! Kwanza bora hata ya Samia anajitahidi kuendeleza mamiradi hewa ya Magu, Magu yeye kutwa alikuwa anapita kuwatukana watangulizi wake...
 
And alikuwa anakopa kwa siri as if hiyo hela angelipa kutoka mifukoni mwake, akiwa majukwaani anawatukana mabeberu, Usiku anawapigia simu kuwakopa hela!! Trl 29 kwa miaka 5 ni nyingi sana, and sijui kafanyia nini hiyo hela, maana mamiradi yake yote yapo under 50% ya utekelezaji
Mkuu 50% ya project ni kubwa! Sema unachuki na JPM ndo maana hauoni alichofanya JPM hakujipendekeza kwao walikuja wenyewe baada ya kuona mziki wake! Angalia project kama zifuatazo
•Tanzania haikuwahi kuw ana Radar tokea uhuru amejenga nne kwa mkupuo Dar,mwanza,mbeya na klimanjaro
•Tanzania haikuwahi kuwa na Mahakama zakisasa tokea uhuru mahakama standard zilikuwa ni zile za kanda! Leo tunazungumzia mahaka zenye miundombinu ya kisasa!
•Nchi hii ilikuwa na hospital kubwa za kanda nyinhi za mashirika ya dini leo hii tuna hospital kubwa za hadhi ya kitaifa kule Musoma, mtwara,mbeya n.k Wao waliopita hawakufanya haya si kwa kuwa hawakuweza tu bali hata utendaji wao haukuwa katika viwango vya JPM!
•Vituo vya afya,hospital za wilaya, masoko.
•Uanzishwaji wa masoko ya madini mfano soko la dhahabu Geita limeinbiza takribani trilion tatu kwa miaka miwili na nusu!
•Upanuzi wa bandari hapo Dar, mtwara ma tanga!
•Ufufuami wa treni kutokea Dar mpaka moshi/arusha!
•Ujenzi wa flyover,busisi,mto wami n.k

Hayo ni ambo yanahitami usimamizi na fedha kwa hiyo kama matokeo yanaonekana kukopa kwake hakuna shida! Hata nyumbani kwako ukikopa benki ili ujenge nyumba na ukajenga kwa ubora na ikaonekana hakuna mtu atakaye kulaum! Ila kwa vile mmezoea maneno sio utendaji endeleeni kumsifia huyu mama ambaye hana hata historia ya utendaji kwenye maisha yake, kitu pekee kimemfikisha hapo ni kubebwa na siasa!
 
Kwa nini mnalazimisha mtu atawale kama Magu? Nyie jamaa vipi? Unadhani walioweka ukomo wa uongozi ni wajinga? Miaka yako 10 tawala vile unaamini, ikiisha unapisha mwingine atawale anavyoamini, mazuri yako atayaendeleza and mabaya yatapigwa chini, na itaendelea hivyo!! Samia siyo Magu na hawezi kutawala kama Magu, huo ndiyo ukweli!! Na baada ya Samia atakuja mwingine naye hatatawala kama Samia!! Huu upuuzi wenu wa kumgeuza Magu SI Unit ya kutawala TZ hakuna ataufuata!! Kwanza bora hata ya Samia anajitahidi kuendeleza mamiradi hewa ya Magu, Magu yeye kutwa alikuwa anapita kuwatukana watangulizi wake...
Sema mradi hewa ni upi? Kama ni hewa si aufute! Uwezo wake mdogo!
 
Ni swala la muda tutajua ukweli. Ila mtoa mada be fair usilete hoja zisizo na mashiko. Hata wakati JPM nchi ilipopokea mkopo ilikuwa ikitangazwa. Pili Deni aliliorithi JPM lilikuwa kwa kasi sana maana lilikuwa limeiva JPM focus ilikuwa si kulipa deni kwanza bali ilikuwa ni kujenga uwezo wa ndani ilituweze kulipa madeni. Miundombinu ilijengwa ililenga kukuza uchumi wa taifa ili siku zijazo liwe na uwezo kulipa madeni yake. Kumbuka Kenya walipofikia yaani wanakopa hela ili kulipa deni.
 
Mpumbavu sana huyo achana naye, yaani jf bado kuna wajinga kama hawa kweli? Jitu halijui kuwa ukichukua mkopo hiyo hela ni yako maana umeamua kuitumia mapema tu!
Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
 
Ni aheri deni lipae ila vitu viwe vinaonekana wazi, hebu tunakanyaga lami za kueleweka na barabara za kiwango cha zege mpaka mitaani! Wakati unalalamika kutendwa na Magufuli mkoonduh wako unapepea kuelekea ulipojenga Mbezi Kibanda Cha mkaa kupitia barabara 8 za lami huku ukipaa toka kwenye kijazi interchange.

Je, unakumbuka ni kero kiasi gani ulizipata kwa kukaa masaa zaidi ya 2 kuvuka tu eneo la Ubungo maziwa mpaka ubungo maji tokana na msuko suko wa magari?
 
Ni swala la muda tutajua ukweli. Ila mtoa mada be fair usilete hoja zisizo na mashiko. Hata wakati JPM nchi ilipopokea mkopo ilikuwa ikitangazwa. Pili Deni aliliorithi JPM lilikuwa kwa kasi sana maana lilikuwa limeiva JPM focus ilikuwa si kulipa deni kwanza bali ilikuwa ni kujenga uwezo wa ndani ilituweze kulipa madeni. Miundombinu ilijengwa ililenga kukuza uchumi wa taifa ili siku zijazo liwe na uwezo kulipa madeni yake. Kumbuka Kenya walipofikia yaani wanakopa hela ili kulipa deni.
Halafu hajasema kuwa deni la Kikwete na Mkapa kuiva kwake kunachangia kiasi gani kwenye hizo 78.2T.

Halafu eti yeye ndiye kasababisha Samia kuapishwa Qyummae zake huyu mbwa kasoro mkia!
 
Hamna nchi isiyokopa wewe, na hamna anayechezea fedha, acha kuamini hizo stories zenu za vijiweni na chuki za kijinga! And kama wewe kwenye familia yako unategemea kipato kimoja tu kuiendesha basi wewe ni wa hovyo kabisa
Sijui unapinga nini naona unapiga kelele tu hapa, unalia Magufuli kukopa ila nyie kwenu kukopa ni kawaida, na kama humuoni anayechezea fedha ni uamuzi wako kwa mahaba yako ila mimi namuona.

Kwangu bora aliekopa kujenga SGR na Stiglers Gorge kuliko nyie mnaokopa kujenga madarasa ambayo fedha zake tunakatwa kila siku kwenye miamala ya simu, akili zenu mgando sana.
 
Mkuu 50% ya project ni kubwa! Sema unachuki na JPM ndo maana hauoni alichofanya JPM hakujipendekeza kwao walikuja wenyewe baada ya kuona mziki wake! Angalia project kama zifuatazo
Hivyo vitu vimefanyika, ni sawa, and huyu aliyeingia anaendelea navyo kwa speed ambayo naweza sema inaizidi ya huyo jamaa yako! Kipimo pekee cha kuonekana mtendaji TZ ni kuwa mpiga kelele mbele ya macamera na vitisho vya kindezi (Leo hii ndiyo kipimo hicho kinatumika eti kusema Jokate ndiyo DC jembe anastahili uRC!!!), ndiyo kipimo alichopimiwa Makonda, Sabaya, Magu, A.Mrema na watu wa aina hiyo!!

Mother siyo mtu wa makeke, kwa standards za TZ mtu wa hivyo kwao ni dhaifu, siyo Mtendaji! Kuhusu kubebwa, Mtu kawa mbunge, waziri serikali ya mapinduzi, waziri serikali ya muungano, makamu mwenyekiti bunge la katiba, kateuliwa kuwa mgombea mwenza 2 times na huyo jamaa yako and wewe unasema anabebwa na siyo mtendaji!!!!!!!!

TZ tuna udhaifu wa kuchukulia vitu poa sana, kwenye ukoo wako sidhani kama kuna mtu amewahi kulamba hata ubunge!!! Samia atatawala kama Samia, na JPM siyo SI Unit ya uongozi TZ
 
Kwa hiyo Balile anataka kuuaminisha umma kuwa asingeandika andiko lake Samia asingeapishwa? Nshomile kwa sifa jamani! Suala la Kikatiba liwe influenced na andiko la Balile! Kwenye madeni hapo sawa, lkn kwenye uapisho wa Mama Samia, huna chochote kushupaza shingo mtani, huusiki kwa lolote deogratius Balile
 
Ni aheri deni lipae ila vitu viwe vinaonekana wazi, hebu tunakanyaga lami za kueleweka na barabara za kiwango cha zege mpaka mitaani! Wakati unalalamika kutendwa na Magufuli mkoonduh wako unapepea kuelekea ulipojenga Mbezi Kibanda Cha mkaa kupitia barabara 6 za lami huku ukipaa toka kwenye kijazi interchange.

Je, unakumbuka ni kero kiasi gani ulizipata kwa kukaa masaa zaidi ya 2 kuvuka tu eneo la Ubungo maziwa mpaka ubungo maji tokana na msuko suko wa magari?
Mkuu hawa watu ni wapumbavu sana! JPM hata hizi barabra wakati wa Kikwete kapambana sana kusimamia! Lakini ukiangali mitaa hata Dar huko temeke,buza,arusha, mwanza maeneo kama mitaa ya rufiki na mjini kati kule mwanza hapakuwa na rami! Huyu Balile nakuja kutuletea promo hapa! Bababara kutokea kibaha mpaka kimara ingekuwa Rais dhaifu asiye na maamuzi ingekuwepo? Vipi Jam ya magari ingekuwaje? Mkopo sio shida shida ni vitendo kutoka na mkopo vinaonekana?
 
Sasa kama Hayati Magufuli alikopa sana, ni kwanini Rais wa sasa na yeye anaendelea kukopa?

Tufike pahala tuache upambe na chuki na kisha tuwe wakweli kwa maendeleo ya nchi yetu.
Nchi inamadeni alafu tunaendelea kukopa kwa kigezo kuwa deni letu ni stahimilivu!?

Tufike pahali sasa tujifunge mkanda, tuanze na kupunguza mishahara minono ya viongozi, zahara zote zisizo na tija zifutwe mfano:- Barabara imejengwa ikakamili alafu kiongozi anakwenda kuizindua kwa ziara yenye gharama kubwa.
Serikali iache kutumia magari ya gharama (V8) nk

Nina amini kama serikali itaamua kuacha matumizi ya anasa basi kwa kiasi hiki hiki ambacho kodi hukusanywa deni litalipwa.

Ila kama wananchi tutaendelea na ushabiki maandazi kwa hiki chama cha ccm basi siku moja tutajikuta nchi imeuzwa.
 
Sema mradi hewa ni upi? Kama ni hewa si aufute! Uwezo wake mdogo!
Afute miradi ambayo jamaa yako alishatufunga kwenye mikataba ya hovyo? Unadhani yeye ni kama jamaa yako ambaye alikuwa anafuta tu miradi ili apate masifa jukwaani mwisho wa siku ikawa inatucost kama taifa? Makesi mangapi tumegaragazwa enzi za utawala wake sababu ya maamuzi yake ya kindezi na masifa ya kijinga?

Ndege zetu zilikamatwa na kuliletea aibu taifa sababu kubwa si ilikuwa maamuzi yake ya kutotumia akili? kifupi system ilishamchoka na ndiyo maana........Uwezo wa Mother ni mkubwa mnoo, mtu anayejiamini hanaga makeke, ukiona mtu makelele mengi, kugawa gawa mahela hovyo barabarani, kununua jogoo kwa laki moja ili kufurahisha watu ujue hamna kitu huyooo, empty head
 
Hivyo vitu vimefanyika, ni sawa, and huyu aliyeingia anaendelea navyo kwa speed ambayo naweza sema inaizidi ya huyo jamaa yako! Kipimo pekee cha kuonekana mtendaji TZ ni kuwa mpiga kelele mbele ya macamera na vitisho vya kindezi (Leo hii ndiyo kipimo hicho kinatumika eti kusema Jokate ndiyo DC jembe anastahili uRC!!!), ndiyo kipimo alichopimiwa Makonda, Sabaya, Magu, A.Mrema na watu wa aina hiyo!! Mother siyo mtu wa makeke, kwa standards za TZ mtu wa hivyo kwao ni dhaifu, siyo Mtendaji! Kuhusu kubebwa, Mtu kawa mbunge, waziri serikali ya mapinduzi, waziri serikali ya muungano, makamu mwenyekiti bunge la katiba, kateuliwa kuwa mgombea mwenza 2 times na huyo jamaa yako and wewe unasema anabebwa na siyo mtendaji!!!!!!!! TZ tuna udhaifu wa kuchukulia vitu poa sana, kwenye ukoo wako sidhani kama kuna mtu amewahi kulamba hata ubunge!!! Samia atatawala kama Samia, na JPM siyo SI Unit ya uongozi TZ
Unataka kutuaminisha utendaji wa mama kwenye kusimamia miradi unalinganisha na JPM! Unajua unajichanganya sana huku ukweli unaujua! Mimi sitaki kubishana projo! Unataka kujua kwenye ukoo wetu kuna hata mtu alishawahi kuwa mbunge? Hivi unataka kutuaminisha hapa kuwa koo zote Tanzania zilishatoa wabunge?

Au wewe na familia yako ndo mmetoa wabunge wanaoitwa MAZUZU! Kijana tafuta maisha na usipende kuchukia ukweli utapata matatizo ya moyo! Unamnanga JPM huku unajua ukweli kuwa alikuwa mchapaka kazi hodari tokea utotoni mpaka mautini hata Mbowe wako gaidi analijua hilo na alikili.
 
Kwa nini mnalazimisha mtu atawale kama Magu? Nyie jamaa vipi? Unadhani walioweka ukomo wa uongozi ni wajinga? Miaka yako 10 tawala vile unaamini, ikiisha unapisha mwingine atawale anavyoamini, mazuri yako atayaendeleza and mabaya yatapigwa chini, na itaendelea hivyo!! Samia siyo Magu na hawezi kutawala kama Magu, huo ndiyo ukweli!! Na baada ya Samia atakuja mwingine naye hatatawala kama Samia!! Huu upuuzi wenu wa kumgeuza Magu SI Unit ya kutawala TZ hakuna ataufuata!! Kwanza bora hata ya Samia anajitahidi kuendeleza mamiradi hewa ya Magu, Magu yeye kutwa alikuwa anapita kuwatukana watangulizi wake...
Samia ni Samia; na Magufuli ni Magufuli. Hakuna mtu anataka watu wawili wafanane.

Alikadhalika uongozi ni kanuni ndio maana kuna specific leadership styles zinazofundishwa. Some styles are more effective in one area or a society than in another.

Kwa nchi yetu ukicheka na nyani utavuna mabua, so badala ya kusema mama awe semi autocrat and having a flat structure ili awe anaona kila waziri wake anafanya nini; ndio namna nyingine ya kusema harudi kuisimamia nchi kwa mtindo wa Magufuli.

Atujafikia bado utawala wa laissez faire kiongozi kuwaacha watu wachini waendeshe, wizara, taasisi, mikoa, and so forth with so much freedom. Tushaona aina hiyo ya uongozi katika miaka ya JK sio kila ufisadi ulikuwa na baraka zake isipokuwa his eyes were not on the ball yeye kutwa yupo angani.

Na hili lishaanza kurudi tena, JM ameonyesha mapema sans nishati sio size yake maamuzi aliyochukua ya awali na strategy yake ya green technology anayo pursue kwa nguvu zote( will become costly to the nation is so many areas. Watch this space wala sio majungu.

Tanzania ni nchi ambayo inahitaji attitude change kuanzia viongozi wanavyojitambulisha (most of them tend to think they are special), wananchi kuelewa wajibu wao, serikali kuelewa wajibu wake na kila kitu kinachohusiana na binadamu; na kuwabadili watu tabia na fikra zao sio kazi rahisi popote duniani.

Mfano mwingine ni huu majungu lengo la hii mada ni self defence; sitoshangaa soon kuona IMF wanakuja kuweka vizingiti vya kukopa mpaka mwenendo wa uchumi ubadilike na makusanyo yawe sustainable.

But then watu walishaonya usibadili mtindo wa TRA kuna mapungufu madogo madogo ila kwa asilimia kubwa ivyo ndio namna hiko chombo kinavyotakiwa kufanya kazi kuna watu awakuzoea kulipa kodi halali huko nyuma ndio msingi wa kelele.
 
And alikuwa anakopa kwa siri as if hiyo hela angelipa kutoka mifukoni mwake, akiwa majukwaani anawatukana mabeberu, Usiku anawapigia simu kuwakopa hela!! Trl 29 kwa miaka 5 ni nyingi sana, and sijui kafanyia nini hiyo hela, maana mamiradi yake yote yapo under 50% ya utekelezaji
Ilikuwa ni siri kwako.

Kama unasubiri kila kitu kutafuniwa na kina Lisu hakika hungeweza kujua
 
Meko alikopa mikopo ya hovyo, fullstop!! Mikopo nafuu waliyokopa wenzie kabla yake, na anayokopa Mama sasa alinyimwa kutokana na udikteta wake uchwara!! Trl 29 kwa miaka 5, tena mikopo ya biashara, thats insane!! Huyo Meko wako ndiyo alikuwa hakopesheki mikopo nafuu
Mikopo nafuu kama ipi?
 
Mkuu hawa watu ni wapumbavu sana! JPM hata hizi barabra wakati wa Kikwete kapambana sana kusimamia! Lakini ukiangali mitaa hata Dar huko temeke,buza,arusha, mwanza maeneo kama mitaa ya rufiki na mjini kati kule mwanza hapakuwa na rami! Huyu Balile nakuja kutuletea promo hapa! Bababara kutokea kibaha mpaka kimara ingekuwa Rais dhaifu asiye na maamuzi ingekuwepo? Vipi Jam ya magari ingekuwaje? Mkopo sio shida shida ni vitendo kutoka na mkopo vinaonekana?
Sahizi tunaambiwa mikopo itajenga madarasa na zahanati! At the same time, tozo zitajenga shule na zahanati ili watoto wetu wasome WTF!?

Yani mikopo yote mpaka ya COviD 19 ni ya kujengea tu! Bado ameweka wapigaji kwenye system bila kujielewa yani! Wacha tuone huko Tanesco baada ya kuanza kukaribisha wawekezaji uchwara kipigo kitakuwaje
 
Back
Top Bottom