Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Kwa nini mnalazimisha mtu atawale kama Magu? Nyie jamaa vipi? Unadhani walioweka ukomo wa uongozi ni wajinga? Miaka yako 10 tawala vile unaamini, ikiisha unapisha mwingine atawale anavyoamini, mazuri yako atayaendeleza and mabaya yatapigwa chini, na itaendelea hivyo!! Samia siyo Magu na hawezi kutawala kama Magu, huo ndiyo ukweli!! Na baada ya Samia atakuja mwingine naye hatatawala kama Samia!! Huu upuuzi wenu wa kumgeuza Magu SI Unit ya kutawala TZ hakuna ataufuata!! Kwanza bora hata ya Samia anajitahidi kuendeleza mamiradi hewa ya Magu, Magu yeye kutwa alikuwa anapita kuwatukana watangulizi wake...
Yani ni miradi hewa ila anaiendeleza?

Ujinga mzigo
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje? Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki? Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.
Watu wengine wajinga Sana mkuu anadhani anadanganya watoto tofauti ya Deni hili na Yale anayodhani yalikuwa madogo Ni fedha ilitumika kufanyia Nini, Kuna wakati tulifika mahali tukawa tunakopa ili kulipa mishahara. Kwa ujumla bin adamu Hana shukurani.
 
Swali pesa zimetumika kinyume na matumizi au vitu vinaonekana nafikiri hata wewe mwandishi umekiri vitu vilifanyika ila hasira zako ni kuwa hukuambiwa ukweli kama ni mkopo!
 
Halafu hajasema kuwa deni la Kikwete na Mkapa kuiva kwake kunachangia kiasi gani kwenye hizo 78.2T.

Halafu eti yeye ndiye kasababisha Samia kuapishwa Qyummae zake huyu mbwa kasoro mkia!
Kuiva kwa deni maana yake muda wa kuanza kulipa deni lako na riba yake umefika. Haimaanishi kuwa hilo sasa ni deni jipya on top of that.

Na tunapocalculate deni la Taifa maana yake vitu vyote hivyo unavyovisema tumeshaviinclude ndani yake.

Kwa hiyo ukiambiwa mwaka 2005 Kikwete alikuta deni la Trillion 20, basi hilo ndo deni alilolikuta, akizembea kulipa linajiaccumulate, na hiyo accumulation inaongezwa kwenye deni, na kile atajachokopa yeye nacho kinaongezwa kwenye deni.

Kwa hiyo kama Magufuli alikuta deni la Trillion 42 mwaka 2015, basi ndo deni hilo alilokuta limeshainclude vyote (riba na mkopo wa JK), Sasa na yeye Magufuli kaavha deni la Trillion 70, maana yake kaongeza Trilion zake za kutosha tu kwenye deni alilokuta. Yeye kama rais ilibidi Alipe, hakuna excuse kuwa ni madeni ya watangulizi wangu. Kwani Mkapa, JK hawakuwa na watangulizi?, Mbona wao rate ya ukuaji wa deni haikuwa kama ya Magufuli?
 
Unataka kutuaminisha utendaji wa mama kwenye kusimamia miradi unalinganisha na JPM! Unajua unajichanganya sana huku ukweli unaujua! Mimi sitaki kubishana projo! Unataka kujua kwenye ukoo wetu kuna hata mtu alishawahi kuwa mbunge? Hivi unataka kutuaminisha hapa kuwa koo zote Tanzania zilishatoa wabunge? Au wewe na familia yako ndo mmetoa wabunge wanaoitwa MAZUZU! Kijana tafuta maisha na usipende kuchukia ukweli utapata matatizo ya moyo! Unamnanga JPM huku unajua ukweli kuwa alikuwa mchapaka kazi hodari tokea utotoni mpaka mautini hata Mbowe wako gaidi analijua hilo na alikili.
Ugaidi wa Mbowe unaingiaje kwenye hii mada? Inaonesha mlikuwa mnamchukia "kweri kweri" huyo Mbowe! Magufuli hajawahi kuwa mtendaji ila ni maneno mengi mdomoni na kuwafunga watu midomo wasiseme kwa kutumia mabavu!! Kifupi kichwani alikuwa empty, one man show aliyeamini yeye ni Mungu mtu!! Ila sioni kama ni afya sana kumzungumzia kwa sasa, kwani kwa kupigwa kwake tayari taifa limepona.
 
Ni aheri deni lipae ila vitu viwe vinaonekana wazi, hebu tunakanyaga lami za kueleweka na barabara za kiwango cha zege mpaka mitaani! Wakati unalalamika kutendwa na Magufuli mkoonduh wako unapepea kuelekea ulipojenga Mbezi Kibanda Cha mkaa kupitia barabara 6 za lami huku ukipaa toka kwenye kijazi interchange.

Je, unakumbuka ni kero kiasi gani ulizipata kwa kukaa masaa zaidi ya 2 kuvuka tu eneo la Ubungo maziwa mpaka ubungo maji tokana na msuko suko wa magari?
Vitu vinaonekana, kwa mfano uwanja wa ndege Chato. Ule ni bonge la mradi! 😁
 
Kwa hiyo Balile anataka kuuaminisha umma kuwa asingeandika andiko lake Samia asingeapishwa? Nshomile kwa sifa jamani! Suala la Kikatiba liwe influenced na andiko la Balile! Kwenye madeni hapo sawa, lkn kwenye uapisho wa Mama Samia, huna chochote kushupaza shingo mtani, huusiki kwa lolote deogratius Balile
Mwenda wazimu huyo!
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Zama zile ukiandika habari kama hii yatakupata mzito, hivyo Sasa ndio muda sahihi wa kuandika na hakuna tatizo kufanya hivyo.
 
Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
Barabara za mitaani ni pesa ya metropolitan project (world bank ) pesa zilisainiwa kipindi Cha Kikwete

Umeme vijijini tunachangia wananchi kwa kukatwa kwenye Luku / ila zamani ilikuwa MCC project ndio inafund.

Madaraja ya Dar Ni pesa za mjapani.
 
Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.
Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.
Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibariki Tanzania.

Copyright ©2021. Gazeti la Jamhuri
"Haya yote tunayafanya kwa fedha zetu wenyewe"

clip_now_20211009_102142.png
 
Mkuu 50% ya project ni kubwa! Sema unachuki na JPM ndo maana hauoni alichofanya JPM hakujipendekeza kwao walikuja wenyewe baada ya kuona mziki wake! Angalia project kama zifuatazo
•Tanzania haikuwahi kuw ana Radar tokea uhuru amejenga nne kwa mkupuo Dar,mwanza,mbeya na klimanjaro
•Tanzania haikuwahi kuwa na Mahakama zakisasa tokea uhuru mahakama standard zilikuwa ni zile za kanda! Leo tunazungumzia mahaka zenye miundombinu ya kisasa!
•Nchi hii ilikuwa na hospital kubwa za kanda nyinhi za mashirika ya dini leo hii tuna hospital kubwa za hadhi ya kitaifa kule Musoma, mtwara,mbeya n.k Wao waliopita hawakufanya haya si kwa kuwa hawakuweza tu bali hata utendaji wao haukuwa katika viwango vya JPM!
•Vituo vya afya,hospital za wilaya, masoko.
•Uanzishwaji wa masoko ya madini mfano soko la dhahabu Geita limeinbiza takribani trilion tatu kwa miaka miwili na nusu!
•Upanuzi wa bandari hapo Dar, mtwara ma tanga!
•Ufufuami wa treni kutokea Dar mpaka moshi/arusha!
•Ujenzi wa flyover,busisi,mto wami n.k

Hayo ni ambo yanahitami usimamizi na fedha kwa hiyo kama matokeo yanaonekana kukopa kwake hakuna shida! Hata nyumbani kwako ukikopa benki ili ujenge nyumba na ukajenga kwa ubora na ikaonekana hakuna mtu atakaye kulaum! Ila kwa vile mmezoea maneno sio utendaji endeleeni kumsifia huyu mama ambaye hana hata historia ya utendaji kwenye maisha yake, kitu pekee kimemfikisha hapo ni kubebwa na siasa!
Hizo hospital za kanda unazoengelea ulishawahi kuzitembelea au unaziona kwenye picha,
Majengo yake ni uchafu mtupu, je kuna huduma gani za maana katika majengo hayo?.

Mbona mbeya alishindwa kuifanya iwe kama Bugando,Kcmc na Muhimbili?.

Tumekulia maisha ya umaskini hivyo hudhani gorofa/jengo ndiyo kiwango cha huduma.

Jamaa vitu vyake vyote alivyovifanya uongo ulikuwa mwingi sana, wala hakuwa na uchungu na fedha ya nchi yetu bali aliangalia kuufurahisha moyo wake uliojaa maisha ya sifa.
 
Samia ni Samia; na Magufuli ni Magufuli. Hakuna mtu anataka watu wawili wafanane.

Alikadhalika uongozi ni kanuni ndio maana kuna specific leadership styles zinazofundishwa. Some styles are more effective in one area or a society than in another.

Kwa nchi yetu ukicheka na nyani utavuna mabua, so badala ya kusema mama awe semi autocrat and having a flat structure ili awe anaona kila waziri wake anafanya nini; ndio namna nyingine ya kusema harudi kuisimamia nchi kwa mtindo wa Magufuli.

Atujafikia bado utawala wa laissez faire kiongozi kuwaacha watu wachini waendeshe, wizara, taasisi, mikoa, and so forth with so much freedom. Tushaona aina hiyo ya uongozi katika miaka ya JK sio kila ufisadi ulikuwa na baraka zake isipokuwa his eyes were not on the ball yeye kutwa yupo angani.

Na hili lishaanza kurudi tena, JM ameonyesha mapema sans nishati sio size yake maamuzi aliyochukua ya awali na strategy yake ya green technology anayo pursue kwa nguvu zote( will become costly to the nation is so many areas. Watch this space wala sio majungu.

Tanzania ni nchi ambayo inahitaji attitude change kuanzia viongozi wanavyojitambulisha (most of them to think they are special), wananchi kuelewa wajibu wao, serikali kuelewa wajibu wake na kila kitu kinachohusiana na binadamu; na kuwabadili watu tabia na fikra zao sio kazi rahisi popote duniani.

Mfano mwingine ni huu majungu lengo la hii mada ni self defence; sitoshangaa soon kuona IMF wanakuja kuweka vizingiti vya kukopa mpaka mwenendo wa uchumi ubadilike na makusanyo yawe sustainable.

But then watu walishaonya usibadili mtindo wa TRA kuna mapungufu madogo madogo ila kwa asilimia kubwa ivyo ndio namna hiko chombo kinavyotakiwa kufanya kazi kuna watu awakuzoea kulipa kodi halali huko nyuma ndio msingi wa kelele.
Kwa hiyo Mkuu unapenda utawala wa "One Man Show"? Kila kitu aamue Rais? Ni ngumu sana kwa nchi kubwa kama TZ!! May be inaweza kuwa sababu ya kuuchokonoa moyo wake kwa miaka 5 tu ya kwanza, huwezi ukabeba matatizo ya watanzania yote kwenye moyo mmoja!! Ila nakumbuka alisema analala na mafaili kitandani, which is not healthy!! Haijalishi watu wako wapo corrupt/wazembe kiasi gani lazima uwe na watu katika hao uwaamini na wakusaidie, atayezingua nawe unamzingua
 
Mimi namshangaa Balile anajificha kwenye kichaka cha deni la taifa kukua! Je anataka kutuaminisha kuwa JPM na IMF&WB walimkopesha pesa kama maandazi! Kwanza ndo kipindi ambacho walikuwa wanakuja kumuona zaidi kuliko kipindi chechote,

Unakopesheka kama unauwezo ufatao:.

•Unauwezo wa kulipa hapa wanaangalia ukuaji wako wa kiuchumi sio kulingana na wewe kuwapa taarifa tu ila kulingana na uchunguzi wao!

•Kulingana na uwezo wako wa kusimamia miradi kutokana na mkopo huo na hilo waliliona kwa JPM maana alikopa na vitu vikafanyika kwa kuonekana mfano kama serkali ilikopa kwaajili ya kusamabaza umeme kweli umeme ulisambazwa, na pia kama ni vituo vya afya kweli vilijengwa, kama ni fly over kweli zilionekana! Hapa unadeliver matokeo ya mkopo so unaaminika kwa mtoa pesa,

•Uwezo wako wa kupambana na rushwa hapa ikumbukwe wakati wa JPM Tanzania ilipanda katika viwango vya nchi zilizopambana na rushwa.

Hapa Mr Balile nchi kukopa sio shida ila uwezo wako wa kutoa matokeo ndo jambo la msingi! Miaka yote nchi hii imekuwa na stendi kama mazizi ya ng'ombe lakini JPM ameleta transformation kubwa sana kwenye stendi zetu ndo maana unaweza kuona hata leo stendi kila kona ya nchi zinajengwa!

Niwakumbushe IMF na WB hawajawi hela kama njugu! Wanavigezo ndo maana hata Rais Samia juzi alisema hizi hela za UVICO nikipimo kwa serkali yake!
Magufuli alikuwa anakopa kinyemela na kuna kipindi alikuwa black listed na WB kuwa amevuka threshold. Amekopa sana AfDB na commercial banks kama StanChart na Credit Suisse.
 
Kwa hiyo Mkuu unapenda utawala wa "One Man Show"? Kila kitu aamue Rais? Ni ngumu sana kwa nchi kubwa kama TZ!! May be inaweza kuwa sababu ya kuuchokonoa moyo wake kwa miaka 5 tu ya kwanza, huwezi ukabeba matatizo ya watanzania yote kwenye moyo mmoja!! Ila nakumbuka alisema analala na mafaili kitandani, which is not healthy!! Haijalishi watu wako wapo corrupt/wazembe kiasi gani lazima uwe na watu katika hao uwaamini na wakusaidie, atayezingua nawe unamzingua
Raisi kuwa mahala pote kwa wakati mmoja aliwezekani na Magufuli hakuwa ‘one man show’ it’s just a label ya watu ambao hawakuzoea kusimamiwa.

Boss ndio mwenye mamlaka ya ku set agenda (pamoja na ilani ya chama) kwa maana hiyo anaweza amua namna kazi itakavyofanyika kufikia malengo.

Tatizo huo ulikuwa ni utaratibu mpya wa uwajibikaji ambao watu serikalini awakuzoea na kwenye chama watu kutotaka reforms.

But otherwise pamoja na mapungufu yake Magufuli alikuwa anaipeleka nchi kwenye right direction.

Anyway asubuhi njema.
 
Ni aheri deni lipae ila vitu viwe vinaonekana wazi, hebu tunakanyaga lami za kueleweka na barabara za kiwango cha zege mpaka mitaani! Wakati unalalamika kutendwa na Magufuli mkoonduh wako unapepea kuelekea ulipojenga Mbezi Kibanda Cha mkaa kupitia barabara 6 za lami huku ukipaa toka kwenye kijazi interchange.

Je, unakumbuka ni kero kiasi gani ulizipata kwa kukaa masaa zaidi ya 2 kuvuka tu eneo la Ubungo maziwa mpaka ubungo maji tokana na msuko suko wa magari?
Ila watanzania mna ujinga Sana sijui ni madhara ya elimu tunayopata Hadi tunAshindwa kutafuta taarifa.

Barabara za lami na mataa unayoyaona mitaani kwenye majiji yote Ni mradi wa Dar metropolitan project , huu mradi aliusaini kikwete na unaenda kuisha mwaka 2022. Ni pesa za world bank. Sijui kwanini sifa mnampa Magufuli peke Yake. Ingia hapa world usome mwenyewe. Development Projects : Dar es Salaam Metropolitan Development Project - P123134

Sipingi uchapakazi wa Magufuli ila tuache kupotosha.

Mradi wa umeme vijijini kikwete aliuacha ukiwa unakuwa financed na MCC PROJECT ya Marekani na lengo ilikuwa vijiji vyote viwe na umeme mpaka 2020. Ila Magufuli alipokonywa huo mradi wa MCC na Marekani, leo tunakatwa hela za REA kila tukinunua Luku.


Daraja la Ubungo upembuzi yakinifu na mkopo wa pesa zake umeanza kuanzia kipindi Cha kikwete. Naomba uchukue muda kusoma hii article TANROADS – Ubungo Interchange – Dar es Salaam
 
Nafikiri alikopa kulingana pia na uwezo wa nchi! Unajua ukuaji wa uchumi ndo uwezo wa kukopesheka pia! Na utambue miaka yote tumekopa lakini kilichokuwa kinafanyika cha maana hakikuwepo! Ila kwa vile wote mmegeuka wakosoaji wa Maguguli ili kumlinda mama! Mwambie apambane asisingizie Madeni hata Marekani wanamadeni ya kutisha!
Hoja ya kipuuzi kabisa! Unasema miaka uote hakuna kilichofanyika! Nini kikubwa cha pekee kikubwa alichofanya marehemu ambacho kilikuwa hakijafanyika?
 
Back
Top Bottom