Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Mleta mada popote ulipo wewe ni mjinga na mnafiki wa kiwango Cha SGR.
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki?

Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.

Kipi kimekamilika?
 
Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
Asante sana umemswalika vizuri.
 
Balile ndio napo muonaga anapenda kujisifu kwa ujinga, cheap popularity, ana ujinga fulani wa asili Balile, hasa hapo aliposema eti yeye ndio alisema Katiba inasema nn baada ya Rais aliyeko madarakani kufariki, yaani eti watu wengine walikuwa hawajui ila yeye ndio alisema katiba inasemaje, yaani yeye Balile ndio alitamka Makamu wa Rais ndio atakuwa Rais kama katiba inavyosema, na wengine walikuwa hawajui katiba inasemaje, hapa kaandika ujinga wake wa asili wa kwao huko, everyone is stupid kwa degree fulani.

Balile alikuwa Pro Magufuli sanaaa akiwa hai, iweje asisema akiwa hai huu uozo wa mikopo ya hovyo na riba hatari hivi, hadi amekufa ndio kaandika, na data zilikuwepo, huu ni unafiki mbaya sana, Balile ni mnafiki sana, hapa anajionyesha kwa Mama Samia yeye ndio mzuri sanaa, subiri Mama Samia amalize muda wake, huyu huyu Balile atamuandika Mama Samia vibaya sana, ndio tabia ya watu wanafiki, hypocrite and stupid Balile.

Let's go back kwa mikopo mikubwa ya siri na hatari kabisa ya JPM.

Kiukweli kabisa, JPM aliharibu sana kwa mikopo mikubwa ya riba ya kibiashara kwa siri kabisa. Hata matumizi ya mikopo mikubwa hiyo kwa riba za kibiashara ilikuwa siri sana. Alituaminisha ni hela zetu wenyewe mara zote, kumbe ni uongo kabisa.

Kwa hili JPM katukaanga na kipindi kifupi 5yrs kakopa trillions 29 nyingi sana sanaa kwa siri na riba kubwa sana. This is crime aisee
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Balile ni mnafiki sanaaa.kila kukicha alikua anampamba jiwe, leo kafa anajifanya kidume
 
Nafikiri alikopa kulingana pia na uwezo wa nchi! Unajua ukuaji wa uchumi ndo uwezo wa kukopesheka pia! Na utambue miaka yote tumekopa lakini kilichokuwa kinafanyika cha maana hakikuwepo! Ila kwa vile wote mmegeuka wakosoaji wa Maguguli ili kumlinda mama! Mwambie apambane asisingizie Madeni hata Marekani wanamadeni ya kutisha!
Kinacho zungumziwa ni ule uongo wake eti ni hela ya ndani
 
Sema uwanja ubadirishwe matumizi!

Maana lengo la uwanja kujengwa ilikuwa uwe wa safari za kawaida za ndege na ATCL walikuwa wameshaanzisha root , unapokuja kubadirisha matumizi Hilo ni suala lingine Sasa.

Halafu nani kakwambia miradi ya Jeshi Kama uwanja wa ndege huo ujengwe na kila kampuni. Unajua sensitivity ya uwanja Wa ndege wa kijeshi?


Unadhani Jeshi ni Kama kula unaamua tu

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Kama tunaweza kutumia ule wa kiraia wa Mwanza tunashindwaje kuutumia wa chato ambao umejificha kwenye macho ya wageni lakini bado unaweza kutumika kwa malengo yote mawili Kama ulivyo wa Mwanza kwa sasa.
 
Nani alikuambia kujenga miondombinu ndio kunakuza uchumi kiasi cha kulipa madeni makubwa? Mbona miondombinu imejengwa tangu uhuru na madeni yamezidi kuongezeka?
Ni swala la muda tutajua ukweli. Ila mtoa mada be fair usilete hoja zisizo na mashiko. Hata wakati JPM nchi ilipopokea mkopo ilikuwa ikitangazwa. Pili Deni aliliorithi JPM lilikuwa kwa kasi sana maana lilikuwa limeiva JPM focus ilikuwa si kulipa deni kwanza bali ilikuwa ni kujenga uwezo wa ndani ilituweze kulipa madeni. Miundombinu ilijengwa ililenga kukuza uchumi wa taifa ili siku zijazo liwe na uwezo kulipa madeni yake. Kumbuka Kenya walipofikia yaani wanakopa hela ili kulipa deni.
 
And alikuwa anakopa kwa siri as if hiyo hela angelipa kutoka mifukoni mwake, akiwa majukwaani anawatukana mabeberu, Usiku anawapigia simu kuwakopa hela!! Trl 29 kwa miaka 5 ni nyingi sana, and sijui kafanyia nini hiyo hela, maana mamiradi yake yote yapo under 50% ya utekelezaji
Achane upuuzi hakuna siri wala ajabu unakopa kufanya vitu vya maana sio unakopa kupambana na korona ambayo haIpo.
Under 50%??? leteni janja janja huyo Bi. Hangaya tutamnyoosha
 
Mkuu 50% ya project ni kubwa! Sema unachuki na JPM ndo maana hauoni alichofanya JPM hakujipendekeza kwao walikuja wenyewe baada ya kuona mziki wake! Angalia project kama zifuatazo
•Tanzania haikuwahi kuw ana Radar tokea uhuru amejenga nne kwa mkupuo Dar,mwanza,mbeya na klimanjaro
•Tanzania haikuwahi kuwa na Mahakama zakisasa tokea uhuru mahakama standard zilikuwa ni zile za kanda! Leo tunazungumzia mahaka zenye miundombinu ya kisasa!
•Nchi hii ilikuwa na hospital kubwa za kanda nyinhi za mashirika ya dini leo hii tuna hospital kubwa za hadhi ya kitaifa kule Musoma, mtwara,mbeya n.k Wao waliopita hawakufanya haya si kwa kuwa hawakuweza tu bali hata utendaji wao haukuwa katika viwango vya JPM!
•Vituo vya afya,hospital za wilaya, masoko.
•Uanzishwaji wa masoko ya madini mfano soko la dhahabu Geita limeinbiza takribani trilion tatu kwa miaka miwili na nusu!
•Upanuzi wa bandari hapo Dar, mtwara ma tanga!
•Ufufuami wa treni kutokea Dar mpaka moshi/arusha!
•Ujenzi wa flyover,busisi,mto wami n.k

Hayo ni ambo yanahitami usimamizi na fedha kwa hiyo kama matokeo yanaonekana kukopa kwake hakuna shida! Hata nyumbani kwako ukikopa benki ili ujenge nyumba na ukajenga kwa ubora na ikaonekana hakuna mtu atakaye kulaum! Ila kwa vile mmezoea maneno sio utendaji endeleeni kumsifia huyu mama ambaye hana hata historia ya utendaji kwenye maisha yake, kitu pekee kimemfikisha hapo ni kubebwa na siasa!

Ingefaa kila kimoja uandike na fedha iliyotumika tuone tumepigwa au la
 
Hizo hospital za kanda unazoengelea ulishawahi kuzitembelea au unaziona kwenye picha,
Majengo yake ni uchafu mtupu, je kuna huduma gani za maana katika majengo hayo?.
Mbona mbeya alishindwa kuifanya iwe kama Bugando,Kcmc na Muhimbili?.
Tumekulia maisha ya umaskini hivyo hudhani gorofa/jengo ndiyo kiwango cha huduma.
Jamaa vitu vyake vyote alivyovifanya uongo ulikuwa mwingi sana, wala hakuwa na uchungu na fedha ya nchi yetu bali aliangalia kuufurahisha moyo wake uliojaa maisha ya sifa.
Kama unakiri majengo yapo Tena mazuri tupige hatua ya pili,ya tatu na baadae tuwe na Huduma Bora. Ulitaka x-ray zikafungwe kwenye miti? Tunaanza na miundo mbinu Kwanza tukishindwa kumalizia Ni ujinga wa Magufuli au Ni ujinga wetu!
 
Hoja ya kipuuzi kabisa! Unasema miaka uote hakuna kilichofanyika! Nini kikubwa cha pekee kikubwa alichofanya marehemu ambacho kilikuwa hakijafanyika?
Ka,Uliza maswali sensible bwana! In kingai voice.com
 
Wanafiki hawataingia mbinguni.
Huyu mpumbavu sana! Anajua Tanzania inaingiza shilingi ngapi kwa mwaka? Huo mradi wa SGR unacost shilingi ngapi ambazo serikali yetu isineweza kugharamia? Hivi Duniani swala la kukopa nalo ni la kushangaaa? Hata yeye mwenyew akiangalia huo uzi wake kila Raisi aliyeingia madarakani alichangia kuongeza deni.

Yaani huu uzi umejaa upumbavu mtupu.
 
  • Nzuri
Reactions: 1gb
Nani alikuambia kujenga miondombinu ndio kunakuza uchumi kiasi cha kulipa madeni makubwa? Mbona miondombinu imejengwa tangu uhuru na madeni yamezidi kuongezeka?

Mkuu Samahani Nikuulize Vitu Gani Vinafanya Uchumi Ukue Ukitoa Hiyo Miundombinu Unayo Ikataa.
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki?

Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.
Sijui kama umeelewa mada. Kama umeelewa basi unatatizo kubwa
 
Back
Top Bottom